Mwenendo wa CUF unanifanya nizichukie siasa za vyama vingi nchini

Tangu lini CHADEMA wamesema hivyo ? Mbona CUF wasema watapiga kambi ARUSHA ? kama VILE hakuna Vyama Vingine ? Isipokuwa CUF na CUF pekee, na wakapokelewa na MKUU wa POLISI wa MKOA, MKUU wa MKOA Viongozi Waandamizi wa Mkoa Sasa hapo hauoni ya kuwa ni furaha na faraja kwa CUF kupendwa na CHAMA TAWALA ? Haukuona MKUTANO wa CUF ulifanana kama wa CCM ? Ulikuwa na MALORI na MABASI ya kubebaWananchi; Wananchi walikuwa Wamevaa Sare za CUF za kupendeza haswa kama wa CCM; Walisimika Mwanachama MMOJA tu kuingia CUF... na MAPOLISI HAWAKUWEPO KAMA VILE MKUTANO ULIKUWA WA CCM...

Kaka aliyepokelewa ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, hivyo polisi na viongozi wa serikali walikuwa lazima wahusike
 
Halmashauri ngapi Chadema wameungana na ccm? hlo hamulioni? kwa hyo mlitaka wazanzibar wauliwe mutawale achen unafiki wananch wa zanzbar wameamua kua na serikal wanayoitaka...hiv ktk mikutano watu wakivaa baraghashia inawauma eeh mbona wakat wa kugombania uhuru hamkuona achen udini huo..
 
NAFIKIRI PROF. LIPUMBA ANABURUZWA NA MAALIM SEIF! MAALIM SEIF=CUF(CCM-B). Akiambiwa fanya hivi anafanya, 2015 sijui atagombea tena urais! kazi kweli! Kwenye mikutano wanabeba/wanasafirisha watu, kwa nini wasimwombe mme wao nyinyiem awaazime wafuasi wahudhurie mikutano yao!
 
Kweli kazi ipo, na utawala uliopo kupitia msajili wa vyama vya siasa wataendelea kusajili vyama vingi hata vifike 200, lakini vile vya upinzani vya kweli tendwa atatishia kuvifuta au kufuta kabisa! Cuf ni popo, utawala anapenda na upinzani anapenda!
 
Na nyie na mawazo ya kale ya nyerere hamfiki popote hivi bado hamuelewi ubovu wa sera zake ndio umetufikisha hapa leo
Kwenye siasa opposition una oppose aliyeko madarakani pamoja na opposition wenzako
CDM ya 2010 hayayatatokea 2015
CUF wana stand juu zaidi
Haya yalitokea wakati wa mrema
Na ndio itavokua 2015

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Too low! Masabuli at work. Quote me " u r an empty brain entity"
 
Penguine, pengine niko nyuma na matukio. Hivi CUF imeanza lini kuwa chama cha upinzani? Naelewa upinzani wa CUF ulikwisha 2005 mara baada ya Mahita kuwapokonya visu walivyokuwa navyo katika mikutano yao na mpaka hivi sasa kimeshasalimu amri na ni msaidizi (assistant) wa karibu wa CCM. Embu nipeni updates wanajamvi kwani ninashangaa kusikia watu wanalalamika eti CUF inaua upinzani na wakati kwa kufanya hivyo, inafanya kazi yake iliyopewa na CCM mara baada ya makubaliano ya Zanzibar. Hivi kweli leo hii utalinganisha CUF na Chadema eti vyote ni vyama vya upinzani? Sio kweli kabisa. Ukweli ni kwamba CUF ni chama cha kundi la watanzania wachahce waishio visiwani Pemba. Watu hao wapo kama 300,000 hivi ambao ni sawa na asilimia 0.71 ya watanzania wote. Mark my words, CUF hii itaambulia less than 2% ya kura za urais 2015. Huwezi hata kidogo kuilinganisha na chama cha watanzania wengi kama Chadema. Hatuna hata sababu za kuijadiri CUF kwani haiwezi kuleta madhara yeyote kwatanzania wa leo wanaelewa chama ni kipi na aliyetumwa ni yupi?
 
