Mwanza: Wabunge wawili wa CHADEMA wapigwa mapanga na mmoja yupo hoi!

Duh! siasa za Nchi hii sijui zitatufikisha wapi. Anyway; Zitto simamia huo mchakato ili makamanda waliojeuriwa wahudumiwe ipasavyo na hatimaye warudi kulikomboa Taifa.
 
Chama cha wahuni kinaendeshwa kihuni! Wizi, dhuluma na mauaji ni siasa au nini? Poleni sana waheshimiwa!

Jeshi la polisi tunahitaji kuona meno yenu juu ya uhuni wa hao wapuuzi waliofanya upuuzi huo! Ieleweke wazi haya mambo yakiachiwa yatapelekea machafuko nchi hii, na mambo yakiharibika hakuna ambae atakua salama,si viongozi wala familia zao! Wote hatutokua salama kwa ajili ya u j. i n ga wa watu wachache
 
Tupo Hospitali ya Bugando hapa. Ndg. Kiwia, mb anatoa maelezo kwa maafisa wa polisi.

Hali ya ndg. Kiwia sio nzuri sana. Anatakiwa kufanyiwa ct scan kuona athari aliyopata (maana kapigwa na shoka na mapanga kichwani). Bahati mbaya hapa Bugando kifaa hicho hakifanyi kazi.
Sala zangu kwa Mb Kiwia, nasikia uchungu usio kifani
 
Hali ya ndg. Kiwia sio nzuri sana. Anatakiwa kufanyiwa ct scan kuona athari aliyopata (maana kapigwa na shoka na mapanga kichwani). Bahati mbaya hapa Bugando kifaa hicho hakifanyi kazi.
poleni,nawashauli mpelekeni kiwia regencý sio mhìmbilì maana ct scan ya mhimbili ni kanyaboya
 
Hiyo ndo CCM bwana!! This is very sad. Cha kushangaza kuna majitu bado wanaona CCM ndo baba na mama. Huko wapi Rejao ulete ujinga wako.
 
Siasa za Tanzania zinazidi kujidhihirisha kuwa hazina tofauti na nchi nyingine za Kiafrika. Chama cha siasa kuwa na makundi ya wahuni na kupiga watu ni hatari na chama hicho kinakosa 'moral' authority ya kutawala.
pamoja kamanda, tunaomba apatikane kwanza huyo Ahmedi Kilindi halafu watu wengine watakuja kupatikana
 
Mpaka hapo tutakapo badilisha katiba na kufanya cheo cha IGP kuwa mtu wa kuajiliwa na si kuteuliwa na Rais nchi yetu itaendelea kuwa na Polisi CCM au hata polisi Chadema. Hapa kwa wenzetu IGP angewajibishwa. Haya madudu yanafanywa na CCM kwa kushirikiana na Polisi. Jana huko Kiwira watu wamepigwa mabomu baada ya polisi kuambiwa kuna watu wanapeana rushwa! this is shame
 
Tupo Hospitali ya Bugando hapa. Ndg. Kiwia, mb anatoa maelezo kwa maafisa wa polisi.

Kuna mmoja wa majeruhi ambaye yupo hapa mwanzoni alisema yeye ni mtu wetu na ameumizwa pia. Imegundulika ni mtu wa UVCCM, Ahmed Mkilindi ambaye ndiye alikuwa anaongoza kikosi kilichowavamia kina Kiwia. Amepata jeraha mkononi (friendly fire?). Mwenyekiti wa CCM mkoa yupo hapa kaja kumwona. Nimewaambia Polisi mtu huyu asitolewe hospitali kinyemela bali atoe maelezo polisi kwanza. Huyu ni mtuhumiwa wa kwanza kabisa.

Hali ya ndg. Kiwia sio nzuri sana. Anatakiwa kufanyiwa ct scan kuona athari aliyopata (maana kapigwa na shoka na mapanga kichwani). Bahati mbaya hapa Bugando kifaa hicho hakifanyi kazi.

Nimezungumza na Katibu wa Bunge na ndani ya muda mfupi ndg. Kiwia atasafirishwa kupelekwa Muhimbili kwa uangalizi zaidi.
Ndg. Machemuli anaendelea vizuri alitoka hospitali jana (alipata huduma ya Kwanza Sekou Toure).

