Mwenendo wa Kesi za EPA

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,422
911,172
Upelelezi dhidi ya kina Lukaza wahusisha Interpol


Na Benjamin Masese

KESI ya ya wizi wa mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu Tanzania (BoT) inayowakabili, Bw. Johnson Lukaza na
ndugu yake Mwesiga Lukaza iliendelea jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa upande wa mashtaka kueleza jinsi walivyofanya upelelezi.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya mwaka 2004/2005 walikula njama za kughushi nyaraka mbalimbali na kujipatia sh. bilioni 6 kwa njia ya udanganyifu kwa kutumia kampuni ya Changanyikeni Residential Complex Ltd ya Tanzania wakidai wanakusanya madeni ya kampuni ya Marubeni Corporation ya Japan.

Akitoa ushahidi huo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Salim Kisai alisema jopo la upelelezi lilianza kufanya kutafuta zilipo ofisi za Marubeni na kuzipata nchini Kenya, kwa kushirikiana na Polisi wa Kimataifa wa Interpol.

Alisema kuwa katika harakati za upelelezi huo walikutana na Meneja wa Tawi la Marubeni na kupitia nyaraka mbalimbali zinahusiana na BoT.

Bw. Kisai alisema kuwa baadhi ya nyaraka zilionekana kusainiwa na viongozi wa tawi la Marubeni la Kenya, lakini uongozi uliokuwepo ulimkana kiongozi aliyesaini malipo hayo pia kutotambua mihuri iliyokuwa imegongwa katika nyaraka hizo.

Hata hivyo alisema mihuri iliyotumika kugonga nyaraka hizo ilikuwa tofauti na nyaraka za BoT.

Vile vile alisema kuwa upelelezi uliendelea hadi nchini Japani palipo na makao makuu ya Marubeni na kufanya mazungumzo na mkurugenzi wa kampuni hiyo ya uwekezaji wa magari aina ya Nissan na kupata nyaraka mbalimbali zinazohusiana na kesi.

Mawakili wanaowatetea kina Lukaza walimtaka Bw. Kisai kuonesha nyaraka alizozipata Japani, naye akadai kwamba alishindwa kuondoka nazo kutokana na utaratibu wao kuwa tofauti na wa Tanzania.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena Machi 28, mwaka huu ili kuendelea na ushahidi.
 
Mwenendo kesi ya kina Maranda sasa wakamilika

Thursday, 24 March 2011 20:03 administrator



Na Mwandishi Wetu
UPANDE wa mashitaka na ule wa utetezi katika kesi ya wizi wa sh. bilioni 2.2 kupitia akaunti ya EPA, inayomkabili mfanyabiashara Rajabu Maranda na binamu yake, umekabidhiwa mwenendo wa shauri hilo. atua hiyo, inatokana na upande wa mashitaka kufunga ushahidi wao na hivyo pande zote kutakiwa kuandaa hoja za kisheria iwapo wanaona washitakiwa wana kesi ya kujibu au la. aranda na Farijala Hussein, wanaokabiliwa na mashitaka ya kughushi, kuwasiliasha hati za uongo, wizi wa sh. 660,210,000 na kujipatia ingizo la fedha la sh. 1,605,839,041.25.
Washitakiwa hao walipanda kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Ilvin Mugeta. pande wa Mashitaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Fredrick Manyanda, ulidai shauri hilo linakuja kwa kutajwa kwa ajili ya kuangalia iwapo mwenendo wa kesi hiyo upo tayari. akimu Mugeta alisema kuwa upo tayari ambapo upande wa mashitaka na ule wa utetezi ulipatiwa nakala za mwenendo huo.
Shauri hilo liliahirishwa hadi Aprili 4, mwaka huu, litakapotajwa ili kupangiwa tarehe ya pande hizo kuwasilisha hoja zao za kisheria kwa njia ya mdomo.
Washitakiwa hao wanadaiwa kujipatia fedha hizo kwa madai ya kwamba wao ni wabia wa Kampuni ya Money Planners & Consultants ambayo imepewa mamlaka ya kukusanya deni hilo na Kampuni ya B. Grancel & Company Limited ya Ujerumani.
 
