Mwanzo wa Mwisho wa Sisiemu Ulianzia huku!

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,963
10,460
Dalili za kufa kwa sisiemu zilianza siku nyingi sana, sema tu ilikuwa inatuwia vigumu baadhi yetu kugundua. Mambo haya yalianzia vijijini, ndio yakaja kwa akina Buwagi na Richmond

Ilianzia hivi.

Viongozi wauza Ardhi ya Kijiji

na Mwandishi Wetu, Tarime

MGOGORO wa ardhi kati ya viongozi wa Kata ya Kibasuka na wananchi wa Kijiji cha Nyakunguru wilayani hapa mkoani Mara, umefikia mahali pabaya baada ya wananchi kudai kuwa, wametishiwa kuuawa kama wataendelea kuhoji uuzwaji wa ardhi ya kijiji chao.
Mbali na kutishiwa kuuawa, wananchi hao wanadai pia kuwa wamekuwa wakipokea vitisho vya kubambikiwa kesi za mauaji iwapo wataendelea kulilalamikia suala hilo kupitia kwa viongozi wa ngazi za juu na vyombo vya habari.
Wananchi hao walitoa kilio chao jana katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mbunge wa Tarime, Zakayo Wangwe, kijijini hapo.
Wangwe alifika kijijini hapo kufuatilia chanzo cha mgogoro huo uliosababisha wanachi kutokuwa na imani na viongozi wa kijiji na kata.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kijijini hapo, Sairo Wambura, aliwaongoza wananchi hao na kudai kuwa, viongozi waliojichukulia ardhi bila ridhaa ya serikali ya kijiji hicho, wamekuwa wakiwatisha wananchi kuwa watawaripoti katika Jeshi la Polisi kuwa, walihusika katika mauaji ya watu kadhaa ili wapate kesi za mauaji na hivyo kukosa nafasi ya kufuatilia suala hilo.
Walimwambia mbunge wao kuwa, tayari watu watatu, akiwemo Mwenyekiti wa CCM wa Kijiji cha Nyakunguru, wameunganishwa katika kesi za mauaji kwa madai kuwa ni moja ya mbinu za kuwanyamazisha.
Inadaiwa kuwa, watu hao walikamatwa na kuunganishwa katika kesi hiyo baada ya taarifa zilizotolewa polisi na baadhi ya viongozi wa kijiji na kata, wakiongozwa na ofisa mtendaji wa Kata ya Kibasuka, Rhobi Matugura.
Wakazi hao waliwakataa viongozi hao mbele ya mbunge wao na kuamua kumuondoa madarakani Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji, Abel Maginga na kamati yake.
Aidha, waliiomba Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, itangaze uchaguzi mdogo wa kuziba pengo hilo, sambamba na kuitaka serikali iwahamishe mara moja watendaji wake wanaotuhumiwa kujihusisha na sakata hilo.
Waliwataja wanaodaiwa kubambikiwa kesi za mauaji kuwa ni Mwenyekiti wa CCM wa kijiji hicho, Julius Magebo Magige, Chacha Mwita Gotono na Maro Seba.
Inadaiwa kuwa baadhi ya viongozi wa kijiji na kata ya Kibasuka, wamejichukulia ardhi kinyemela, na eneo lipatalo ekari 10 tayari limeshauzwa kwa mgodi wa dhahabu wa North Mara.
Viongozi wanaodaiwa kuhusika katika njama hizo, ni pamoja na diwani wa kata hiyo, John Mayo, Ofisa Mtendaji Rhobi Matugura, Mratibu Elimu Kata, Adriano Johanes, Mwenyekiti wa Kijiji, Abel Maginga, Mwenyekiti wa Kitongoji, Timas Chacha sambamba na wajumbe wa kamati ya fedha na mipango ya kijiji hicho.
Viongozi hao wanadaiwa kuchukua eneo lenye ukubwa wa ekari 24, na kuuza matofali 30,000 yaliyokuwa kwa ajili ya ujenzi wa shule. Tayari ekari 10 zimeshauzwa kwa Kampuni ya North Mara likiwemo jengo la ofisi ya CCM.
Kampuni hiyo imekiri kununua eneo hilo kwa sh milioni 6.2, fedha ambazo pia hazijulikani zilipo hadi sasa.
Baada ya kusikia malalamiko hayo, Wangwe alisema atayafikisha kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Magufuli, kwa hatua zaidi.
Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa Kijiji cha Nyakunguru na kata hiyo ya Kibasuka, walikanusha kuhusika na uporaji wa ardhi na kubambika watu kesi za mauaji, huku wakikiri kuwa suala la uuzaji wa ardhi lilifanyika kwa baraka zote za wananchi.
Diwani wa kata hiyo, Mayo na Mratibu Elimu Kata, Johanes, walisema wanao ushahidi wa nyaraka, ambazo zinaonyesha kuwa wananchi walikubali kuuza ardhi hiyo kwa kutia saini zao katika nyaraka hizo, jambo ambalo linapingwa vikali na wananchi wanaodai kuwa nyaraka hizo ni za kugushi.

