Mwekezaji 'kusaidia kujenga Mahakama ya Rufaa' siyo sawa!

Nchi ilishauzwa nashangaa hawatuwagii shea yetu ili tuwe watumwa halali ndani ya nchi yetu. Mwekezaji kujenga Mahakama ya JMT hahahahahahahahaha, Nape na chama chenu hamuona hata aibu????
 
wanafikiria vya rahisi rahisi tu. Kwa mtindo huu, hawana tofauti na mateja, wananadi dala dala kwa ujira mdogo kumaliza matatizo yaliyo mbele ya mboni zao.....

Viongozi wote wanaona kama Tanzania ni mali ya urithi: sehemu ambayo wanachuma bila kutoka jasho na wakiona vipi wanauza kwa bei ndogo sana na hata uchungu hawausikii na watoto na wajukuu hawakumbukwi.

Nawaambia, Viongozi wenye uchungu na nchi hii wanaweza kukaa kwa starehe bila kubanana wakipanda bajaji.
 
Jitokezeni tuingie mtaani haya mambo ya kipuuzi sasa yametosha ipo siku na ile Ikulu watasema mwekezaji amejitolea kujenga nyingine nchi ya ajabu haikosi maajabu!!!
 
Aende tu na pale white house, mbona linafasi likubwa tu! Yaani sidhani kama kuna watu kwenye baadhi ya maofisi ya serikali kama wanafikiri!

Naye mheshimiwa waziri kalirusha hewani bila kutafuna maneno?
 
Matusi ya Selina Kombani in the making kweli hii nchi haina bilioni 100 za kujenga chombo muhimu na tunu ya taifa kama MAHAKAMA YA RUFAA hawa CCM na serikali yao ni janga la kitaifa
Pili Jengo lile ni la historia yeye anaenda kulinganisha na makaburi what is the thinking capacity ya waziri KOmbani maudhi matupu,yaani watamaliza majengo yote ya kale kwa sababu ya kulizisha waarabu na wahindi
 
Kuna wakati uwa natamani niamke asubui nisiangalie TV, kusikiliza redio, kusoma magazeti, kuingia mtandaoni wala kuwasha simu yaani total blackout kwa huu upuuzi unaondelea hapa nchini, Masaburi labda alilijua hili mapema akaamua kusema yale, mambo mengine yanatia hasira sana mpaka mtu unajiuliza watu hawa watawala wana akili gani, wanawaza nini vichwani mwao??? yaani, THIS IS TOO MUCH!!!!!!!!!

Namsikiliza Mh Waziri wa Sheria na Katiba akijenga hoja kuwa kuna mwekezaji anajitolea kujenga mahakama ya rufaa kama atapewa hilo jengo la Mahakama ya Rufaa - iliyokuwa Forodhani Hotel.

Mimi naona hata kama ndivyo haitakuwa sawa kwa mwekezaji kutujengea MAHAKAMA YA RUFAA - THE HIGHEST COURT IN THE COUNTRY.

Ni bora Serikali isihusishe ujenzi huo na mwekezaji hata kama ndio PPP...NASEMA HAPANA!
 
Mhhhh,

Hii nchi bwana...Kila kitu kinatembea kichwa chini miguu juu!!

Hope baada ya hili watajenga hoja kuwa ikulu haitakiwi kuwa kwenye sehemu ambayo inafaa kujenga hotel ya nyota 10!! Na kwamba Rais akikaa Kibamba ni poa tu...

Na baada ya hapo, lazima waanze kutupiga bei sisi wenyewe..Bahati nzuri wengine hatuna thamani kubwa kwa wawekezaji, kwa hiyo lazima tutapona tu!!
 
wazir unafananisha jengo linlotumiwa na court of appeal kama kaburi, that iz illogical and non sense with all due respect
 
  • Thanks
Reactions: FJM
tumetawalwa katika hela yetu tukakubali, tumetawalwa katika bisahara ya mafuta tumekubali, tumetwalwa ............... tumekubali sasa ifike wakati tuseme hapana kwenye mahakam zetu, hawawezi kututawala kwenye vyombo vya kutoa haki, wanyonge tutakimbila wapi kama hapo pakiuzwa dhahiri shahiri
 
Hawa wanaowaita wawekezaji, wameshajua kuwa "masikini ukimpa msaada anakuwa mtumwa kwako". SS tutegemee kesi ya mahindi kumpelekea nyani atoe hukumu!!
 
wazir unafananisha jengo linlotumiwa na court of appeal kama kaburi, that iz illogical and non sense with all due respect

Ina maana wale wote wanaotumia jengo ( their Lordships) ni wafu, inabidi awaombe radhi majaji tusi zito sana hilo
 
Next madhani watauza eneo la geti ya Ikulu upande wa PM wakingojea jumba kubwa ili kujenga hoja .Mie yangu macho hakika aibu hadi mwisho Nchi hii duh ! JK wa nini mlimpa kura ?
 
Namsikiliza Mh Waziri wa Sheria na Katiba akijenga hoja kuwa kuna mwekezaji anajitolea kujenga mahakama ya rufaa kama atapewa hilo jengo la Mahakama ya Rufaa - iliyokuwa Forodhani Hotel.
``Kama atapewa hilo jengo`` maana yake nini, atakuwa anawakodisha ofisi za mahakama kwenye jengo lake jipya au wanabadilishana viwanja yeye abomoe hapo ajenge night pub yake wao wahame, au kimesemwa nini hasa? Na huyo anaewajengea bure ni mwekezaji au mfadhili? Apewe jengo hilo ndio nini?
 
Bado kidogo utasikia ikulu anapewa mwekezaji, kwa jinc hii! Kweli nakumbuka stor ya mfalme juha! Bt 2nao wa2 wa jinc hii
 
Yaani mwekezaji hadi kwenye mahakama? It's ludicrous to even entertain such a thought. But that's just me.
Nyani,
Ni hivi; yule tajiri anayemiliki Kempiski analitolea mate eneo la Mahakama ya rufaa, na amemshawishi swahiba wake mkuu ( ambaye kwa sasa atabakia nameless) kuwa yeye tajiri awajengee Mahakama ya rufaa jengo jipya kwenginepo mjini, kama ni mbagala, kijitonyama, sijui, ili yeye, mmiliki wa Kempiski aendeleze matanuzi katika eneo hilo la jengo la mahakama ambalo limekarabatiwa hivi karibuni tu kwa hela nyingi za walipa kodi. Upo hapo?
 
natamani wasome waone aibu yao! hivi wanajua thamani halisi ya eneo hilo? wanajua historia ya majengo hayo? mbona wazungu hawabomoi ya kwao huko london kwetu ndo vp? tunajua wajenga hoja mmefuta au mtafuta ila ipo siku nafsi itawauma na hamtakuwa na nafasi ya kutuomba msamaha please dont be stupid!
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom