Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Mwanza wamtaka Kikwete ajiuzulu
na Mwandishi wetu, Mwanza
CHAMA cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti nchini (RAAWU), mkoani Mwanza kimewataka Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Mambo ya Ndani Shamsi Vuai Nahodha waachie ngazi mara moja kutokana na kashfa ya Dowans na vurugu zilizosababisha maafa na vifo vya raia mkoani Arusha.
Mwingine ambaye ametakiwa kujiuzulu ni Inspekta Jenerali wa Polisi Said Mwema. Wanadai viongozi hao watatu wameshindwa kutimiza vema wajibu wao na maamuzi yao tata yamesababisha maafa ambayo yangeweza kuepukika.
RAAWU pia imewataka Watanzania kutoogopa wanaposimamia na kutetea haki zao za msingi Kikatiba kwani ni dhahiri kwamba serikali ya Rais Jakaya Kikwete imeyumba mno na imekosa mwelekeo wa kiutawala.
Kauli ya RAAWU ilitolewa jana na Katibu wa RAAWU Kanda ya Ziwa, Ramadhan Mwendwa, katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima juu ya mustakabali wa nchi.
Alisema Rais Kikwete hawezi kukwepa kashfa ya Dowans ambayo sasa serikali inalazimika kuilipa mabilioni ya shilingi wakati maisha ya wananchi yakiwa duni. Dowans ndiyo ilirithi mikoba yaRichmond ambayo ilibebwa na Baraza la Mawaziri chini ya Rais Kikwete na kupewa mradi wa kufua umeme wa dharura huku wakijua kuwa haikuwa na uwezo huo.
"Sisi RAAWU tunashawishika kuamini kwamba Rais Kikwete ameshiriki moja kwa moja katika mkataba wa Dowans, ndiyo maana ameshindwa kuueleza umma juu ya kampuni hii. Inaonekana hapa kuna mchezo mchafu unafanywa na viongozi wetu... haiwezekani serikali inatangaza kulipa mabilioni ya fedha bila Bunge na Baraza la Mawaziri kuridhia" alisema Mwendwa.
Aidha, Mwendwa alimmwagia sifa nyingi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kwa kukataa Dowans kulipwa mabilioni hayo ya fedha, na kusema: "Waziri Sitta anajua ujanja unaochezwa hapa."
Vile vile, alihoji sababu ya serikali kuendelea kuilipa kampuni ya IPTL, huku ikilisukumia mzigo Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO) lilipe fedha hizo wakati mikataba imesainiwa na serikali.
Alisema IGP Mwema na Waziri Nahodha wameonekana kushindwa kuwatumikia Watanzania, ndiyo maana idara zao zimeanza kutumia nguvu kwa kuua raia wasiokuwa na hatia.
"Polisi haina mamlaka ya kupiga risasi na kuua wananchi wanaoandamana kwa amani, tena hawana silaha wala hawajafanya fujo. Kwa maana hiyo, tunataka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na IGP Mwema waachie madaraka yao haraka sana" alisema.