Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanzo wa mwisho wa michango mikubwa ya sherehe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NGULI, Dec 20, 2010.

 1. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,819
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nimekuwa nafuatilia jinsi desturi ya kuchangia na kufanya sherehe kubwa inavyozidi kushika kasi, ikipelekea ule wigo wa kuomba michango kupanuka kiasi kwamba sasa hata mtu ambaye jina lako halijui vizuri anaweza kukuomba mchango.

  Aidha michango na sherehe hizi zimekuwa mzigo mkubwa sana kwa baadhi ya watu, ikiwa ni pamoja na wale wenye kipato kidogo wanaochangiwa na kulazimika kulipa michango hiyo kwa miaka mingi. Je, wajua kuwa kuna familia ambazo zimefikia kulazimisha ndugu wauze mashamba au mifugo mtaji ili kupata fedha za kuchangia sherehe?. Je, wajua kuwa kuna watu ambao zaidi ya nusu ya kipato chao wanatumia kuchangia sherehe na huku wakishindwa kulipia huduma muhimu kama shule, matibabu, lishe, nk. Na kuwa wakati mwingine wewe au mimi (au wengine kama mimi na wewe) ndio wenyeviti na makatibu wa sherehe hiyo?.

  Na ni sisi tunaoona fahari ya kutumia milioni 30 au zaidi kwenye sherehe usiku mmoja?
  Kuna kijana mmoja jamaa yetu juzi juzi alipata shule Australia akawa anatafuta mchango wa dola 5,000 aende. Alipata 2,000 na amwekwama kwenda.

  Mwaka kesho akisema anaoa tutamchangia milioni 15-20!!!. Hii si hadithi, ni ukweli, na ni kielelezo cha ulimbukeni tuliofikia.

  Siku za karibuni nimetambua kuwa kuna kundi kubwa tu linasikitishwa na huu mwenendo, na hata kutambua kuwa tunaweza kuwa tunaandikiwa dhambi kubwa (na hukumu yatusubiri) kwa jinsi wengi wetu tunashindwa kusaidia mambo ya msingi lakini tunakuwa wepesi kutoa kwenye sherehe. Wengi wanaamini kuwa tumeshatumbukia kwenye lindi la mazoea ambapo hatuwezi kujitoa mpaka upepo uje ubadilike wenyewe!.
  Mimi nafikiri wasomi tuna jukumu muhimu la kuwa chachu ya mabadiliko pale ambapo mazoea yenye madhara yanavuka mipaka na kuweza hata kuwa chanzo cha ufukara na kuviza maendeleo.

  Ili kubadilisha hili jambo, lazima tuanzie mahali. Mimi napendeleza na kuanza kutekeleza. Kuanzia Januari 2011, nitapunguza michango ninayotoa.

  Nitatoa tu kwa mtu wa karibu sana, na nitachanga kidogo. Usishangae nikakuchangia 20,000/= kama ulitegemea 50,000/= kwa mfano. Kuanzia July 2011, nitaacha kabisa kuchangia sherehe. Badala yake nitakuwa nachangia elimu pale ambapo mzazi hayupo au mhusika kweli hana uwezo na pia nitachangia miradi mingine ya jamii na maendeleo.

  Je waniunga mkono? Kama ndiyo sambaza huu ujumbe kwa mtandao wako.

  Dr. D.R.Olomi
  Box 35036
  Dar es Salaam, Tanzania
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,234
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Nimeshangaa juzi nimetumiwa minutes za kikao cha harusi yenye bajeti ya Mil 21 huko Dar, eti nichangie...Kwa hili nitaonekana mbaya, hawapati mia yangu!
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 27,106
  Likes Received: 5,298
  Trophy Points: 280
  Kuchangia harusi ni gharama kubwa sana.
  Unatoa pesa ya mchango, unanunu zawadi ya maharusi na inabidi uweke mafuta mengi kwenye gari ili kuweza kushiriki kwenye harusi.
  Mi sioni haja ya watu kuchangiwa.
  Mmependana, nendeni kanisani rudini nyumbani yatosha
   
 4. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,517
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ni ulimbukeni na hauna tija milion 20 mnaichoma siku moja.