Siri kashfa ya EPA hadharani
• Mnyika amwandikia barua Spika kutaka ufafanuzi

na Martin Malera, Dodoma


amka2.gif
WAKATI utata wa sh bilioni 135 zilizoibwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), unaendelea kuligubika taifa, imebainika kuwa serikali imeamua kulibeba deni hilo na kuliingiza katika deni la taifa.
Chini ya utaratibu huo, serikali italilipa deni hilo kwa riba na hadi deni hilo litakapo iva, serikali italazimika kulipa sh bilioni 230 badala ya sh bilioni 137.7 zilizoibwa na wajanja.
Hali hiyo imebainishwa katika taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ripoti yake ya fedha za Serikali Kuu kwa mwaka ulioishia Juni 30 2009, fungu 22 kuhusu deni la taifa na matumizi mengine ya taifa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, serikali imebadilisha deni katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) la sh bilioni 137.7 kuwa dhamana ya serikali zitakazolipwa kwa riba ya kiwango cha sh bilioni 11.50 katika kipindi cha miaka 20 kilichopitishwa .
Kwa hali hiyo, deni lote ambalo linapaswa kulipwa na serikali kwa riba litafikia sh bilioni 230, hivyo kulifanya taifa kubeba deni la EPA.
Hatua hiyo ambayo inazidisha mzigo wa madeni kwa serikali, imemfanya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, kumwandikia barua Spika wa Bunge, Anne Makinda akitaka ufafanuzi juu ya wizi wa EPA, kupitia Kampuni ya Kagoda.
"Mheshimiwa Spika, haya yanafanyika bila Bunge lako kushirikishwa kwa ukamilifu ikiwemo kutaarifiwa makampuni ambayo yamerejesha fedha za EPA, kiasi kilichorejeshwa kwa kila kampuni na orodha ya makampuni ambayo hayajarejesha pamoja na wamiliki wake, mojawapo ya makampuni hayo ikiwa ni Kagoda," alisema Mnyika.
Kabla ya kufikia uamuzi wa kulibeba deni hilo, serikali iliunda tume ya watu watatu kuchunguza na kubaini wezi wa fedha hizo na kuzirejesha bila kufikishwa mahakamani. Hata hivyo taarifa ya tume hiyo iliyoongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, imebaki kuwa siri, kwani haijulikani watuhumiwa gani wamerejesha, kiasi cha pesa kilichopatika na kiasi cha fedha kilichobaki mikononi mwa watuhumiwa wengine.
Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima kuhusiana na hatua hiyo ya serikali kuingiza fedha za wizi wa EPA katika deni la taifa, ndio uliosababisha Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, kuuliza swali bungeni.
Mnyika akiuliza swali la nyongeza juzi, alitaka kujua uchunguzi wa wizi wa fedha za EPA kupitia Kampuni ya Kagoda, umefikia wapi.
Lakini wakati akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe, alijibu kwa kifupi sana kwamba serikali bado inaendelea na uchunguzi wa tuhuma dhidi ya kampuni hiyo.
Hata hivyo uchunguzi zaidi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa Mnyika amemwandikia barua Spika wa Bunge, Anne Makinda, akieleza kutoridhishwa kwake na majibu ya Waziri Chikawe kuhusu uchunguzi juu ya Kampuni ya Kagoda ilivyohusika na wizi wa fedha za EPA.
"Utakumbuka kwamba katika mkutano wa tatu wa Bunge, kikao cha kwanza, Aprili 5 mwaka huu, niliuliza swali la nyongeza kutokana na swali la msingi namba nne kwa Ofisi ya Rais (Utawala Bora).
"Katika swali hilo nilihoji serikali itoe kauli kuhusu hatua zilizochukuliwa kuhusiana na Kampuni ya Kagoda Agricultural Limited na kukumbusha kwamba serikali imekuwa ikitoa ahadi za mara kwa mara bungeni kuwa uchunguzi unaendelea kwa kushirikiana na vyombo vya kimataifa. Niliuliza ni lini uchunguzi huo utakamilika?
"Katika majibu yake, waziri alitoa jibu fupi kwamba uchunguzi bado unaendelea, bila kutoa majibu ya ukamilifu kama Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la 2007) kifungu 46 (1), kinavyohitaji," alisema.
Mnyika alisema kwa ajili hiyo, anaomba kuwasilisha maelezo yafuatayo bungeni kwa mujibu wa kanuni ya 50 na ya 28 ili kuitaka serikali kutoa majibu ya ukamilifu kwa kuwa miaka takriban mitatu imepita toka uchunguzi husika uanze.
Ikumbukwe kwamba Kagoda inatuhumiwa kuchota jumla ya dola za Marekani 30,732,658.82 (sh 40 bilioni) katika Akanuti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya BoT.
Fedha hizi na nyingine zipatazo sh bil. 73 zilichotwa katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.
Serikali imekuwa ikitoa kauli za kujichanganya kuhusu ufisadi wa Kagoda. Mathalani Septemba 15, 2006, Waziri wa Fedha wakati huo, Zakia Meghji, aliwaandikia wakaguzi wa hesabu wa Kampuni ya Deloitte & Touche ya Afrika Kusini akisema, fedha za Kagoda zilitumika kwa "kazi za usalama wa taifa."
Nyaraka mbalimbali, zinaonyesha kuwa cheti cha usajili wa Kagoda Na. 54040 kilichotolewa na Ofisi ya Wakala wa Usajili wa Leseni za Biashara na Makampuni (BRELA), kinaonyesha Kagoda ilisajiliwa Septemba 29, 2005 na waliohusika kuisajili wanatajwa kwa majina.
Hadi sasa siri za ufisadi wa kampuni hiyo na kampuni nyingine zilizohusika na wizi wa fedha za EPA zimebaki kwa Rais Jakaya Kikwete, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, Mkurugezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hoseah na Johnson Mwanyika, ambao walikuwa wajumbe wa Kamati Maalumu ya Rais ya kufuatilia walioiba benki.
 