Haoku peke yako Mkuu! Profesa Lipumba anajidhalilisha yeye, familia yake na wasomi wote kwa ujumla. Profesa wa Uchumi, lakini njaa inamsumbua na kutumiwa kirahisi na JK.

hivi siku hizi prf ana familia? kwa upande wa kisiasa anavyobehave implication ni kuwa ameshindwa, basi walao ameona bora akubali kutumiwa maana inampatia ugali na nauli za kuzunguka zunguka.
singependa pia kuimba wimbo wanaouimba ccm na cuf juu ya cdm, maana inakuwa kama malumbano, ila watu wa type ya cuf wana msuli wa kukomaa na uwongo, utashindwa wewe unayesema kweli. ali mradi akushinde kwa kukusingizia, hiyo ndio observation yangu, so wale msio na msuli huo, please don't waste your callories, hamtaweza. wakianza kukuita wewe mdini nyamaza tu, japo anajua kabisa kuwa yeye ndio mdini, watapenda watu wawaamini wao na wewe watu wakuchukie ndicho wanachokazana nacho. waacheni kama walivyo, wenye kupenda mageuzi ya kweli yatakayopelekea maendeleo ya kweli jitahidini/tujitahidi na tuamini kwamba daima penye ukweli uongo hujitenga. na zaidi Mungu huonekana zaidi kwenye kweli.
kuna swali moja tu, hivi cdm wamekua adui/wapinzani wa wote? hata wale wenye malengo yanayofanana na cdm nao wamegeuka na kuungana na adui/mpinzani (ccm) kumpinga cdm?! hapo tunajumlisha na kutoa = wivu kuona kuna mafanikio na kukubalika
 
Ni aibu kubwa kuona CUF pamoja na uprofessor wao wanashindwa kutofautisha na kutambua hasa adui yao ni nani?Kwa sote tuliofuatia mikutano yao ya Arusha ni wazi kuwa CUF ni chama cha kidini,hakina malengo ya kuchukua nchi bali kuisaidia CCM iendelee kutawala milele na pia ni chama ambacho hakina vision yoyote.To my opinion tofauti ya CUF na uamsho ni kuwa CUF hawachomi makanisa wala baa,ila si ajabu kuwa wafuasi wengi wa Uamsho pia ni CUF .
 
Mnamo mwaka 1992, rasmi Taifa letu liliingia katika Mfumo wa Vyama vingi vya Siasa. Inaelezwa kwamba Mfumo huu haukuwa chaguo la Wananchi waliowengi (80% ya idadi ya watanzania waliohojiwa miaka hiyo).

Hata hivyo, Mwl. Nyerere akaona siyo kweli kwamba waliowengi ndiyo wako sawa wakati wote; akaamuru nchi ifuate mtazamo wa wananchi wachache waliotaka vyama vingi (20% ya idadi ya watanzania waliohojiwa miaka hiyo). Mtazamo mpana ilikuwa ni katika umuhimu wa vyama vingi vya siasa nchini katika kuchochea uwazi, ufanisi na uwajibikaji wa serikali iliyopo madarakani.

Kwa mtazamo wangu binafsi naona kama CUF inaenda kinyume na mtazamo huo mpana aliokuwa nao Mwl. Nyerere. Mtazamo wa vyama vingi vya siasa kusaidia kuleta maendeleo ya wananchi na nchi kwa ujumla kwa kuchochea uwazi, uwajibikaji na ufanisi wa Serikali iliyoko madarakani. CUF mmejisahau kabisa, mnatia aibu, mnaaibisha mmetupilia mbali dhana ya kuchochea maendeleo kwa kudai uwazi, uwajibikaji na ufanisi wa serikali iliyoko madarakani. CUF mnapambana na SERIKALI KIVULI YA CHADEMA. Great shame!

Siyo vibaya kuleta siasa za kukosoana, kuelimishana, kujengana na kurekebishana pale mnapoona mwenzenu fulani (here to mean chama fulani cha siasa miongoni mwenu) kinaenenda kwa namna ambayo haifai kwa ustawi wa taifa na watu wake. MKOSOENI na KOSOANENI kwa kuwa Tanzania ambayo kila chama cha siasa kinaililia kuiongoza ni yetu sote. Lakini katika hili, CUF hamko hivyo! Shame on you! Kazi yenu imekuwa ni kupambana na Serikali kivuli ya CHADEMA huku mkisahau kuleta uchochezi katika huduma bora za maji safi na salama mjini na vijijini, huduma za viwango vya juu ya elimu na mafunzo ya ufundi, kushuka kwa mfumuko wa bei na MFUMUKO WA UFISADI nchini.

