Mwenye taarifa ya Dr Harrison Mwakyembe

samilakadunda

JF-Expert Member
Oct 13, 2011
1,780
354
Wadau tunaomba kujuzwa juu ya hali ya Dr mwakiembe ambaye alisafirishwa hivi karibuni kwenda india kwamatibu.MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU MBARIKI DR MWAKIEMBE.
 
Nimesoma thread moja inamuonesha amepiga picha na wafanyakazi wa hospitali huko anakougulia; wanasema anaendelea vizuri ingawa hawasemi kama diagnosis ya maradhi yake kama imetibitisha kulishwa sumu au au mambo mengine!!
 
Sio Dr Halison Mwakiembe, ni Dkt Harisson Mwakyembe!

Unajua ukiangalia haya mambo kijuu juu it's fine typo! Lakini kama taifa kuna kila dalili tuna tatizo kubwa mno kwenye suala zima la kusoma na kuandika correctly. Copy and paste bado zinatushinda. Nikikumbuka kisa cha babu wa Loliondo kila siku alikuwa anapewa majina mapya na vyombo vya habari!!!!!! Nimeshaziona humu JF breed badala ya bleed, flame badala ya frame, Ripumba, lushwa, halaka halaka haina balaka you name it!!!!!!!
 
Unajua ukiangalia haya mambo kijuu juu it's fine typo! Lakini kama taifa kuna kila dalili tuna tatizo kubwa mno kwenye suala zima la kusoma na kuandika correctly. Copy and paste bado zinatushinda. Nikikumbuka kisa cha babu wa Loliondo kila siku alikuwa anapewa majina mapya na vyombo vya habari!!!!!! Nimeshaziona humu JF breed badala ya breed, flame badala ya frame, Ripumba, lushwa, halaka halaka haina balaka you name it!!!!!!!

Shule za vodafasta mkuu...

Janga la kitaifa
 
Shule za vodafasta mkuu...

Janga la kitaifa

Mkuu siyo utani unajua it's shocking angalia kama hii comment nimeikuta mwananchi:

#7 Mizzambi ya Meazza 2011-10-17 02:57
WAlioba, Kingunge na Butiku kauli zenu kuhusu vijana ni za kikomunisti na hazina hekima kabisaa.Unaposema vijana wawajibike una maana gani wewe bujiku na wenzako?Vijana wa kitanzania ndio waliopata malezi machafu sana kupita vijana wote barani africa. Walinyimwa haki miliki katika miziki yao! walinyimwa uhuru wa kuongea kiingereza!Hawa kuwa na TV na hivyo kujifunza mengi ya dunia!Walifukuz iwa makocha wao wa soka Tambwe Leya na Kamara mwaka 1976 na waziri wa michezo wakati huo Sarakikya!Vija walilazimishwa kuimba kwaya, kucheza chipukizi na ngonjeea za kuwapamba wanasiasa! Ni wapi hapa africa ulikuta vijana wanafanyishwa mambo kama hayo? Leo hii vijana wa kenya, Uganda, zambia na malawi wanachukua kazi za watanzania kwa sababu ya kujua kiingereza.Vijana wa kitanzania wamejazana Nairobi kuuza mitumba tuu! Sasa mnaposema kuwa vijana wawajibike mna maana gani? Badala ya kuzipamba nchi tajiri ili vijana wetu wapate soko la soka la kulipwa huko kwao nyie ndio kwanzaa mnawatukana ili kujipendekeza kwa mataifa ya kiarabu.Ghana, zaire, Ivory cost, zambia, nIgeria na cameroo vijana wao wamepata ajira katika nchi zote za ulaya na Israel. Israel ndiko kuna waghana utadhani ndio kwao.Vijana kama kina ngasa, ulimwengu Thomas na wengine wanawajibika na kujituma ili wawe wachezaji wa kulipwwwa. Sasa sera zenu za kuichukia Israel hadhalani ndio hiyoo ina wakomoa vijana wetu. Tazaman mabutu alivyo walea vijana wake.Ni matajiri kimuziki, kisoka na mpira wa vikapu ambapo wamepata ajira na masoko duniani kote. Kueni na kuamini Injiri!

Who the heck is that Walioba? Inakuwaje jina maarufu linaloandikwa magazetini karibu kila siku linakosewa kwa mtindo ule wa kumix "r" and "l"?????? Kiurahisi kabisa ungeweza kusema ni typo! lakini vipi na hayo maneno mengine? Kweli kuna janga la kitaifa.
 
Mkuu siyo utani unajua it's shocking angalia kama hii comment nimeikuta mwananchi:

Who the heck is that Walioba? Inakuwaje jina maarufu linaloandikwa magazetini karibu kila siku linakosewa kwa mtindo ule wa kumix "r" and "l"?????? Kiurahisi kabisa ungeweza kusema ni typo! lakini vipi na hayo maneno mengine? Kweli kuna janga la kitaifa.
Mkuu umenigusa sana,hii ni dalili ya janga lingine kwa vijana! Mimi mwenyewe huwa nakereka sana.siku hizi elimu za awali kama msingi mtoto akirudi anakwambia "good morning father" unashangilia! Zamani kulikuwa na msisito wa hati na kuandika kwa usahihi maneno.ukiwa na hati chafu unaandikia penseli hadi ukome na rula za mikono huku ukiona aibu wenzio wameruhusiwa kutumia peni.unaweza kutumiwa sms na dogo wa form 3 ukachanganyikiwa kabisa tena na hivi vifupi vyao wanavyotumia wanajisahau wanaviweka hadi kwenye mitihani na unakuta mwl kaweka tiki! Hizo ripoti zitazokuwa zinaandikwa na hawa lazima uwe na sharobaro pembeni akusaidie kufafanua!
 
Yaani unajua mkuu nikikumbuka enzi zile hata mtoto wa darasa la tatu asingeweza kuandika walioba, na tena kama alijijua kwamba ana tatizo la l, r lazima angeuliza kwanza. Kama ulivyoelezea hapo ule mchaka mchaka wa darasa la kwanza na la pili ilikuwa hukatizi bila kuzielewa herufi zinavyoandikwa na kutamkwa.

Nimetolea mfano mara nyingi sana hapa wa watu ambao siku zote hutamka s badala ya z, lakini hata siku moja huwezi kukuta ameandika "mesa" au "sulia" au hiyo ilikuwa ni "samani sana". Inaonyesha wazi kuna bonge la carelessness katika elimu yetu ya msingi.
 
  • Thanks
Reactions: Ame

habari ya mwakyembe mnaiua?
 
wakati anatoka huku alikuwa anaweza kutembea, anaongea, ila mwili ulikuwa umevimba....hiy picha ya jana anaonekana amethoofika, mwili bado umevimba.....bado anaumwa
 
Hii post ipo somewhere humu JF, kuna tatizo ndugu zangu lazima tukiri!!!!!!! And something need to be done now!!!!!!!!

Mimi ni mshabiki mkubwa wa soka ya hapa Tanzania hali kadharika kutokana na utandawazi uliopo sasa na napenda pia soka ya nje ya Tanzania. Lakini kubwa nimekuwa nikifatilia kwa ukaribu mwenendo wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars). Kwa maoni yangu sielewi hasa kile wenzetu walipopewa dhamana ya kuendesha michezo nchini ikiwemo soka kama wanajua wanachokifanya. Tumekuwa wepesi wa kutamani mafanikio bila kuyatokea jasho. maneno mengi yanazungumzwa na viongozi wa vyama vya soka kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa hadi taifa kuwa eti soka ya Tanzania imekuwa, mimi nasema hapana imeshuka tena kwa kasi kubwa ni kama gari iliyoshindwa kupanda mlima ikarudi nyuma.