Fedha za EPA zilikuwa mzigo NBC-Shahidi Send to a friend Thursday, 14 April 2011 21:07

Tausi Ally
MFANYAKAZI wa Benki ya NBC, Lyson Mwakapenda (67), ameieleza Mahakama kuwa benki hiyo, ilizirejesha fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), baada ya kuziona kuwa ni mzigo kufuatia kitendo cha kukaa nazo kwa kipindi kirefu.

Mwakapenda alikuwa akitoa ushahidi wake mbele ya jopo la mahakimu watatu linaloongozwa na Jaji Beatrice Mutungi, katika kesi ya wizi wa Sh2.2 bilioni za EPA, inayowakabili wakurugenzi wa Kampuni ya Njake Hotel &Tours, Jonathan Munisi na Japhet Lema.
Katika ushahidi huo alioutoa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, Mwakapenda, alidai kuwa yeye ndiye aliyesimamia malimbikizo ya fedha za EPA, yaliyotokana na fedha za kigeni zilizolipwa na wafanyabiashara walioangiza bidhaa zao kutoka nje ya nchi.

Alidai kuwa baada ya uhaba wa fedha za kigeni,Benki ya NBC ililazimika kufungua akaunti hiyo ya EPA.Aliendelea kudai kuwa Benki ya NBC ilikaa na fedha hizo kwa kipindi kirefu kiasi cha kuonekana kuwa ni mzingo na hivyo NBC iliamua kuzirejesha BoT baada ya Hazina na BoT, kukubaliana kuhusu kuhamisha fedha hizo kutoka katika matawi ya NBC kwenda kwenye akaunti ya EPA.

Alidai kuwa NBC, ilikuwa inafanya kazi hiyo kwa maelekezo kutoka BoT. Baada ya kumaliza ushahidi huo, Wakili wa Serikali Alapha Msafiri, alidai kuwa shahidi wanayemtarajia kuwa wa mwisho katika kesi hiyo, yuko nje ya nchi na kwamba wanafanya utaratibu wa kumwita.

Katika kesi hiyo, Kampuni ya Njake Hotel & Tours inadaiwa kuchota kiasi hicho cha fedha kwa madai iliku ilirithishwa deni hilo na Kampuni ya E.Itoh ya Japan.Baada ya maelezo hayo, Jaji Mutungi aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 29, mwaka huu itakapoendelea kusikilizwa.

Mapema Msimamizi wa Idara ya EPA katika Benki Kuu ya Tanzania, Steven Mwakalukwa, alidai kuwa Kampuni ya Njake Hotel & Tours ililipwa Sh2.2 bilioni kwa kufuata taratibu zote za kibenki.Mwakalukwa ambaye ni shahidi wa pili wa upande wa mashtaka, alidai kuwa malipo hayo yalilipwa kwa Kampuni ya Njake Hotel & Tours kwa njia ya mtandao wa TISS kwenda Arusha katika akaunti namba 0781219002 iliyopo katika Benki ya Exim Arusha.