Siasa za Tanzania zinazidi kujidhihirisha kuwa hazina tofauti na nchi nyingine za Kiafrika. Chama cha siasa kuwa na makundi ya wahuni na kupiga watu ni hatari na chama hicho kinakosa 'moral' authority ya kutawala.

Tusubiri uchunguzi zaidi wa Polisi. I am so depressed
Hiki kitendo ni cha kulaaniwa na watanzania wote bila kujali itikadi zetu za vyama.
 
Yaani sasa ccm siasa za kistaarabu wameamua kuzipa kisogo, huku wakina machemba na lusinde wanapotomosha mitusi mbele ya wazazi na watoto wetu waliojitolea kwenda kuwasikiliza katika mikutano yao, huku tena wameunda kikosi cha mauaji kama utawala wa mabutu, sasa ni dhahiri ccm inaelekea kufa jamani ni heri 2015 ifike haraka tumalize kazi tuondokane na balaa hili aghfff
 
Poleni makamanda wetu hizo ndio baadhi ya gharama za kuongoza mapambano ya ukombozi!

Hakika vitisho, nguvu na hata mauaji yanayofanywa na ccm hayatazima moto wa mabadiliko unawaka nchi nzima sasa!! Msife moyo tupo nanyi pamoja wakati huu mgumu! Silikilizia muziki wa hapa Arumeru watakapojaribu kchakachua kura zetu! Huenda usa river ikageuka taharir square na safari ikaanzia hapa kwenda magogoni!!
 
If the story is true then the situation is now getting out of control! It is serious! Something has to be done about this or else the nation will slip into political chaos!

I think it is going to be the beginning of the era whereby every political leader in Tanzania ranging from a street/village chairman to a member of parliament is armed with a number of bodyguards.

Where are we heading to as a nation? All this violence just for a ward election?
 
Jamani na mambo haya ya Tamaduni za wenzetu mtawauwa watu kwa presha jamani mi wasiwasi wangu umeanzia kwanza kwa chanzo cha habari pili namna habari ilivyoandikwa.
 
pamoja kamanda, tunaomba apatikane kwanza huyo Ahmedi Kilindi halafu watu wengine watakuja kupatikana

Huyo Ahmed Kilindi ndi prime suspect!tunataka kuona polisi wanakua serious na ili,wasilete mzaha hata kidogo.hata kama kuna wafanya biashara wakubwa wamehusika na ili nao wawe kwenye mikono ya sheria,hakuna kulindana tena sababu ya pesa zao!
 
Yaani sasa ccm siasa za kistaarabu wameamua kuzipa kisogo, huku wakina machemba na lusinde wanapotomosha mitusi mbele ya wazazi na watoto wetu waliojitolea kwenda kuwasikiliza katika mikutano yao, huku tena wameunda kikosi cha mauaji kama utawala wa mabutu, sasa ni dhahiri ccm inaelekea kufa jamani ni heri 2015 ifike haraka tumalize kazi tuondokane na balaa hili aghfff
2015 ni mbali sana mkuu hatuwezi kuona damu zinaendelea kumwagika tukae kimya tukisubiri 2015!! hapana right time ikija tutaenda ku occupy magogoni!!
 
Kwanni wanafanya unyama huu? Kule Arumeru mpaka sasa ndugu Omary maarufu kama Matelephone mpaka sasa hajulikani alipo... CCM wakiongozwa na Beno Malisa wamemteka...huu ushenzi sasa ufike mwisho
 
Oh.. That's too much...
The RAPE of DEMOCRACY from CCM, but time will tell.
Let the justice take place..
Get well soon all comrades.
 
Tupo Hospitali ya Bugando hapa. Ndg. Kiwia, mb anatoa maelezo kwa maafisa wa polisi.

Poleni sana Zitto... Hali ya sasa inatisha.

Lakini kuna jambo moja hapa... Mbali na kupeleka taarifa polisi, vyombo vya habari vimehabarishwa??? Kuandika humu JF peke yake haitoshi. Jambo kama hili linatakiwa lichukuliwe kwa uzito wa hali ya juu. Na wananchi wote tuhabarishwe..

Mara nyingi napata hisia za kuwepo TV huru ya kidemokrasia.. Vitu kama hivi vya kinyama, vinapaswa vikemewe na dunia nzima.
 
Back
Top Bottom