Ikaja hivi

na Mwandishi Wetu, Musoma 7/4/2007

VIONGOZI wa kijiji kimoja mkoani Mara, wameuza eneo la ekari 10 kwa kampuni ya uchimbaji madini na kusababisha malalamiko kutoka kwa wananchi.
Miongoni mwa maeneo ambayo yako ndani ya ardhi iliyouzwa na viongozi hao katika mazingira ya kutatanisha na ambayo tayari yameanza kulalamikiwa, ni shule moja ya msingi na ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambazo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika kiujenzi.
Hatua hiyo ya viongozi wa kijiji imesababisha malalamiko juu ya uuzwaji huo wa ardhi, na sasa suala hilo limeshafikishwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na viongozi wa CCM, ambao wanalalamikia kuuzwa kwa ofisi yao kinyemela.
Habari ambazo Tanzania Daima imezipata zinaeleza kuwa, tayari Mkuu wa Mkoa wa Mara, Isidori Shirima, ameombwa kuingilia kati mgogoro huo wa ardhi unaofukuta katika Kijiji cha Nyamichare, Kata ya Kibasuka wilayani Tarime.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake 20 aliofuatana nao, Katibu wa CCM wa Kijiji cha Nyamichare, Sairo Wambura, alidai mbele ya waandishi wa habari mjini hapa kuwa, baadhi ya viongozi hao, wakiongozwa na mwenyekiti wa kijiji hicho, Abel Maginga, wameuza ardhi yenye ukubwa wa ekari 10.
Alidai kuwa, ardhi hiyo iliuzwa mwaka jana kwa wamiliki wa mgodi wa dhahabu wa North Mara.
Wambura alizidi kudai kuwa, ardhi hiyo iliyouzwa bila ya ridhaa ya serikali ya kijiji hicho, inajumuisha eneo la Shule ya Msingi Nyakunguru C na ndani yake kulikuwa na jengo la ofisi ya CCM, ambalo lilikuwa katika hatua za awali za ujenzi.
Alidai kuwa, baada ya kuuza eneo hilo, viongozi hao sasa wako mbioni kuuza pia eneo lililosalia la ekari 24, katika mazingira hayo hayo ya siri, huku uongozi wa mgodi wa North Mara ukiwa mbioni kulifanyia tathimini kabla ya kulinunua kwa lengo la kupanua eneo la mgodi.
Alifafanua kuwa, wamejaribu kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufikisha malalamiko yao katika ngazi husika za kata na wilaya, lakini hawakupata msaada wowote na ndiyo maana wameamua kuuomba uongozi wa mkoa uingilie suala hilo.
Uongozi wa CCM wilayani Tarime umekiri kupokea malalamiko hayo ya kuuzwa kwa ardhi hiyo, likiwemo jengo la chama hicho na kuongeza kuwa, Oktoba mwaka jana, uliwaandikia viongozi wa Kata ya Kibasuka ukilalamikia kitendo hicho, lakini hadi sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kurekebisha kasoro hizo.
Kwa upande wao, uongozi wa mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick, umekiri kununua eneo hilo kutoka kwa uongozi wa kijiji hicho cha Nyamichare kwa gharama ya sh milioni 6.2 na kufafanua kwamba, wananchi wanapaswa kuwasiliana na viongozi wao ili kupata taarifa sahihi ya manunuzi hayo.
Shirima alipoulizwa kuhusu suala hilo, alikiri kupokea taarifa za malalamiko hayo na akaahidi kumuagiza Mkuu wa Wilaya (DC) ya Tarime, Stanley Kolimba, kulitafutia suala hilo ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Ikaja tena
Moto CCM, mwenyekiti adundwa, ofisi yafungwa

2007-03-26 16:05:33
Na Frank Mbunda, Temeke
Kitimtim cha aina yake kimezuka katika ofisi moja ya chama cha Mapinduzi Jijini Dar es Salaam ambapo Mwenyekiti inasemekana ametembezewa mkong`oto usio wa kawaida na kisha ofisi yake kutiwa kufuli na yeye pamoja na viongozi wenzake kuonywa kutokanyaga humo tena.

Zahama hilo limetokea katika tawi la Matumbi, kata ya Temeke 14.

Wananchama hao wenye hasira wanadaiwa kumdunda Mwenyekiti wao wa tawi, Bw. Yusufu Pwim (Tolu), wakimtuhumu yeye na katibu wake Bw. Suleiman Majebele, kuhusika na uuzwaji wa eneo la chama.