Aliendelea kudai kuwa kumbukumbu za malipo hayo zimehifadhiwa katika jalada ambalo alilitoa mahakamani kama moja ya kielelezo cha ushahidi, katika kesi hiyo.
 
Comments




+2 #1 aieli nkya 2011-04-15 08:57 Tatizo nchi hii inaendesha shughuili zake kwa msingi ya Wizi na Huruma. kuna sababu gani kuendelea kuwalea haya majambazi wanao hujumu uchumi wa nchi?
Quote







Refresh comments list
 
Hukumu kesi ya EPA mwezi ujao

Imeandikwa na Regina Kumba; Tarehe: 29th April 2011 @ 23:45 Imesomwa na watu: 55; Jumla ya maoni: 0







HUKUMU ya kwanza ya kesi ya wizi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inayowakabili mfanyabiashara na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rajab Maranda na mpwa wake, Farijala Hussein imeahirishwa kutokana na udhuru wa Mwenyekiti wa Jopo lililokuwa linasikiliza kesi hiyo, Sauli Kinemela.

Tangu mapema leo, ndugu na jamaa walikuwa wamefurika katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, kusikiliza hukumu ya kesi hiyo.


Kesi hiyo iliitwa mbele ya hakimu Mustapher Siyani aliyesema anaiahirisha kesi hiyo kwa kuwa mwenyekiti wa jopo lililokuwa likisikiliza kesi hiyo, Kinemela ana majukumu mengine nje ya Dar es Salaam na hivyo amepewa maelekezo ipangiwe baada ya wiki tatu.


"Mwenyekiti amesafiri nje ya Dar es Salaam na pia ana majukumu mengine hivyo nimeelekezwa iahirishwe mpaka baada ya wiki tatu kuanzia sasa kwa hukumu," amesema hakimu Siyani na kupanga Mei 23 mwaka huu.


Baada ya ahirisho hilo washitakiwa hao waliondoka mahakamani huku wakikwepa kamera za wanahabari huku wakiwaacha ndugu zao mahakamani.


Kesi hiyo inayowakabili watuhumiwa hao ni ya Sh bilioni 1.8 ambayo ni kati ya kesi za EPA zilizofunguliwa mfululizo mwaka 2008. Ilikuwa ikiendeshwa kwa msaada wa waendesha mashitaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).


Ni kesi pekee kati ya kesi hizo ambayo imefikia hatua ya kutolewa hukumu baada ya kusikilizwa ushahidi wa pande zote mbili.


Washitakiwa hao wanadaiwa kula njama, kughushi, wizi, kuwasilisha hati za uongo na kujipatia ingizo la fedha kwa njia ya udanyifu kiasi cha Sh 1,864,949,294.45, mali ya Benki Kuu (BoT) walipojaribu kuonesha kuwa kampuni yao ya Kiloloma Brothers ilipewa idhini ya kukusanya deni la Kampuni ya BC Cars Export ya Mumbai, India.


Maranda anakabiliwa na kesi nne za aina hiyo katika mahakama hiyo wakati Farijala anakabiliwa na kesi tatu za aina hiyo na wote wapo nje kwa dhamana.


Kesi nyingine zinazowakabili washitakiwa hao zilitajwa jana mahakamani hapo na kupangiwa kutajwa Mei 27 mwaka huu huku mshitakiwa Farijala mahakama imruhusu kwenda Kigoma baada ya kuomba ruhusa.
 
Mahakama, kesi za EPA zimewakinai?
blank.gif
pic_happy3.jpg

blank.gif
bullet3.gif
bullet3.gif
bullet3.gif
blank.gif
blank.gif
h.sep1.gif
Wasiliana na Mwandishi
phone2.gif
0716-774494
Tuma barua-pepe






