Mwenge: Majambazi wawapora mzigo mzito (Mamillioni) Wachina kwenye foleni...

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,700
29,111
Vijana wa kazi wakiwa juu ya boda boda na silaha za kivita wavamia Noah ya wachina, na kuitoboa toboa na risasi kidogo kisha kunyakua mamillion ya wachina hao na kutokomea nayo kusiko julikana na kuwaacha wachina wamepagawa!

Wachina waonekana wakihaha na kuchanganyikiwa. Yote hayo yamejiri mwenge jioni hii.

Ukisafirisha hela usimnong'oneze hata mkeo, watu washajichokea maisha mda huu, wanakwapua chochote kilicho mbele yao.
 
bora, manake huo mzigo ulikuwa wa kwenda kuhamisha watu, nusu ya ardhi ya dsm na pwani nahisi imenunuliwa na wachina na wahindi.
 
Habari hii ni kweli ikizingatiwa kuwa lara 1 hajawahi kupost chochote hapa. Poleni sana wachina.
 
Last edited by a moderator:
Wapuuzi acha waibiwe tu, kuna watu wanafanya kazi za kusafirisha fedha, CIT, malipo kidogo tu na fedha zinakuwa salama, wakiibiwa CIT, unalipwa.
 
Back
Top Bottom