Mwaswali kwa PM Pinda

Bitabo

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
1,900
687
1. Mh Mbowe amuuliza PM juu ya kauli za CCM na serikali eti wakichagua wapinzani majimbo yao hayatapata fedha za maendeleo. Mf. ni kauli ya Mary Nagu kwenye kampeni Arumeru,
Ole Medeye huko Meru, Magufuli huko Igunga

Pm. Anasikitishwa na ahayo japo si kweli, na anafikiri Watanzania waendelee kujenga demokrasia ya kweli. kauli za kwenye mapaambano ya uchaguzi ni mambo unfortunate lakini sheria zitaendelea kusimamiwa kwa kufuata katiba.
 
Mh. Kasembe wa Masasi-Tatizo la korosho Mikoa ya Mtwara na Lindi

PM. tatizo ni upangaji wa bei dira halaf bei ya soko inabadilika ndo shida inapoanzia. Msimu huu 70% imelipwa, 30 % bado.
Inatakiwa bil. 29 na takwimu atapewa governor wa BOT leo ili hela zitolewe na serikali imedhamini mkopo huo kwa 100%
 
Mh. Kairuki-Wastaafu wa TAZARA wanadai mafao tokea 2007 na serikali imekuwa inatoa kauli mbali mbali ambazo hazitekelezwi.
PM. Mafao imekuwa ni tatizo kidogo kwa wastaafu, serikali inakamilisha kutoa hela kwa awamu tatu za bil. 7 kila awamu. Mawaziri husika wa Zambia na Tanzania wametakiwa kukutana ili kuboresha huduma za TAZARA
 
nipo hapa namsikiliza...jamaa anaustadi mkubwa sana wa kujibu....ingefaa angekua ni waziri mku kwa nchi kama Sweeden mambo yageenda vyema sana...ila siasa za bongo wabongo bila msukumo wa biti viongozi hawaendi...Heko PM kwa busara zako na utashi wako.
 
1. Mh Mbowe amuuliza PM juu ya kauli za CCM na serikali eti wakichagua wapinzani majimbo yao hayatapata fedha za maendeleo. Mf. ni kauli ya Mary Nagu kwenye kampeni Arumeru,
Ole Medeye huko Meru, Magufuli huko Igunga

Pm. Anasikitishwa na ahayo japo si kweli, na anafikiri Watanzania waendelee kujenga demokrasia ya kweli. kauli za kwenye mapaambano ya uchaguzi ni mambo unfortunate lakini sheria zitaendelea kusimamiwa kwa kufuata katiba.

Hivi CDM hawawezi kutumia KAULI hizi za KIBAGUZI kumvua UBUNGE yule FISADI wa mikataba tata ya MADINI Peter Dalali Kafumu (Igunga CCM)
 
Hili la kusema mkichakua wapinzani hakuna maendeleo, nadhani ndio tusi kubwa sana katika demokrasioa... kuliko hata kumtuka mgombea mwenziko kama yale ya Arusha! ....kwa nchi ni hatari sana maana iko siku mtasema mkichakua Mkristo, au Musialam imekula kwenu......

1. Mh Mbowe amuuliza PM juu ya kauli za CCM na serikali eti wakichagua wapinzani majimbo yao hayatapata fedha za maendeleo. Mf. ni kauli ya Mary Nagu kwenye kampeni Arumeru,
Ole Medeye huko Meru, Magufuli huko Igunga

Pm. Anasikitishwa na ahayo japo si kweli, na anafikiri Watanzania waendelee kujenga demokrasia ya kweli. kauli za kwenye mapaambano ya uchaguzi ni mambo unfortunate lakini sheria zitaendelea kusimamiwa kwa kufuata katiba.
 
Imesikitisha sana PM akijibu swali la Mh. Mbowe kwa nini baadhi ya viongozi wakati wa kampeni wanatoa vitisho kuwa fedha za maendeleo hazitapelekwa huko kama hawachagui wagombea wa CCM.

Waziri mkuu ak kama hayo yalisemwa ni wakati wa mapambano na ni unfortunate tu!