Happiness Katabazi

amka2.gif
NOVEMBA 4, 2008, serikali kupitia Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Eliezer Feleshi, iliandika historia ya kuwafikisha watuhumiwa wa wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
Hatua hiyo ya Feleshi kufungua kesi 14 za EPA kwa watuhumiwa ambao wengine ni maofisa wa BoT na wafanyabiashara maarufu nchini, ilitokana na tuhuma hizo kuibuliwa na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kelele za wananchi na wafadhili kupitia vyombo vya habari ambazo zilisababisha Rais Jakaya Kikwete kuunda tume ya uchunguzi wa wizi huo ambayo ilimshirikisha Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Dk. Edward Hosea na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.
Tume hiyo iliwahoji watuhumiwa na hatimaye ikaridhia watuhumiwa hao wafikishwe mahakamani.
Binafsi nilikuwa miongoni mwa waandishi wa habari wachache hapa nchini ambao tumekuwa tukiziripoti kesi hizo tangu zilizofunguliwa hadi leo hii tunaendelea kuzifuatlia pale Mahakama ya Kisutu.
Nimejifunza mengi kutokana na ushahidi uliokwishatolewa na mashahidi wa upande wa Jamhuri na washitakiwa. Hivyo wakati kesi hizo zinafunguliwa kwa mpigo na kishindo mahakamani hapo Novemba 4, 2008, zilikuwa zinapangiwa kwa mahakimu wakazi wa mahakama hiyo katika hatua za awali.
Ilipofika hatua ya Jamhuri kuieleza mahakama upelelezi wa kesi hizo kuwa umekamilika, uongozi wa mahakama nchini enzi hizo ukiongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Agustino Ramadhani uliweka utaratibu wa kuziendesha tofauti na kesi nyingine.
Uongozi ulieleza kuwa kesi zote za EPA zitasikilizwa kwa mtindo wa jopo ambapo jopo hilo linaundwa na mahakimu wakazi watatu. Na hilo lilifanyika kwani majopo yalipangwa na kesi hizo hadi sasa zinaendelea kusikilizwa kwa mtindo wa majopo na ikitokea hakimu mmoja katika jopo fulani hayupo, basi siku hiyo kesi haitaendelea kwa sababu jopo halijatimia.
Na ikitokea wakili wa mshitakiwa fulani akamwombea ruhusa mteja wake ili atoke nje ya Dar es Salaam, kama jopo halijatimia basi mahakimu hao hukataa kutoa ruhusa hiyo kwa maelezo kuwa hawawezi kutoa ruhusa au kutoa maamuzi mbalimbali katika kesi husika bila idadi ya jopo kutimia.
Si idadi ya jopo kutotimia kulisababisha kesi za EPA kuahirishwa, pia katizo la umeme lilisababisha, kwa sababu uongozi wa mahakama uliweka utaratibu mpya ambapo walitafutwa wataalamu wa kompyuta kutoka Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara, ambao walikuwa wakija na kompyuta zao na kufunga vipaza sauti kurekodi mwenendo mzima wa kesi hizo.
Kwa kweli hilo lilikuwa likifanyika na mara kadhaa mahakama pia ilikuwa ikilazimika kuahirisha kesi hizo kwa sababu ya katizo la umeme kwani kompyuta nazo zilikuwa zikitumia umeme kurekodi mienendo ya kesi hizo 14 za EPA.
Wafanyakazi wa muda mrefu wa mhimili wa mahakama ambao si wasemaji walinieleza huo ni utaratibu mpya kufanyika katika Mahakama ya Kisutu tangu ilipoanza na wengine walidiriki kusema kuwa utumiaji wa teknolojia ya kompyuta kurekodi kesi hizo ulikuwa ni wa gharama na kwamba hautadumu kwa muda mrefu.
Kweli siku chache baadaye waandishi wa habari za mahakama tunaoweka kambi siku tano za jumaa mahakamani hapo tukaanza kuona kesi za EPA zinaendelea kusikilizwa bila ya teknolojia hiyo ya kompyuta kuwepo, na mashahidi wakawa wanafika kutoa ushahidi wao, hadi miaka inakatika sasa.
Binafsi nilijipa jukumu la kufanya uchunguzi wangu kujua kulikoni. Nilielezwa kuwa teknolojia hiyo haitakuwepo tena kwenye kesi hizo kwani ina gharama na kwamba hata upatikaji wa fedha wa kuprinti mwenendo wa kesi hizo uliokuwa ukirekodiwa kwa teknolijia hiyo hapo awali ulikuwa wa shida. Nikaishia kucheka.
Kwa mbwembwe hizo za mahakama na zile zilizokuwa zikionyeshwa na mahakimu wanaounda hayo majopo kwa sisi tuliobahatika kuzishuhudia tulisema kama kweli majopo hayo yataendelea na moyo huo, tulibashiri huenda kesi hizo zitachukua muda mfupi kumalizika.
