Mwendesha pikipiki anusurika katika ajali

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
TATIZO la kutozingatia usalama kwa waendesha pikipiki nchini linazidi kuongezeka kutokana na ajali za kila mara ambapo katika tukio moja wiki hii, mwendesha pikipiki alinusurika kufa katika barabara ya Korogwe eneo la Simba Oil mjini Morogoro kutokana na kukiuka sheria za usalama barabarani.
Kwa mujibu wa mashuhuda, mwendesha pikipiki huyo alikuwa akijaribu kulipita gari lenye namba za usajili T 635 AKM aina ya Toyota Land Cruiser ambapo mbele yake kulikuwa kuna gari dogo lenye namba T 580 AAK lilikokuwa likielekea upande wa pili.
Matokeo yake ni kwamba mwendesha pikipiki huyo alijikuta hawezi kurudi nyuma wala kusonga mbele na hivyo kukwanguliwa na gari hilo lilikokuwa mbele yake na kumtupa chini ambapo alipata majeraha kadhaa kabla ya polisi kufika eneo hilo kuchukua vipimo.
<!--ThumbBegin--> <!--ThumbEnd-->
Pikipiki iliyohusika katika ajali hiyo.

<!--ThumbBegin--> <!--ThumbEnd-->
Mwendesha pikipiki aliyesababisha ajali.

<!--ThumbBegin--> <!--ThumbEnd-->
Kijana aliyepata ajali (kulia aliyeinua mkono) akitoa maelekezo kwa polisi kuhusu ajali ilivyotokea.

<!--ThumbBegin--> <!--ThumbEnd-->
Polisi akiondoka na mwenye pikipiki kwa ajili ya kwenda kutoa maelezo.

<!--ThumbBegin--> <!--ThumbEnd-->
Safari ya kuelekea kituoni ikianza.

<table border="0" cellpadding="0" cellspacing="0" width="100%"><tbody><tr><td class="news1" align="left" width="61%">
</td> <td class="news1" align="right" width="39%">
</td></tr></tbody></table>
 
Dah anabahati huyu angevunjika kiuno hicho lol.
Naona hakufanya maamuzi ya busara kulipita hilo gari.
 
yaani polisi wa kawaida anambeba jamaa kwenda kituoni kuandika maelezo, kwani polisi wa usalama barabarani hawapo? kwanini asiende na dereva wa gari pia?
 
yaani polisi wa kawaida anambeba jamaa kwenda kituoni kuandika maelezo, kwani polisi wa usalama barabarani hawapo? kwanini asiende na dereva wa gari pia?


Kila polisi mwenye uniform anayo madaraka ya kukushughulikia ukifanya makosa ya barabarani, si wenye nyeupe tu kaka.
 
we fidel vipi?
si nilikwambia uwe makini?ona sasa na picha yako wameirusha jf
 
Ah pikipiki bana itanisamehe tu, ni hatari mno kwenye hizi barabara zetu
 
Na kwa tahadhari ni kwamba kama wewe ni derava ogopa sana magari haya Landcuiser, yawe ya serikali au watu binafsi huwa wanaendesha kwa kasi kubwa sana, hasa yale ya serikali. Pia malori ya mchanga!!! Kama unataka ku-overtake check kwanza ni aina gani ya magari ambayo unataka kuyapita!!!
 
Back
Top Bottom