  Baada ya harusi wachangiaji na maharusi ni majuto kwenda mbele.

  Kuna watu wamechangiwa mapesa tele wakanunuliwa na mazawadi tele na mzazi wa mwanamke. Mume hata nyumba yakuweka hizo zawadi hana kapanga chumba na sebule.


  Sherehe ikawa kabambe ya mamilioni,
  bora wangempa bwana harusi hata 5 m akakate kakiwanja pugu.

  Hii tabia ni butu kabisa haina maendeleo.
   
 5. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  ndoa zenyewe za mawazo... hazidumu...
   
 6. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,314
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Tunatoa kwa sababu tunaona aibu tunapoombwa . Inabidi tuwaelimishe wanoomba kwanza waone aibu ya kuomba michango ndipo hali hii itaisha maana duh. Nilikuwa na kadi
  15 za harusi kwa mwezi Nov. na Dec. Nilitoa mchango 3 na zote nikasusa kwenda kuonyesha kuunga mkono hoja hii.
   
 7. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,819
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Pia ukiona mtu hujawasiliana nae kwa muda mrefu akikupigia usipokee simu hio ni KADI ya mchango
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,983
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Watu wepesi sana kuchangia minuso mikubwa mikubwa waombe wakuchangie kwenye ugonjwa unatolewa patupu mgonjwa akifa utawaona kwenye mazishi wanavyo toa michango mikubwa mikubwa
   
 9. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #9
  Dec 20, 2010
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,383
  Likes Received: 399
  Trophy Points: 180
  mi niliacha jamani, mwanzoni ilikuwa kama utani utani tu nawaambia watu sichangii lakini nimeweza kweli hata ofisini mtu akija na kadi namwambia tu hapo hapo kuwa samahani mi huwa sichangii harusi na hata harusi yangu sintafanya sherehe. hiyo ni baada ya kuzidiwa na michango na kukosana na watu kibao kisa sijachangua harusi zao "gadem"
   
 10. Hero

  Hero JF-Expert Member

  #10
  Dec 20, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 570
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Yaani jambo hili kumbe linakera kila mtu eeh! Kama umechangiwa, basi unaweza kuchangia kwa hao waliokuchangia, kwa kuwashukuru kwa kusema asante!
  Unajua ndio maana ndoa nyingi za kifahari hazidumu! Maana watu wametoa kwa manug'uniko sasa baraka itoke wapi? Mie nafikiri cha maana ni kufunga ndoa, mengine ni kufuru tu. Tena utakuta watu wameleeewa ile mbaya!
  Mie niko nawe mtoa hoja, nilishapunguza sana kuchangia, na kama ukiiniita kwenye kamati ndo kabisa siji. Unakuwa na kadi 10 na kila moja ina kiwango cha 50,000/= utafikiri wanajua badget yako!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 11. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #11
  Dec 20, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,819
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ha ha ha ha kumbeeee eeh inawezekana aiseee:teeth:
   
 12. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #12
  Dec 20, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,101
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
 13. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #13
  Dec 20, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,819
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
   
 14. RR

  RR JF-Expert Member

  #14
  Dec 20, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,633
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 160
  Mtu anaanza kukupigia baada ya miaka mitano.......anajizoeza kupiga siku tatu...siku ya nne, mchango! :redfaces::redfaces:
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Dec 20, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 65,144
  Likes Received: 16,105
  Trophy Points: 280
  Uwiano kati ya michango ya miradi ya maendeleo na michango ya mambo ya burudani pengo lake ni kubwa sana.

  Laiti watu wangekuwa na hamasa ya kuchangia mashule, hospitali, ujenzi wa maktaba n.k. pengine tusingekuwa na shule ambazo ziko chini ya miti au huenda tusingekuwa na wagonjwa wanaolala kwenye sakafu za simenti!!