Bado nakumbuka siku moja tukiwa mahakamani hapo, jopo moja linalounda kesi moja ya EPA inayomkabili mshitakiwa Farijala Hussein, lilikataa ombi la Farijala liloomba kesi hiyo iarishwe ili aende nyumbani kupumzika kwakuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa figo na hivyo amemeza dawa zinazomsababishia aende chooni mara kwa mara kujisaidia haja ndogo.
Jopo hilo liliendelea kupokea ushahidi wa shahidi wakati Farijala akiwa kizimbani na mara kwa mara alikuwa akinyoosha kidole juu kuliomba jopo hilo limruhusu ende kujisahidia haja ndogo na kisha kurejea kizimbani.
Hakuna ubishi kwamba upande wa Jamhuri katika kesi za EPA umejitahidi kadiri ya uwezo wake kuhakikisha unawaleta mashahidi wake bila kuchoka ukilinganisha na kesi nyingine ambapo upande wa Jamhuri umekuwa ushindwa kuwaleta mashahidi wake kwa wakati.
Na katika kesi za EPA nitakuwa sijautendea haki upande wa Jamhuri kama sitaupa pongezi kwa kuweza kuwaleta mashahidi wao bila visingizio na Jamhuri ingekuwa ikifanya hivyo hata kesi zake katika mahakama zote nchini, wananchi tusingekuwa tukiilaumu.
Kwa muktadha huo hapo juu basi leo Fukuto la Jamii, limesukumwa kuueleza umma na kuuliza uongozi wa mahakama kwamba kulikoni ile kasi ya baadhi ya mahakimu wanaounda kesi za EPA ya kufika mahakamani bila kukosa hata kama kesi hizo zimekuwa zikija kwaajili kusikilizwa au kujatwa, kupungua? Au kesi za EPA zimewakinai?
Haya ninayoaandika sio nimesimuliwa, ninayashuhudia kila kukicha na ndio maana leo nimelazimika kuandika makala hii kwa umma na mahakimu wao ili waweze kutueleza kuwa huenda kesi za EPA zimewakinani ndiyo maana siku hizi hata kesi hizo wakizipangia tarehe, itakuja kwaajili ya upande wa Jamhuri au utetezi kuwasilisha majumuisho ya washitakiwa wana kesi ya kujibu na mashahidi kuendelea kutoa ushahidi wao, huku baadhi ya mahakimu wanaounda majopo wakiwa hawaonekani.
Na matokeo yake waandishi wa habari za mahakama siku hizi tumekuwa tukishuhudia hakimu mwingine kabisa ambaye hata kwenye yale majopo 14 yanayosikiliza kesi 14 za EPA hayupo, akifika ndani ya chumba cha mahakama huku akitabasamu anaanza kueleza kuwa amepata taarifa kutoka kwa wana jopo (mahakimu wakazi) wanaosikiliza kesi husika kwamba hawapo hivyo yeye amekuja kuiahirisha kesi hiyo na kupanga tarehe nyingine.
Na ushahidi mmoja wapo unaounga mkono hoja yangu hiyo ni lile tukio lililotokea Aprili 29 mwaka huu. Ahadi iliyotolewa na Mahakama ya Kisutu Januari 26 mwaka huu, kuwa Aprili 29 ingetolewa hukumu ya kesi ya wizi wa fedha za EPA inayomkabili Mweka Hazina wa (CCM), Rajabu Maranda (53) na mpwa wake, Farijala Hussein, ilishindwa kutekelezwa kwa vitendo.
Jopo la mahakimu wakazi linaloundwa na Saul Kinemela, Focus Bambikya na Ilvin Mugeta, ambalo ndilo lilikuwa likisikiliza kesi hiyo ya jinai namnba 1161/2008 hawakuweza kutokea mahakamani.
Hivyo Mahakama ya Kisutu ililamizimika kumtuma Hakimu Mkazi Musthapher Siyani, ambaye hajawahi kusikiliza kesi za EPA zilizofunguliwa na serikali, kuja kuahirisha hukumu pamoja na kesi nyingine tano za EPA zinazowakabili watuhumiwa hao na wengine ambao ni Jayantkumar Chandubhai Patel ‘Jeetu Patel ‘na wenzake.Akitoa sababu ya kushindwa kusomwa kwa hukumu hiyo, Hakimu Siyani alisema amepata taarifa kuwa kiongozi wa jopo hilo Saul Kinemela yupo nje ya Dar es Salaam. Na kweli baada ya uchunguzi wa Fukuto la Jamii ulibaini Kinemela alifuatana na Waziri wa Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka mkoani Songea kwa ajili ya maadhimisho ya kilele cha Siku ya Usalama Mahala pa Kazi.