CUF mmekuwa mkiimba nyimbo zinazotyuniwa na CHADEMA kwa lengo la kukandamizana nyie wenyewe mlio vyama vya upinzani. Mfano wa nyimbo hizo ni wimbo wa Operation Sangara Mkauitikia, Wimbo wa M4C mmeuitikia, nasikia mmeanzakuitikia hata kwa wananchi kujishika kichwani ati kulaani wanaowatumia vijana katika siasa. very shame and severe lack of innovativeness.

Ni maoni tu.
Hii inadhihirisha uhuni alio ufanya Rajabu Kiravu kwa kuinyima CDM ushindi kwani kwa jinsi hali ilivyo CDM ndio chama tawala na msinshangae kuwa na wapinzani ambao wengi hamkutarajia, pia yatupasa kujua kwenye ukweli uongo hujitenga na mkitaka kufahamu angalieni CDM inavyo ongoza nchi kwa kuanzisha kitu na serekali kutekeleza
 
Ni aibu kubwa kuona CUF pamoja na uprofessor wao wanashindwa kutofautisha na kutambua hasa adui yao ni nani?Kwa sote tuliofuatia mikutano yao ya Arusha ni wazi kuwa CUF ni chama cha kidini,hakina malengo ya kuchukua nchi bali kuisaidia CCM iendelee kutawala milele na pia ni chama ambacho hakina vision yoyote.To my opinion tofauti ya CUF na uamsho ni kuwa CUF hawachomi makanisa wala baa,ila si ajabu kuwa wafuasi wengi wa Uamsho pia ni CUF .

HALAFU CHADEMA ni CHAMA CHA WAKRISTO, WAIMBA KWAYA NA WALEVI WA VIROBA?
 
Mkutano wa Arusha umenifanya nianze kumdharau Prof. Lipumba, nilikua namuheshim sana, kwasasa heshima kwake ni Zero
 
Mnamo mwaka 1992, rasmi Taifa letu liliingia katika Mfumo wa Vyama vingi vya Siasa. Inaelezwa kwamba Mfumo huu haukuwa chaguo la Wananchi waliowengi (80% ya idadi ya watanzania waliohojiwa miaka hiyo).

Hata hivyo, Mwl. Nyerere akaona siyo kweli kwamba waliowengi ndiyo wako sawa wakati wote; akaamuru nchi ifuate mtazamo wa wananchi wachache waliotaka vyama vingi (20% ya idadi ya watanzania waliohojiwa miaka hiyo). Mtazamo mpana ilikuwa ni katika umuhimu wa vyama vingi vya siasa nchini katika kuchochea uwazi, ufanisi na uwajibikaji wa serikali iliyopo madarakani.

Kwa mtazamo wangu binafsi naona kama CUF inaenda kinyume na mtazamo huo mpana aliokuwa nao Mwl. Nyerere. Mtazamo wa vyama vingi vya siasa kusaidia kuleta maendeleo ya wananchi na nchi kwa ujumla kwa kuchochea uwazi, uwajibikaji na ufanisi wa Serikali iliyoko madarakani. CUF mmejisahau kabisa, mnatia aibu, mnaaibisha mmetupilia mbali dhana ya kuchochea maendeleo kwa kudai uwazi, uwajibikaji na ufanisi wa serikali iliyoko madarakani. CUF mnapambana na SERIKALI KIVULI YA CHADEMA. Great shame!

Siyo vibaya kuleta siasa za kukosoana, kuelimishana, kujengana na kurekebishana pale mnapoona mwenzenu fulani (here to mean chama fulani cha siasa miongoni mwenu) kinaenenda kwa namna ambayo haifai kwa ustawi wa taifa na watu wake. MKOSOENI na KOSOANENI kwa kuwa Tanzania ambayo kila chama cha siasa kinaililia kuiongoza ni yetu sote. Lakini katika hili, CUF hamko hivyo! Shame on you! Kazi yenu imekuwa ni kupambana na Serikali kivuli ya CHADEMA huku mkisahau kuleta uchochezi katika huduma bora za maji safi na salama mjini na vijijini, huduma za viwango vya juu ya elimu na mafunzo ya ufundi, kushuka kwa mfumuko wa bei na MFUMUKO WA UFISADI nchini.

