MWANGOSI nakulilia

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Daud Mwangosi,ulale salama,
Ulikupata mkosi,ukatuacha nyuma,
Wamekuua Polisi,tena bila huruma,
Mwangosi nakulilia.

Ukiwa kazini,unajitafutia kipato,
Umejawa umakini,ili kutunza watoto,
Polisi mahayawani,wakaleta habari nzito,
Mwangosi nakulilia.

Channel Ten,kituo chako cha kazi,
From then,umewaachia majonzi,
Yes we can,wataindeleza kazi,
Mwangosi nakulilia.

Ni nzima Tanzania,utaratibu unafahamika,
Polisi wafanya hima,kombe kufunika,
Wenyewe hawana bima,milele kufika,
Mwangosi nakulilia.

Tume imeshaundwa,uchunguzi kufanya,
Tayari imeshashindwa,ushahidi kukusanya,
Polisi wanapondwa,kwa wanayoyafanya,
Mwangosi nakulilia.

Sikia ahadi yangu,Hayati Mwangosi,
Polisi adui zangu,hata kwenye kadamnasi,
Nitamaliza hasira zangu,nikiamua kuasi,
Mwangosi nakulilia.

Raha ya milele umpe ee Bwana,na mwanga wa milele umwangazie.Apumzike kwa amani.Amina.

ulikuwa kaka yetu, tulikutegemea kwa kila kitu,
hatuamini macho yetu kama wewe leo tena si kitu,
hatutoacha kukulilia katu, milele utabaki kweye mioyo yetu,
mshangao kwa kila anayekufahamu, hatuamini kama umekufa kwa bomu,
kaka mwangosi hivi kweli we ni marehemu? bora ungeugua tukakuuguza hata tusingelaumu,
 
tutakukumbuka siku zote. hakika kaka yetu damu yako iliyo mwagika ni sawa na mbegu ya ngano iliyo zikwa aridhini.
Itaota nakutoa matunda mengi na mazuri
 
Kyala akusaje malafyale, umalile imbombo pa kisu! Nu jesu bhalingoghile pakikohekano pa bhupoki gwitu. Lambalala kikolo, utukwaghanila kumwanya kwa tata!:amen:
 
Wosia tayari nilishaandika, kwa wanangu katika zote rika. atakayechagua kazi upolisi, atafunwe na mnyama nyika. Nduguze wasijekanyaga, mazishini kumzika. Polisi wa Tanzania, ni kazi ilolaanika.
 
MNYIKUNGU umetoa maneno makali na mazito kwa mtu yoyote atayesoma. Hakika Mwangosi amekuwa si kitu tena mbele ya polisi bali ni nyamanyama na mautumbo tu!!! THIS IS UNFAIR.

FROM MY HEART, SOMETHING MUST BE DONE, AND I WILL DO IT.

ulikuwa kaka yetu, tulikutegemea kwa kila kitu,
hatuamini macho yetu kama wewe leo tena si kitu,
hatutoacha kukulilia katu, milele utabaki kweye mioyo yetu,
mshangao kwa kila anayekufahamu, hatuamini kama umekufa kwa bomu,
kaka mwangosi hivi kweli we ni marehemu? bora ungeugua tukakuuguza hata tusingelaumu,
 
Tutakukumbuka daima,
kwa uzalendo uloonesha,
haki za wandishi wa habari kupigania,
ukawa mwiba kwa mafisadi,
na tunu kwa wanyonge,
tutaenzi mapambano uloanzisha,
upumzike kwa amani kaka
 
Inaumiza sana watanzania wenzangu, try to think, what's inside mwangosi's family? mke na watoto wanajua baba amekwenda kutafuta riziki, kumbe maguberi polisi wamemuangamiza, Mungu atalipa tu, yeye ndiye kila kitu
 
Mwangosi tulikupenda, Mungu kapenda zaidi, mipolisi ikakutenda, kwa maagizo ya mafisadi, roho zao zina inda, wamekufisha kigaidi, nafsi zetu zimenyonda, kisasi tunaahidi, M4C itasonga, damu yako kama UDI, malipo ni hapahapa, maadamu wa duniani. PUMZIKA KWA AMANI!
 