Hata hivyo kuahirishwa kwa hukumu hiyo si siri kumeacha maswali mengi kwa baadhi ya wananchi waliohudhuria mahakamani hapo wakishangazwa na kitendo cha mahakimu wote watatu wanaounda jopo na wanaosikiliza kesi nyingine tano kushindwa kutokea mahakamani hadi kufikia hatua ya kuahirisha kesi zao licha ya kuwa kesi moja namba 1163/2008 inayomkabili Maranda na Farijala kuja kwa ajili ya kufanyiwa majumuisho ya washitakiwa hao kama wana kesi ya kujibu au la.
Swali ambalo tumekuwa tukijiuliza wananchi, je, wakati jopo hilo linapanga tarehe ya hukumu kiongozi huyo wa jopo Kinemela hakuwa akijua tarehe hiyo ya hukumu ni siku ya maadhimisho hayo?
Kama kweli hukumu imeishaandaliwa ni kwanini isitolewe idhini ya kusomwa hukumu hiyo na wana jopo wenzake bila ya yeye kuwepo? Sasa kama ikitokea tena hakimu mwingine anayeunda jopo hilo Mei 23 mwaka huu ambapo kesi hiyo imepangwa kusomwa, akiwa amesafiri, hukumu hiyo haitasomwa tena kwa sababu mwanajopo mmoja amesafiri?
Ni hukumu ngapi zinaandaliwa na mahakimu wengine lakini kutokana na hakimu aliyeiandaa hayupo anatoa idhini hukumu hiyo isomwe na hakimu mwingine na kweli hukumu hiyo inasomwa?
Na ushahidi wa hukumu zilizoandaliwa na majaji wengine na kusomwa na msajili ni pamoja na hukumu ya rufaa ya mwanamuziki wa dansi, Nguza Vicking na wanawawe ambayo ilisikilizwa na hukumu hiyo kuandikwa na jopo la majaji watatu, Nataria Kimaro, Salum Massati na Mbarouk Mbarouk wa Mahakama ya Rufani nchini, ambapo hukumu hiyo ilikuja kusomwa na Msajili Neema Chusi kwa niaba ya jopo hilo.
Hukumu nyingine iliyosomwa bila idadi ya jopo kutimia ni hukumu ya kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Costa Mahalu, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mwaka 2008, ambapo Oktoba 4 mwaka jana, Jopo la majaji watatu lililokuwa likiongozwa na Jaji Kiongozi Fakhi Jundu, Agustine Mwarija na Projest Rugazia lilisoma hukumu yake bila Jaji Rugazia kuwepo mahakamani ambapo Mahakama Kuu ilisema inakubaliana na Mahalu kuwa kifungu cha 36 (4)(e) Sura ya 200 cha Sheria ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2002, kinapingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Kwa hiyo mahakimu wanaosikiliza kesi za EPA na kesi nyingine kama za matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara watambue kuwa wananchi kupitia vyombo vya habari watu wanazifuatilia kwa karibu kesi hizo ili waweze kujua hatima yake kwa kuwa uchunguzi wa kesi za EPA uliwekewa utaratibu wa aina yake tofauti na kesi nyingine.
Fedha nyingi za walipa kodi zilitumika katika ile tume iliyoundwa na rais hivyo wananchi hao ambao kodi zao zilitumika wana haki ya kufuatilia hatima ya kesi hizo.
Sasa inapotokea matukio kama haya ya baadhi ya mahakimu wanaounda kesi hizo kupunguza kasi ya kuudhuria kesi hizo na vyombo vya habari vikaripoti matukio hayo, itasababisha Watanzania kutanguliza hisia mbaya kuhusiana na kesi hizo ya EPA hata kama ushahidi wa hisia hizo walizonazo hawana.
Mahakimu wanaosikiliza kesi hizo warejeshe ile kasi yao ya zamani ya kuhudhuria kesi hizo na waachane na kasumba ya kuwatuma mahakimu wasiosikiliza kesi hizo kuja kuahirisha kesi zao, licha ya kwamba hakuna sheria inayokataza hilo.
Kama uongozi wa mahakama nchini hautasimama vema kuhakikisha majopo hayo yanahudhuria kesi zao bila kukosa, basi kuanzia sasa tuanze kuliwekea mashaka lile tamko la Jaji Kiongozi Fakhi Jundu, kwa umma kwamba kesi za kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2010 zimewekewa utaratibu wa kusikilizwa na majaji kutoka mikoani na kwamba zitakuwa zimemalizika ndani ya miaka miwili tangu zilipofunguliwa.
Kesi hizo za uchaguzi ambazo zilifunguliwa Novemba mwaka jana zimekuwa zikisikilizwa na kuamuliwa na Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kinyume na tamko hilo kwamba majaji watakaosikiliza kesi hizo watatoka mikoani.
Na katika kesi hizo, hakuna hata kesi iliyofikiwa ya shahidi hata mmoja kupanda kizimbani kutoa ushahidi wake.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
 
