Mwenge wa uhuru;Kusahaurika kwa tafsiri/maana yake na umuhimu

Panzermeyer

JF-Expert Member
Jan 21, 2016
471
325
Habari wakuu wote wa JF. Nimekaa nikafikiri na nikagundua kua, shughuli zoote ( kama mbio za mwenge ) pamoja na mwenge wenye, siku hizi zimepoteza tafsiri yake na umuhimu wake kabisaaa. Somo la urai lilitoa tafsiri kadhaa za mwenge, zikiwemo

· Kumurika maadui wote, wa nje na ndani ya Tanzania

Maadui hao ( maadui wa ndani ) ni kama, wahujumu uchumi, wala rushwa, wapinga maendeleo, wapinga mapinduzi. Maadui wengine ( maadui wa nje ) ni kama, mabeberu na wanyonya uchumi wa nchi, maadui wa kisiasa nk. Ukweli dhahiri na usiopingika ni kua, nchi yetu au taifa hili kwasasa linakumbatia maadui wengi sana kwenye ilo kundi la kwanza, wapo wengi sana kiasi cha kusikisha, mbaya zaidi ni kua wanajulikana na bado wanalindwa na serikali kwa kutoshughulikiwa kwa hatua zozote za kisheria kutochukuliwa zaidi yao. Kundi la pili la maadui, ndo wale wanaotuchezea kiini macho, wanatuletea chandarua alfu wanaingilia mlango wa nyuma kwenda kuchukua vito vyetu vya thamani.

Inauma sana kumuna adui ( mwizi ) alfu ukampigia kelele ( ukammulika ), ili wale wenye mamlaka wakusaidie kumchukulia hatua, ila inakua kinyume chake, wao ( wenye mamlaka ) wanakugeukia wewe, wanakushangaa, kisha wanakunyamazisha.

· Kuleta matumaini pale raia au watu wanapoonyesha kukata tamaa

Ilitakiwa iwe kwamba, tukiiangalia serikali yetu na utendaji wetu, tunapata matumaini, faraja na ujasiri wa kupigania maendeleo, lakini leo hii, tunaiangalia serikali, na taswira inayopatikana ni kama ya mtumwa anayemwangalia kabulu kwa jicho la hasira na chuki kali zisizo na kipimo.

- Gharama za maisha zimepanda sana

- Jitihada za mabadiriko ya katiba yetu ya viraka viraka ( yenye mabadiriko mengi mno ) zika rudishwa nyuma kabisa

- Dhuruma ya marudio ya uchaguzi wa zanzibar, na kupeana madaraka ya nchi bira kujali demokrasia, utawala wa sheria na kuheshimu sauti ( kula )za raia

Tumekua, kama vile mtu mwenye kiu, anavyotamania maji, lakini ghafla anakuja kugundua kua, yupo jangwani na anapoteza matumaini yoote ya kukata kiu yake.

· Kuleta hari ya maendeleo

Taifa limejaa rasimali za kutosha, zile za asili na rasimali watu. Kundi la kwanza la rasimali ndo linapewa kupaumbele kwa kutumiwa ipasavyo, lakini ni kwa manufaa ya watu wachache tu, Kundi la pili, ambalo ndo lingeweza kuleta hamasa ya amendeleo ikiwa ni pamoja na kuleta mwongozo wa kutumia vizuri kundi la kwanza na rasimali, lakini badala yake, kundi hili limepuuzwa.

- Mtu anamaliza chuo mwaka huu, lakini anakaa mtaani ata kwa muda wa miaka mitatu

- Upatikanaji wa kazi umekua mgumu kupindukia, mpaka watu wengine wasio na kazi pia wanaona ni sawa kuneemeka kwa shida za wengine. Mfano, post za kwenda jkt, mpaka matangazo feki yanasambazwa mitandaoni na watu wanarubuniwa fedha zao

HAKUNA JINSI, MAISHA LAZIMA YAENDELEE

Naomba tukumbushane zaidi maana/tafsiri za mwenge wa uhuru.
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Hakika "Mbio za mwenge" hazina maana tena labda kama maudhui na kauli mbiu ya kuendelea kufanyika kwa mbio hizo yatabadilishwa na kuwa "kuwasaka kwa udi na uvumba wahujumu uchumi wote; wezi, wala rushwa, mafisadi, majangili na wauza mihadarati na kuwatokomeza"!! Vinginevyo mbio za mwenge zitakuwa kipimo muhimu kwa umakini wa JPM katika juhudi zake za kuokoa fedha za umma! Japo katika miaka ya karibuni mbio hizo zilichukua sura ya kichama tawala zaidi kuliko utaifa; JPM anaweza kusubiri atwae mikoba ya Ccm kabla ya kuchukua hatua mahususi kuhusu mbio hizo; tusubiri tuone!
 
Hakika "Mbio za mwenge" hazina maana tena labda kama maudhui na kauli mbiu ya kuendelea kufanyika kwa mbio hizo yatabadilishwa na kuwa "kuwasaka kwa udi na uvumba wahujumu uchumi wote; wezi, wala rushwa, mafisadi, majangili na wauza mihadarati na kuwatokomeza"!! Vinginevyo mbio za mwenge zitakuwa kipimo muhimu kwa umakini wa JPM katika juhudi zake za kuokoa fedha za umma! Japo katika miaka ya karibuni mbio hizo zilichukua sura ya kichama tawala zaidi kuliko utaifa; JPM anaweza kusubiri atwae mikoba ya Ccm kabla ya kuchukua hatua mahususi kuhusu mbio hizo; tusubiri tuone!
Mkuu, naona tu serikali ifute tu izi mbio za mwenge maana makusudio yake hayatendewi kazi na badala yake wanaishia kuteketeza pesa za nchi
 
Back
Top Bottom