Mwenge ukiwashwa mbele ya wafanyakazi wa serikali na wanafunzi tu, maana yake nini?

frema120

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
5,099
1,338
nimeshangazwa sana kuona mwenge ukimwashwa na waziri mkuu leo mbeya, hukuwahudhuriaji wa sherehe hizo wakiwa wanafunzi na wafanyakazi wa serikali, nini tafsili yake wakuu..

SOURCE; mimi mwenyewe plus itv newz
 
Ndo watu ambao ni rahisi kuwalazimisha
Otherwise kwa watu wengine serikali haina maana
 
Yani mtu mwenye akili timamu unatalajia ahudhurie kusanyiko la kukimbiza moto? no way.
 
mimi nilisha usahau hata unavyofafana naona magari yakiwa speed na polisi wakiwa wametoa silaha za kivita sijui huwa wanaimanisha nini maana hata madini yetu hayalindwi namna hii..
 
He! kumbe mwenge wa nyerere bado upo?. Kila sehemu unapolala Umehusika sana kwenye kusambaza VVU.
 
nimeshangazwa sana kuona mwenge ukimwashwa na waziri mkuu leo mbeya, hukuwahudhuriaji wa sherehe hizo wakiwa wanafunzi na wafanyakazi wa serikali, nini tafsili yake wakuu..

SOURCE; mimi mwenyewe plus itv newz
Mkuu nimeshangaa sana kwa hali niliyo ikuta pale Sokoine nilikuwa na jamaa mmoja aliniuliza hivi kwa nini wasitumie utaratibu wao wa siku zote wa kusafisha watu toka maeneo mbalimbali ili waje wawashe mwenge wetu ....nilikosa jibu
 
Hakuna makitu nnayo yachukia km hayo sijui mibio ya Mwenge!! wala sioni tija yake, CCM walitutesa sana hasa wakati niko shule ya msingi, mnakwenda huko uwanjani mnatoka shuleni kwenu saa tatu asubuhi, mnaandamana na bendi uwanja upo km 4 toka shuleni kwenu. mkifika uwanjani hakuna kivuli jua ni kali, hakuna maji ya kunywa hakuna chakula, enzi zetu wazazi walikuwa hawakupi hata shilingi kwenda nayo shule mnakaa na kiu na njaa tupu, mnatafuta mpaka mnapata bomba linalotoa maji ndo mnakunywa yale maji si salama. Mgeni rasmi atafika saa nane mchana anawakuta mmeshanyong'onyea kwa njaa na kiu. akiingia mgeni rasmi basi mageti yote yanafungwa hakuna kusepa! Dah kweli CCM mlituweza, nikikumbuka huu ujinga sina hamu!!
 
Duh! mkuu umenikumbusha mbali sana na umeamusha hasira zangu upya dhidi ya CCM...Kesho pana mnada kijijini kwetu nitakuwa pale kumwaga elimu ya uraia kama sina akili nzuri vile.
 
nimeshangazwa sana kuona mwenge ukimwashwa na waziri mkuu leo mbeya, hukuwahudhuriaji wa sherehe hizo wakiwa wanafunzi na wafanyakazi wa serikali, nini tafsili yake wakuu..

SOURCE; mimi mwenyewe plus itv newz

Nadhani hata hayo makundi uliyoyakuta yalilazimishwa kwenda kuhudhuria sherehe hizo na zaidi ya hapo ingeweza kuwa aibu. Leo hii watu wanajiuliza Mwenge umekuwa na faida gani kwa watz? Cha msingi ambacho huwa nakiona ni ufunguzi wa miradi kitu ambacho chaweza fanywa na viongozi wa eneo husika au kwa kumualika mtu au kiongozi wamtakaye kufanya ufunguzi huo. Mwenge unakula mamilioni ya shilingi za walipishwa kodi pesa ambazo zingaliweza kutumika kwa manufaa mengine yenye kuonyesha matokeo chanya kwa wananchi kama vile mashule na maabara zake, hospitali na madaktari wa kutosha, madawa na vifaa vingine muhimu. Mwisho wa siku yawapasa waserikali wakae chini na ku
ona namna ya enzi huu mwenge kwa gharama zinazoendana na uchumi wetu leo hii
 
Yani mtu mwenye akili timamu unatalajia ahudhurie kusanyiko la kukimbiza moto? no way.
Heri ya hao wanaomkumbuka Nyerere na kumuenzi kuliko wale wa Arusha wakimsikiliza jamaa Le Totoz aliyevaa nepi akilia lia kuwa kila mtu na lwake
 
Kukimbiza moto na kueneza virusi vya ukimwi na kutumia pesa za walipa kodi kwa Mambo ya kipumbavu huko ndio kumuenzi Nyerere!!??....
 
Ze totoz mko wengi, usipokawekewa luku hako kaluwiluwi kako basi hutaelewa mpumbavu ni nani
 
Back
Top Bottom