Washtakiwa wa kesi ya EPA wahukumiwa kwenda jela miaka mitano Send to a friend Saturday, 21 May 2011 10:09

Makanda wa CCM Farijara Husein na Rajabu Maranda wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano baada ya kukutwa na hatia ya uwizi wa fedha za EPA, Habari kwa undani ungana nasi baadaye
 
Kesi nyingine ya Maranda yaiva Send to a friend Monday, 30 May 2011 21:14

Tausi Ally
KESI ya wizi wa Sh 3.3 bilioni za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inayomkabili kada wa CCM, Rajabu Maranda, binamu yake Farijala Hussein, Ajay Somani na wafanyakazi watatu wa benki hiyo itaendelea kusikilizwa mfululizo kuanzia Julai 19 hadi 21 mwaka huu.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Ilvin Mgeta alisema jana kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa, lakini mwenyekiti wa jopo la mahakimu wanaoisikiliza, Jaji Samuel Kalua hakuwapo kwa kuwa alisafiri kikazi nje ya Jiji la Dar es Salaam hivyo iliaharishwa hadi Julai 19 itakasikilizwa kwa mfululizo.

Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka unatarajia kuwaita jumla ya mashahidi 38 kutoa ushahidi dhidi ya kesi hiyo.
Washtakiwa Farijala Hussein, Rajabu Maranda na Ajay Somani wanadaiwa kuwa kati ya Januari 18 na Novemba 3, 2005, kinyume na kifungu namba 384 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 ya sheria, walikula njama ya wizi wa fedha kutoka BoT.

Pia wanadaiwa kughushi hati ya usajili yenye namba 46218 na kuonyesha kuwa zimesainiwa na kutolewa na Msajili wa Biashara kwa Kampuni ya Mibale Farm wakati si kweli.

Iliendelea kudai kuwa washitakiwa hao, Farijala, Rajabu, Ajay na wafanyakazi wa BoT, Imani Mwaposya, Ester Komu na Sophia Kalika kwa pamoja wanadaiwa kuiba Sh3.3 bilioni za EPA kutoka kwenye benki hiyo baada kudanganya kuwa kampuni yao ya Mibale Farm imepewa deni na kampuni ya Textile Mills Ltd ya nchini India na kujipatia inginzo hilo.

Awali Mei 23, mwaka huu, washtakiwa Farijala na Maranda walihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na kuamuliwa kulipa Sh 1.8 bilioni walizodaiwa kuchotwa BoT na kwamba iwapo watashindwa kuzilipa mali zao zikamatwe na kufilisiwa.Mbali na kesi hizo, kada huyo wa CCM na binamu yake Farijala katika kesi nyingine inayowakabili ya wizi wa Sh2.2 bilioni za EPA, Juni 21, mwaka huu wataawasilisha hoja zao kwenye Mahakama hiyo ya Kisutu kama wana kesi ya kujibu.

 
Comments




0 #1 cowiti j.l 2011-05-31 04:01 kia moja ata wajibika kwa kile alicho kitenda ina kera pale wezi wazao walisamewa na rais atabila kuwakamata kwa kisingizio cha kurudisha pesa walizochukuwa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom