MWANZA KWACHAFUKA: wadau wa sensa waandamana hadi kwa DC baada ya serikali kushindwa kuwalipa.

Alfu Lela Ulela

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
1,255
77
Habari kutoka Mwanza ni kuwa walimu na wadau wengine wa sensa waliokuwa wakiendelea na semina ktk ukumbi wa shule za sekondari Mwanza na Pamba wameingia mtaani na kuandamana hadi kwa mkuu wa wilaya baada ya kumaliza semina leo lakini serikali kushindwa kuwalipa fedha zao.

Taarifa za ndani zinasema tangu juzi serikali ilikuwa inahaha kupata fedha hizo na iliposhindikana, DC wa Nyamagana aliamua kukimbia ofisi na hajaonekana tangu asubuhi. Magari ya polisi yenye maji ya kuwasha na askari wenye silaha wanaendelea kufika eneo hilo na kutishia umati huo kutawanyika...
 
Tunaiomba serikali ijipange vizuri kuhusu zoezi hilo muhimu..vinginevyo tutatia mashaka kuhusu usahihi wa takwimu zitakazopatikana.
 
hili zoezi limeshaingia doa toka zamani sana na halitakuwa na ufanisi wowote......zitatoka takwimu zikionyesha tanzania ina jumla ya watu mil.19..tuko hapa
 
Kweli serikali ijipange upya wenyeviti wa mitaa na vijiji wamesema wanashangaa wao kuambiwa wahamasishe sensa bila malipo wakati wabunge walilipwa sh. milioni moja kila mmoja ili kuhasisha sensa na hawahamasishi!wamesema wao watakaa nyumbani wahesabiwe kama wananchi wengine.
 
Inawezekana serikali inafanya makusudi ili wapate sababu ya kusimamisha zoezi la sensa kwa kisingizio kuwa watendaji wao wamegoma kumbe wameshindwa kuwadhibiti wanaotaka kipengele cha dini kisiwepo na hata sasa wanatishia kukwama kwa zoezi hilo. Pia walifanya makosa makubwa sana kuwaacha waalimu na kuchukua magraduate waliomtaani ambao walishajijengea imani kuwa serikali haiwezi kutekeleza mambo yake mpaka kwa njia ya migomo. Wamekuwa wakigomea pesa zao za kujikimu wakiwa chuoni mara nyingi ndipo wanazipata, sasa wanaendeleza silaha hiyo hadi mtaani.
 
they better abscond the censor thing.
walau itakuwa fundisho kwa dhaifu kikwete
 
Inawezekana serikali inafanya makusudi ili wapate sababu ya kusimamisha zoezi la sensa kwa kisingizio kuwa watendaji wao wamegoma kumbe wameshindwa kuwadhibiti wanaotaka kipengele cha dini kisiwepo na hata sasa wanatishia kukwama kwa zoezi hilo. Pia walifanya makosa makubwa sana kuwaacha waalimu na kuchukua magraduate waliomtaani ambao walishajijengea imani kuwa serikali haiwezi kutekeleza mambo yake mpaka kwa njia ya migomo. Wamekuwa wakigomea pesa zao za kujikimu wakiwa chuoni mara nyingi ndipo wanazipata, sasa wanaendeleza silaha hiyo hadi mtaani.

Serikali itajuta kuchukua graduate kwenye zoezi hili.
 
Chonde chonde Rais wetu; chukua hatua kuhakikisha hili zoezi linafanikiwa japo limeshavurugika kwa kiasi cha kutisha. Nisingefurahi uwe Kiongozi wa kwanza kushindwa hata kuhesabu watu wako! Itakuwa ni failure na aibu ya mwaka kwa serikali yako.

Serikali inayoshindwa kuhesabu wananchi wake itaweza nini sasa? Ni rai yangu tusifike huko; tumia kila uwezo na mamlaka uliyo nayo kufanikisha hili.
 
Bila kuweka wazungu au wachina hakuna DHAIFU aliwezalo.imesha ingia doa wala takwimu tutakayopewa sintoiamini hata kidogo.ingekua kwa hisani ya watu wa marekani hapo ningeamini
 
Habari kutoka Mwanza ni kuwa walimu na wadau wengine wa sensa waliokuwa wakiendelea na semina ktk ukumbi wa shule za sekondari Mwanza na Pamba wameingia mtaani na kuandamana hadi kwa mkuu wa wilaya baada ya kumaliza semina leo lakini serikali kushindwa kuwalipa fedha zao.

Taarifa za ndani zinasema tangu juzi serikali ilikuwa inahaha kupata fedha hizo na iliposhindikana, DC wa Nyamagana aliamua kukimbia ofisi na hajaonekana tangu asubuhi. Magari ya polisi yenye maji ya kuwasha na askari wenye silaha wanaendelea kufika eneo hilo na kutishia umati huo kutawanyika...
.
M4C inaendelea huko Mwanza kwenye Semina ya walimu na Sensa habari zaidi tutawaletea live
 
Back
Top Bottom