CUF mmekuwa mkiimba nyimbo zinazotyuniwa na CHADEMA kwa lengo la kukandamizana nyie wenyewe mlio vyama vya upinzani. Mfano wa nyimbo hizo ni wimbo wa Operation Sangara Mkauitikia, Wimbo wa M4C mmeuitikia, nasikia mmeanzakuitikia hata kwa wananchi kujishika kichwani ati kulaani wanaowatumia vijana katika siasa. very shame and severe lack of innovativeness.

Ni maoni tu.

Mkuu ur dead wrong kama ulifikiri kuna seriousness kwenye mfumo wa vyama vingi hapa Tanzania wengi ya wapinzani ni mapandikizi waliotumwa upinzani kwa manufaa ya Systerm inayotawala. Hapa si lazima iwe CCM lakini ni kikundi cha watu chenye malengo fulani. Unalalamikia CUF kwenda kufanya mkakati wa kukibomoa CHADEMA Arusha, lakini wakati huo huo ulisahau kwamba CHADEMA ndio walioanza kwenda kusini na ajenda moja kuu kuwaamushawakazi wa kusini kwamba wasikiendekeze CUF kwa vile ni mke wa CCM. Hii pekee ilikuwa ni insult kwa CUF. Kama kweli wapinzani wana nia ya kuleta umoja wangewashawishi CUF kufanya mikutano wa pamoja kusini, hata kama CUF wangekataa wananchi tungejua dhamira yao.

Labda nikuulize ukumsikia Slaa analalamikia uteuzi mbovu wa NEC ya CCM. Yeye kama mpinzani wa kweli hakupaswa kuchukizwa na hilo. Aidha kwa hivi karibuni umwewasikia viongozi wakubwa wa CHADEMA wakimsema vibaya Lowasa au Rostam Aziz? unajua kwa nini viongozi hao wanasemwa vibaya na wanaCCM kuliko viongozi wa CHADEMA. Kaka kushabikia vyama ni jambo bora lakini usijekupoteza utu wako na nafsi yako kwa ajili ya wapinzani wa kibongo. Kumbuka maneno ya Mbowe aliyoyasema alivyokuwa USA. Watu wasijekupata stroke pale SLAA atakapojiunga na CCM
 
Mkuu wangu Penguine siasa za vyama vingi nchi hii ni ngumu sana utaumiza sana kichwa chako mkuu wangu! Kwa jinsi Cuf wanavyofanya siasa zao kupambana na chadema as if chadema ndo walioshika dola dah! Kiukweli nimewadharau sana hawa jamaa na naona matumaini ya vyama vya upinzani kushika dola na kuiondoa ccm ni kazi sana Mungu tu labda aingilie kati! Cuf na Lipumba wao wanatuangusha sana!
 
Cuf sio chama cha upinzan ila ni jumuia ya ccm km ilivyo jumuiya nyingine km uvccm na umoja wa wazaz wa ccm
 
Acha kabisa tabia ya kupenda kusema wake za watu. Sio vizuri hivyo kwani mumewe ndie anayemtuma.
halafu bora chuki ya mwanaume ndani ya nyumba kuliko kuchukiwa na mama mwenye nyumba hawa CUF(A.K.A MAMA MAGAMBA wanaenda arusha kudeal na chadema kwa vijembe hawa kina mama ni wabaya saana
 
Una maana gani Kiongozi? Katika hili nani ni mume na Mke ni yupi?

Kwani hutambui kuwa CUF walikwishaolewa na cccm? Hata mikutano wanayaofanya kwa sasa inafadhiliwa na hao ccm na ndio maana unaona wanatumia nguvu kubwa sio kujijenga, bali kuhakikisha eti wanavunja ngome za CHADEMA kama walivyokuwa wanajitapa ktk mkutano wao waliouitisha Dar juzi juzi. Wamebaki na mbinu zisizo na ubunifu kama ccm.
 
Back
Top Bottom