Mwekezaji aichongea TRA

Gudboy

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
867
77
na Irene Mark

MWEKEZAJI wa Kiwanda cha Nguo cha CAMI cha jijini Dar es Salaam, ameulalamikia uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa urasimu na ukiritimba unaokwamisha shughuli zake.


Ukiritimba na urasimu unaofanywa na TRA ulibainika jana, baada ya Kamati ya Bunge ya Biashara na Uwekezaji kutembelea kiwanda hicho.

Wakiwa kiwandani hapo, Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Maurice Lezmi, alisema analipia dola za Marekani 300 kila mwezi kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa kwa ajili ya ghala ambalo TRA wamemzuia kulitumia.

Sababu za kushindwa kutumia ghala hilo ni uchafu ambao TRA wanauelezea kuwa mali waliyoitaifisha baada ya mmoja wa wafanyabiashara waliokuwa hapo kushindwa kulipa deni.

Mfanyabiashara wa awali ilikuwa Kampuni ya Star Apperel, inayoelezwa kudaiwa na TRA, hali iliyosababishwa kuzuiwa kwa takataka hizo ambazo ni vipande vya nguo chakavu vinavyodaiwa kuwa mali yenye thamani.

Hata hivyo, Lezmi alisema anashindwa kusafirisha kontena nne za nguo kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kipindi cha baridi kutokana na TRA kutompa nyaraka zinazoruhusu usafirishaji wa mzigo huo kwa zaidi ya siku 15 hadi jana.

Alisema, meli inayotakiwa kusafirisha kontena hizo inaondoka keshokutwa (Jumatatu) lakini hadi jana, hakuna majibu yeyote wala ukaguzi uliofanywa na TRA kwa ajili ya kuruhusu kuondoka kwa mzigo huo.

“Leo ni siku ya 15 tangu nipeleke nyaraka TRA kwa ajili ya kutaka ruhusa ya kusafirisha kontena hizi zenye nguo maalumu kwa ajili ya kipindi cha baridi nchini Marekani, lakini hadi sasa hakuna majibu, hali inayonipa wasiwasi, huenda nikapata hasara.

“Kuhusu hilo ghala…tangu Juni mwaka jana nilipoingia mkataba na TRA kwa ajili ya kulitumia sijakabidhiwa bado na kila mwezi nalipa dola 300 kwa sababu ndiyo makubaliano yetu.

“Nashindwa kuendeleza biashara yangu kwa ajili ya uzembe…nahisi kuna ukiritimba na urasimu utakaonisababishia hasara, sijaridhishwa kabisa na hali ya uwekezaji nchini. Nashawishika kuwazuia wenzangu kuja kuwekeza hapa,” alisema kwa masikitiko Lezmi.

Kwa upande wake mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema hali hiyo inatokana na Mamlaka ya Mapato na idara nyingine za serikali kufanya kazi kwa mazoea na ubabe.

“Hili ni tatizo kubwa jamani sijawahi kuona mwekezaji analalamikia jambo kama hili…lakini ni lazima idara za serikali ziache kabisa kufanya kazi kwa mazoea na ubabe kwa sababu tutakwamisha maendeleo ya taifa kwa mwendo huu,” alisema Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Kyela (CCM).

Akitoa msimamo wa kamati hiyo, Mwenyekiti wake William Shelukindo, alisema ziara hiyo imeibua jambo ambalo lisipofanyiwa kazi kwa haraka litasababisha nchi kukosa wawekezaji wenye mitaji, mitambo na kutoa ajira kwa vijana.

Shelukindo, alisema iwapo TRA itashindwa kuondoa uchafu uliopo kwenye ghala hilo kwa haraka na kuhakikisha mizigo ya mwekezaji huyo kabla ya kusafirishwa, watawajibika kwa kuwa wanazuia fursa za uwekezaji nchini.

“Tunaahidi kurudi baada ya kikao kijacho cha Bunge ili kuona kama huu uchafu umeondolewa au bado…kwa nini mwekezaji mzuri mwenye uwezo wa kuajiri vijana zaidi ya 800 kwa kipindi cha mwaka mmoja, anyanyasike kiasi hiki?

