Mwaswali kwa PM Pinda

hakuna cha kumsikitisha maana ndo utaratibu wa ccm kuwadanganya wananchi hivyo wakati fedha za maendeleo zinatokana na kodi za watanzania wote
 
nipo hapa namsikiliza...jamaa anaustadi mkubwa sana wa kujibu....ingefaa angekua ni waziri mku kwa nchi kama Sweeden mambo yageenda vyema sana...ila siasa za bongo wabongo bila msukumo wa biti viongozi hawaendi...Heko PM kwa busara zako na utashi wako.

mkuu huyu jamaa anakujibu kwa hekima kama yupo kanisani...tatizo lake kutekeleza majibu yake ndio shughuli hopo. Ukija kumuuliza tena anakujibu majibu matam zaidi ya yale ya awali.
 
Mh. Kilango- Samaki wanaouzwa nje dola bil. 1.3 ambazo ni mara tatu ya mapato tunayopata TZ. mauzo haya yanafanywa na nchi ya kati (middle part).

PM- tatizo ni kuuza mazao yetu bila kusindika ndo maana tunazidiwa na wenzetu. Serikali inajitahidi kutumia Export processing Zone ili kupunguza pengo hili.
 
Mh. Kasembe wa Masasi-Tatizo la korosho Mikoa ya Mtwara na Lindi

PM. tatizo ni upangaji wa bei dira halaf bei ya soko inabadilika ndo shida inapoanzia. Msimu huu 70% imelipwa, 30 % bado.
Inatakiwa bil. 29 na takwimu atapewa governor wa BOT leo ili hela zitolewe na serikali imedhamini mkopo huo kwa 100%

Sio kama maswali ya papo kwa papo ya pinda hayana tija ,yanapoteza muda ,kuibia serikali fedha zisizo za msingi .pinda anajibu kama sio kiongozi yeye kila wakati tutaangali ,tutajaribu ,tunafuikiria majibu gani hayo kiongozi mkuu wa serikali .ajibu kama sokoine pinda hajiamini ,wala sio mtoto wa mkulima hana uzalendo wa taifa kama sokoine ,kama wangalikuwa wanapiga kura mtu wa kufa basi sokoine tungempigia kura uafufuke ili wafe wengine kama hawa wanaopiga majaramba wapotezee hatuna waziri mkuu tanzania ipo figure tu .
 
Umeshangaa nini? Ulitegemea majibu gani kwa swali technical toka kwa watu wenye busara zao kama Mbowe? Hakuna jibu ni aibu tu kwa Pinda na serikali yao dharim. Kwanza Ndugai angelijua swali hilo angemzuia kuuliza au kumnyima nafasi. Aibu tupu kwa serikali. Wamedhihirisha jinsi wanavyovunja katiba ya nchi waziwazi na watanzania wameona wenyewe.
 
Jamani Auulize kuhusu hela viongozi wetu walizoweka njee zitarudishwaje? Zinakadiriwa kufikia Trilion 9
 
...

Wapo pale ku-justify their illegal existence
nimekugongea LIKE!
Yaani hawa viongozi wetu wanashangaza sana, swali likiulizwa na Mpinzani, wao wanajipanga kulipangua badala ya kulijibu. AIBU!
 
naibu spika wa bunge amesema wapigiwe makofi kidogo sbb wao kama kamati ndio walienda uingereza kupambana na wakafanikiwa kuirudisha hiyo chenchi ya rada,(na hili linahitaji pongezi kweli?)waliohusika na wizi huu wa fedha ya rada wamechukuliwa hatua gani?kwa nini uwajibikaji umekuja kutokea wakati wa kudai tu na sio wakati wa kuzuia wizi?
yaaani tuwapigie makofi kwa kwenda kufuata chenji wakati tuliwalipa posho?na wale waliosababisha ulanguzi huo wamechukuliwa hatua gani????bila shaka ni job ndugai aliyeongea kauli hiyo huyu jamaa hajawahi kuwa upande wa wananchi hata siku moja,tumbo lake kwanza,,wananchi baadae,aibu hakika bunge la jamhuri ya muungano lina masipika badala ya speakers.
 
Imesikitisha sana PM akijibu swali la Mh. Mbowe kwa nini baadhi ya viongozi wakati wa kampeni wanatoa vitisho kuwa fedha za maendeleo hazitapelekwa huko kama hawachagui wagombea wa CCM.

Waziri mkuu ak kama hayo yalisemwa ni wakati wa mapambano na ni unfortunate tu!


Ndugu zangu JF naomba mwongozo maana kweli nimesikitika sana na jibu hili hata baada ya Mbowe kumuomba atoe tamko la serikali. Kwa nini PM hakukemea matamko hayo? Je kauli ya serikali ni kujustify upotoshwaji? Ni mapambano ni unfortunate!! Mimi Mtz niliyeangalia jibu hilo bado naumia sana moyoni nipeni mwongozo nifanye nini kuhusu hili.

Na Naibu spika unaruhusu mna move on na maswali mengine kama hili swali la msingi la uvunjaji wa katiba na kuingilia Bunge ambao ndio wanagawa fedha za maendeleo katika bajeti halijibiwi?

Usijali. Tumefungua kesi Igunga kupinga ushindi wa ccm, hoja mojawapo ni hii ya mawaziri kutumia uwaziri wao kupiga siasa. Kumbuka Magufuli kule aliahidi madaraja ili kafumu achaguliwe. Mahakama ikileta longolongo zake tunatumia nguvu ya umma!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Maswali yameisha ngoja nikanywe Jack Daniel kidogo

Hahahah!mapema sana mkuu,angalia usi Kanumbe!mwenyewe niko na kiu lakini navuta muda mpaka lunch time,ndio uzuri wa kua mjasiri wa kutafuta mali (ujasiliamali)
 
Back
Top Bottom