  Lakini minuso ya harusi na upuuzi mwingine kama huo ni full kujiachia mfukoni. Ajabu sana.
   
 16. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #16
  Dec 20, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nguli na wengine,

  Naanza kufarijika kuwa jumuiya inayonizunguka inaanza kuona hili. Wakati nakuja Tanzania toka huko nilikuta mambo haya yamepamba moto sana. Sikuwahi kuhisi wala kujua kuwa watu huchangishana na kuamua kuangamiza kiasi kikubwa kama hiki kwa muda mfupi sana. Wakati huo kuna jamaa yangu ndugu alitualika kwenye kikao alichokiita Kikao cha ukoo. Kufika kwenye kikao nikaambiwa kikao cha harusi.

  Nilikataa kuchangisha na nikawapa darasa kuwa kwenye ukoo wetu kuna vijana wengi ambao wangeweza kuchangia harusi kam wangekuwa wamewezeshwa kwenye elimu. Nikawaambia na wakakubaliana nami kuwa kweli kwenye ukoo wako ambao walishindwa kuendelea na shule kisa kukosa ada! Mimi nilikataa wazi kuwa siishi kwa kuteketeza fedha kwa siku moja. Tangu wakati huo nimeishi kwa dunia ninayoiamini mimi. Ulifika wakati dini ikanilazimisha nifunge ndoa. Nilikubali kwa kuwa mama yangu alinisihi ili arudi kundini.

  Nilifunga ndoa. Ndoa yangu haikuwa na watu zaidi ya 20. Na niliwaalika na kulipia bili kama niendavyo baa. Kidogo kidogo wadogo zangu kwenye ukoo nao wakafata nyayo zangu. Niongeapo sasa hivi tuko kwenye mchakato wa kuanzisha mfuko wa elimu wa ukoo. Tunataka mwanaukoo yeyote asishindwe kuendelea na shule kisa kakosa ada. Baada ya hapo tutaendelea na jamii inatotuzunguka hadi hapo tutakapotokomeza ujinga kijijini kwetu.

  Ni wakati muafaka kwa Watanzania wote kuacha mtindo huu wa kuchangisha fedha nyingi kwa sherehe badala yake wawekeze kwenye kuchangishana kwa elimu. wakati fulani huko Kenya utasikia bandiko " FAMILIA YA SO AND SO INAKUKARIBISHA KWENYE HARAMBEE YA KUMCHISHIA MTOTO WAO ANAYEENDA KUSOMA MAHALI FULANI" na believe me wamefanikiwa sana. Why not us? Harusi ni suala ambalo ni very personal, wenzetu hagharimiakia shughuli hizi kwa mifuko yao sio kutegemea mifuko ya watu.

  Kama ni kuiga TUACHE SASA!
   
 17. S

  Sina pa kwenda Senior Member

  #17
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani msilaumu tu unajua watu wanachangisha sababu nao walikuchangia ndio hivyo inavyoenda sasa wewe unalaumu coz ushamaliza shughuli yako sio
   
 18. mapango

  mapango Member

  #18
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Ni tabia mbaya sana tuliyoizoea, nimeichukia sana, hivyo kweli mil20 kwa harusi? mimi pesa kama hizo naoa wake 20! na sherehe nafanya, watakula pilau na nyama!, tuache ujinga!
   
 19. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #19
  Dec 20, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,711
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  acheni ubahili bana, changieni harusi ili tuujaze ulimwengu, kuna kila dalili kwamba utajaa karibuni.
   
 20. L

  Leornado JF-Expert Member

  #20
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hii kitu kweli kabisa, kuna jamaa nilikuwa nae facebook, karibia miaka mitatu hatujawasiliana zaidi ya kwa marafiki FB, ghafla mwezi uliopita nikashangaa kanisalimia ghafla..msg iliofata baada ya slamu akaniambia anaoa mwezi huu na kafurahi saana kuwasiliana na mimi.... nilimweleza ukweli kuwa hali si nzuri. Chat ikaishia hapo hapo lol
   
Loading...