“Nahisi kuna mchezo mchafu wa rushwa unafanyika hapa, sasa tunaitaka TRA kuwajibika kwa hili haraka sana…huyu akiwaeleza wenzake au kupata hasara kwa kushindwa kusafirisha nguo zake itakuwa hasara kwa nchi. Watu watakosa ajira na pato la taifa litaporomoka,” alisisitiza Shelukindo.

Kiwanda hicho kilianza kazi Juni mwaka jana, kina lengo la kuajiri vijana 1,000 kwa mwaka lakini hadi sasa tayari kimewapatia ajira vijana 800, wengi wao wakiwa wasichana. Hata hivyo juhudi za Tanzania Daima, kumpata Mkurugenzi wa TRA, Harry Kitillya zilishindikana.

TANZANIA DAIMA
 
Tuna njaa ya wawekezaje na sifa na ndio maana wanasiasa wetu pia hujidhalilisha kusema tu bila kutumia akili, maana kwa kweli mimi sioni kama ni tatizo mpaka kamati iambiwe. Kama wanalipia bila kutumia ghala si wadai fidia kwa TRA. Hata mkataba wao hawajatuonyesha kujua ukweli wa mambo.
 


“Kuhusu hilo ghala…tangu Juni mwaka jana nilipoingia mkataba na TRA kwa ajili ya kulitumia sijakabidhiwa bado na kila mwezi nalipa dola 300 kwa sababu ndiyo makubaliano yetu.

Du ghala for tht price for a month? Ni wapi huko???????
 
Mahakama za biashara zipo,mikataba ipo.Natumai huyu kama ni mzungu hawezi kuwa na mkataba usio kuwa na kipengele ambacho kinahusu kudai fidia pindi mambo yakienda ndvyo sivyo na hatokua muoga wa kukatisha/vunja mkataba wenyewe pindi ikibainika kuna hasara kama ilivyo mikataba yetu mibovu,kila kukicha utasikia tukiivunja tutapata hasara nk.
Ni vema akasimamia mkataba unasemaje,na kuichukulia hatua TRA ikibainika kweli uzembe upo.Ili iwe fundisho kwa taasisi zetu zenye uzembe kiutendaji.
 
Tuna njaa ya wawekezaje na sifa na ndio maana wanasiasa wetu pia hujidhalilisha kusema tu bila kutumia akili, maana kwa kweli mimi sioni kama ni tatizo mpaka kamati iambiwe. Kama wanalipia bila kutumia ghala si wadai fidia kwa TRA. Hata mkataba wao hawajatuonyesha kujua ukweli wa mambo.

Nyie ndo wale wale mnaopenda kufanya kazi kwa mazoea!

So ulitaka huyo mwekezaji asilalamike wakati kamati imemtembelea hapo kwake na kumuuliza kama anapata matatizo yoyote? Suala la kwenda mahakamani ni lingine kabisa! cha msingi hapa kamati ilitembelea kiwanda kile kujionea shughuli zake, impact yake kny uchumi wetu, matatizo wanayopata, na mawazo au ushauri wanaopenda kutoa kwa serikali ya TZ......! and that's what they had to say!

Tatizo lenu nyie mmezoea kumung'unya maneno sana......we need to call a spade, spade......! TRA na vitengo vingine vya serikali wanatakiwa kubadili utendaji wao wa kazi, sio kufanya kazi kwa mazoea tu!
 
kuna maghala cheaper kuliko hilo mzee, hapa hapa bandarisalama. lakini nadhani alimaanisha $3000


Sasa hii nini tena mkuu????? habari inasema $300 watu tunashangaa, wewe hutaki tushangae for a reason kwamba yapo hata cheaper than that. Then unaweka maneno mdomoni kwa the so called mwekezaji kwamba alimaanisha $3000.

Typical uswahili!
 
Back
Top Bottom