Hatua ya kipigo na kuwazuia viongozi hao kukanyaga katika eneo hilo, imefuatia malalamiko ya wanachama hao kwamba viongozi hao wameliuza kwa siri eneo hilo kwa mama mmoja.

Mwenyekiti huyo alipotakiwa kueleza nini kilitokea hata kufikia hatua hiyo, aligoma kusema lolote huku akiwalaumu wanachama waliohusika na kipigo dhidi yake kuwa ni wahuni na wasiojua maadili ya uongozi ndani ya chama.

`Sitaki kusema lolote kuhusu hilo, hawa wahuni, lakini wajue kwamba mimi ni kiongozi niliyechaguliwa, waache waendelee na vurugu zao,` amesema Bw. Pwim, huku akiondoka katika eneo hilo.

Alasiri ilipowasiliana na Katibu wa CCM wa Wilaya aliyetambuliwa kwa jina moja la Bw. Matoroka, kufuatia tukio hilo, amekiri kutokea kwa vurugu hizo katika tawi hilo.

`Ni kweli nilikwenda katika tawi la CCM Matumbi, kulitokea kutokuelewana baina ya wanachama na viongozi wao, lakini tumezungumza na mambo yamekwisha,` akasema Bw. Matoroka.

Amesema kikao hicho cha usuluhishi, anaamini kitarejesha hali ya amani.

Hata hivyo Katibu huyo amekanusha madai kwamba viongozi hao wa tawi wameliuza eneo hilo la chama, na akasema wanachama walipotoshwa na baadhi ya watu kwamba eneo hilo limeuzwa.

`Niliambiwa kwamba Mwenyekiti alipigwa, nimeonana naye, tumeyazungumza na kurekebisha kasoro na tofauti baina yao na wanachama, pia tumekubaliana yaishe, na kuwaomba wanachama waifungue ofisi ya chama` akasema Bw. Matoroka.

Kwa upande wake Katibu wa Tawi hilo, Bw. Majebele, alipotakiwa na Alasiri kutoa ufafanuzi wa suala hilo, alisita kueleza kilichojitoleza kwa madai kwamba yeye si msemaji wa CCM.

`Ni kweli hapa kuna matatizo baina yetu kama viongozi wa tawi na wanachama, lakini kama unavyojua CCM inaongozwa kwa misingi bora, hivyo si kila mtu ni msemaji wa jambo lolote linalohusu chama na mali zake, bali msemaji wetu ni Katibu wa CCM wa Wilaya,` akasema Bw. Majebele.

Awali ilielezwa na wanachama hao kuwa Bw. Pwin, alipigwa akituhumiwa kuwa kinara katika kundi la viongozi wa tawi hilo wanaodaiwa kuhusika na hujuma uuzwaji wa eneo hilo.

Wakizungumza na Alasiri jana usiku, baadhi ya wanachama, walidai kuwa baada ya mwenyekiti huyo kupata kipigo, sasa wanajiandaa kumchapa Katibu wa tawi hilo, Bw. Majebele.

Kwa mujibu wa baadhi ya wanachama wa tawi hilo, viongozi hao wawili wanadaiwa kuuza eneo hilo kwa mama mmoja mkazi wa Upanga, ili aweze kujenga kituo cha mafuta.

Wanachama hao wamedai kuwa eneo hilo lenye maduka na vitega uchumi vingine lilizinduliwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Rashid Mfaume Kawawa, Simba wa Vita, mwaka juzi.

Wanachama hao wamedai kwamba pamoja na kikao hicho kilichofanyika jana na kumalizika jioni baina yao na Katibu wa Wilaya, lakini pia hawatakuwa tayari kuifungua ofisi hiyo ili kuruhusu viongozi hao kuendelea na kazi.

`Hatutaifungua ofisi hii, mpaka hapo Mzee Kawawa atakapoelezwe wazi na viongozi wa tawi kwamba eneo hili la CCM limeuzwa na kubadilishiwa matumizi,` wakadai wanachama


Kwa hiyo Uharamia wa akina Buzwagi haujaanza katika ngazi za juu katika sisiemu. huu ulikuwa ni muendelezo tu wa yale yanayotokea ngazi za chini.
 
CCM..chama cha mapinduzi,
mapinduzi ya nani
mapinduzi ya nini

Mapinduzi ya Wakulima na wafanyakazi, lakini ni mapinduzi ya aina gani, ni mapinduzi ya kuwadidimiza kiuchumi Leo ukimuuliza Mtanzania aliyeishi enzi za Ukoloni, atakuambia ni heri wakolini wa Kizungu wangerudi kuliko hawa wanamapinduzi tulio nao.

Wakulima na wafanyakazi wengi wao ni maskini wa kutupwa, bendera ya CCM imebeba jembe na nyundo huku ikiwatupilia mbali wahusika.

Ama kweli CCM imeleta mapinduzi.
 
Back
Top Bottom