MNYIKUNGU umetoa maneno makali na mazito kwa mtu yoyote atayesoma. Hakika Mwangosi amekuwa si kitu tena mbele ya polisi bali ni nyamanyama na mautumbo tu!!! THIS IS UNFAIR.

FROM MY HEART, SOMETHING MUST BE DONE, AND I WILL DO IT.
unajua kwa mtu yoyote aliyekuwa anamfaham mwangosi hawezi kukubali wala kuamini namna alivyotupotea ghafla,saa nyingine najiuliza au tumepelekwa somalia bila wenyewe kujijua? kama ni hapa tanzania je ni ile tanzania tuliyokuwa tunaambiwa kuwa ni kisiwa cha amani?, kwa kweli nawaza mengi, nimeishiwa nguvu, sijawahi kuona wala sikutarajia kuona kifo cha aina ile kwa mtu ninayemfahamu tena kwa nchi yetu ya tanzania.

mtu alikuwa kazini akitafuta mkate wake wa kila siku na pia akitimiza wajibu wake wa kutuhabarisha, polisi bila aibu wakamshika wakampiga kisha wakamuua, HIVI HUU NI UNYAMA KIASI GANI, YAANI BADALA YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU TUNAAGA MANYAMA YA MAREHEMU HUU UKATILI HAUKUBALIKI, AMINI USIAMINI UKIONA MOSHI UNAFUKA BASI JUA CHINI PANA MOTO UNAWAKA, NAWAAMBIA DAMU YA MWANGOSI NA WOTE WALIOUWAWA KWA UONEVU WA POLISI BADO ZITAHITAJI KULIPA KISASI, ZAMANI TULIKUWA TUNABAMBIKIZIWA KESI NA KUFUNGWA BILA HATIA, LAKINI SIKU HIZI WAMEANZA KUTUUA BILA HATIA.TUUNGANE PAMOJA NA TUCHUKUE HATUA.
 
Ni kilio na huzuni kuu moyoni,hivi hawa wanaotuua wataishi milele?R.I.P kamanda Mwangosi umefia vitani ukitafuta haki ya taifa hili....
 
Kyala akusaje malafyale, umalile imbombo pa kisu! Nu jesu bhalingoghile pakikohekano pa bhupoki gwitu. Lambalala kikolo, utukwaghanila kumwanya kwa tata!:amen:

botukombeka mwangosi mwipomba, kale ajege nani omo mwipomba, onsangalofu ongolofu ikojaga nano omomwipomba
 
botukombeka mwangosi mwipomba, kale ajege nani omo mwipomba, onsangalofu ongolofu ikojaga nano omomwipomba
Bhasangarufu habha bha gholofu bhisa, bhisa kuja na tata gwa kumwanya. Ngupasya umbili gwangu...................
 
Tangulia tangulia Mwangosi tangulia, tutakufuata ukifika kwa wapendwa wetu huko wasalimu, Mwambie Mwalimu Nyerere tupo na wanafunzi wake wameamua kutuuwa kwa njaa, kuzidisha matabaka, kuuwa waandishi, jeshi lake limekuwa chinja chinja.. wafikishie salaam zangu wote wapenda mabadiliko tunakuja na daima hatutawasahau.
 
Ameliza wengi. Demokrasia inaendelea kubakwa na ccm kila kukicha lkn sisi tuna mungu wkt wao wana mabomu na risasi za moto. Itafahamika tu
 
Tunamlilia wote ndugu, nice shairi. Amefungua macho ya dunia (though in a sad way) to see and learn about this inhumane, corrupt, vicious, Dumb and coward Tanzanian Government treats her own people. Unfreakin' Believable!
 
Mmejaliwa ubunifu wa mashairi wana JF. sote tunamlilia Mwangosi RIP
Tunamlilia wote ndugu, nice shairi. Amefungua macho ya dunia (though in a sad way) to see and learn about this inhumane, corrupt, vicious, Dumb and coward Tanzanian Government treats her own people. Unfreakin' Believable!
 
  • Thanks
Reactions: kui
Back
Top Bottom