Ndugu zangu JF naomba mwongozo maana kweli nimesikitika sana na jibu hili hata baada ya Mbowe kumuomba atoe tamko la serikali. Kwa nini PM hakukemea matamko hayo? Je kauli ya serikali ni kujustify upotoshwaji? Ni mapambano ni unfortunate!! Mimi Mtz niliyeangalia jibu hilo bado naumia sana moyoni nipeni mwongozo nifanye nini kuhusu hili.

Na Naibu spika unaruhusu mna move on na maswali mengine kama hili swali la msingi la uvunjaji wa katiba na kuingilia Bunge ambao ndio wanagawa fedha za maendeleo katika bajeti halijibiwi?
 
Mh. Mangungu (kama sijakosea jina)- tatizo la mfumuko wa bei, serikali inachukua hatua gani
PM- Bei ya vyakula ndo inachangia sana mfumuko wa bei, serikali inatumia njia za kupunguza bei ya vyakula kama sukari, unga, n.k. japo serikali haijapata suluhisho la moja kwa moja na sasa mafuta nayo yamazidi kupanda bei.
PM anaomba Watanzania kushirikiana na serikali ili kutatua shida hii hasa wafanyabiashara ambao wanatoa bei zisizo na uhalali na bidhaa husika.
 
Mh. Mohamed- Mwaka wa bajeti 2011/12 ndo unaishia ila taasisi za serikali hazina fedha, je ni kweli seriakli imefilisika au mipango ya serikali haitekelezeki?

PM- serikali haijafilisika maana hata wabunge msingekuwa hapa bungeni ila bajeti ni kali kidogo na serikali inapunguza matumizi kwenye bajeti. Hatutakwama ila tutafika mwisho wa mwaka tukiwa tumefunga mikanda sana.
 
Nimemsikiliza lakini ana tabia ya kutaka kuhurumiwa kwenye ukweli na anasikitika pasipo masikitiko kwani hilo alikuwa hajalisikia kutoka kwa Mawazir wenzake akina Nagu, Maghufuli na wengine? Hizo kauli zimekuwa zikitolewa na zinamegua mshikamano na ujamaa aloujenga Mwl J.K ni za kukemea sana ili demokrasia ichukue nafasi.
 
" Paundi 29 hivi na point"hajataja kiwango kamili kwa nini.Huo ndio umakini Wa waziri mkuu(mkuu ktk Serikali)?Alikuwa akizungumzia chenchi ya rada baada ya kuulizwa swali.
 
Mwigulu- Chenji ya rada imerudi kiasi gani na hizo fedha zitaenda lini kwenye sekta ya elimu kama ilivyokubaliwa na kwa utaratibu gani?

PM- Kweli pound mil. 29.5 (bil. 72.3 tshs) na ziko BOT. fedha ziende kwenye matumizi ya vitabu kwa primary school. fedha zitaneda tamisemi na wizarani. matumaini ni kuwa zoezi likienda vizuri, tatizo la vitabu litapungua sana ila tumefungua account maalum pale BOT na CAG apewe nafasi ya kufanya ukaguzi wa kina kuona matumizi yake yawe yaliyokusudiwa
 
Mh. Gekul- ni miaka almost 3 serikali kutoa pembejeo kwa wakulima ila pembejeo zinachelewa kupelekwa.

PM- Aliyepewa tender last year alichelewa kutoa vocha naz ikabidi abadilishwe ndo maana pembejeo zimechelewa. CAG ameagizwa akague utaratibu huu wa vocha kama unamnufaisha mkulima japo this year hazitachelewa
 
Naibu spika Wa Bunge amesema wapigiwe makofi kidogo sbb wao Kama kamati ndio walienda Uingereza kupambana na wakafanikiwa kuirudisha hiyo chenchi ya rada,(na hili linahitaji pongezi kweli?)Waliohusika na wizi huu Wa fedha ya rada wamechukuliwa hatua gani?Kwa nini uwajibikaji umekuja kutokea wakati Wa kudai tu na sio wakati Wa kuzuia wizi?
 
Dont expect anything from Pinda or Makinda or Ndugai pale mjengoni.

Wapo pale ku-justify their illegal existence
 
Back
Top Bottom