Kwa maoni yangu hebu watanzania tuamke na tuwe serious na kile tunachotamani kufanikiwa nacho. Katika soka msingi wa mafanikio ni mipango ya kuandaa timu za watoto na vijana ambao mwishowe ndio hao huingia timu ya taifa. Siamini katika kubadirisha makocha kama nguo kuwa ndio suluhu. Hapa hata tungeletewa Sir Alex Furgeson, Jose Morinho au Carlo Ancelloti hakuna kipya kwani tatizo ni msingi mbovu. Karibu 80% ya wachezaji waliopo sasa katika timu a taifa ni wachezaji wasio na uwezo na kasi ya kucheza mpira wa sasa. Bila kubadirisha mitazamo yetu ili kujenga msingi imara na endelevu taifa stars itaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu kama alivyowahi kusea raisi mstaafu wa awamu ya pili alhaji Ali HAsani Mwinyi kila mtu anajifunzia kunyoa kwetu. Naongea hili kama mtanzania ninayekerwa na hali ya timu yetu ya taifa. Viongozi wabadirike na kuwa na mtazamo chanya. Sasa hivi dunia imekuwa kama kijiji habari na mamb mbali mbali tunayapata kwa urahisi. Inashamgaza sana licha ya sasa hivi taifa stars kuwa na wafadhili wengi na wanaotoa fedha nyingi timu inadorora kila uchao. Miaka ya 80 ambapo suala la timu ya taifa walitupiwa FAT bado mpira ulionekana kiasi cha timu kukata tiketi kucheza mashindano ya Afrika.

Tusipoamka wenyewe hakuna atakayekuja kutuamsha tutabaki kubadirisha makocha tukidhani wao ndio wanaocheza mpira na kuleta mafanikio......naishi hapa kwa leo hebu tujadili wapenda soka.
 
Mnafundishana lugha sasa
wkt wananchi tunataka kujua hali ya Dr.
 
Mkuu umenigusa sana,hii ni dalili ya janga lingine kwa vijana! Mimi mwenyewe huwa nakereka sana.siku hizi elimu za awali kama msingi mtoto akirudi anakwambia "good morning father" unashangilia! Zamani kulikuwa na msisito wa hati na kuandika kwa usahihi maneno.ukiwa na hati chafu unaandikia penseli hadi ukome na rula za mikono huku ukiona aibu wenzio wameruhusiwa kutumia peni.unaweza kutumiwa sms na dogo wa form 3 ukachanganyikiwa kabisa tena na hivi vifupi vyao wanavyotumia wanajisahau wanaviweka hadi kwenye mitihani na unakuta mwl kaweka tiki! Hizo ripoti zitazokuwa zinaandikwa na hawa lazima uwe na sharobaro pembeni akusaidie kufafanua!

Hahahahahahahahahahahahahahahahaaaaaa kaka umeuaaaaaaaaaa, Kiswahili kingine fasaha hadi balaaa. Sasa na hiyo ni typo au Maana duh. Ulimaanisha Msisitizo au Msisito ni neno linalojitegemea? Maana kwa kikwetu umetukana mwana.
 
Unajua ukiangalia haya mambo kijuu juu it's fine typo! Lakini kama taifa kuna kila dalili tuna tatizo kubwa mno kwenye suala zima la kusoma na kuandika correctly. Copy and paste bado zinatushinda. Nikikumbuka kisa cha babu wa Loliondo kila siku alikuwa anapewa majina mapya na vyombo vya habari!!!!!! Nimeshaziona humu JF breed badala ya bleed, flame badala ya frame, Ripumba, lushwa, halaka halaka haina balaka you name it!!!!!!!
Wala siyo error typing ni kutokuwa makini. Watanzania wengi hawako makini kwenye vitu vingi, kitu kama jina wanaona ni kitu cha kawaida. Lakini kukosea jina ni kosa kubwa sana. Halafu huu ni uwanja wa great thinkers, hata kucopy na kupaste jina nayo kazi. Au ndo kwenda kinyume na ujumbe wa Invisible , ''Ficha Upumbavu na wala siyo werevu'' ? . Mi naona hapo ni kuanika upumbavu wako ambao umeuzidi werevu.
 
Back
Top Bottom