Mwandosya na Maji!

Tz. kazi ipo, kila kitu siasa. Prof hana hulka ya kupiga porojo ambapo kwa wabongo utaambiwa ni kiburi, lakini hata kama ana kiburi na hiyo ndio hulka yake, jee tumhukumu kwa hiyo hulka au kwa utendaji wake!

Nina mfano mmoja pengine utasaidia kuona tatizo katika sekta hiyo liko wapi. Hivi sa upo mpango mkubwa tu wa usambazaji maji nchini unaogharimiwa na Benki ya dunia lakini wilaya nyingi zilichelewesha kuanza utekelezaji kutokana na watalaamu waliko kwenye Halmashauri za Wilaya kushindwa kuwasilisha project writes up zao, hadi JK kumuomba Mwandosya apeleke wataalamu toka pale wizarani kwenye wilaya kusaidia utekelezaji wa kazi hiyo.

Wenye uelewa zaidi wa mradi huo wanaweza kuweka data sawa sawa lakini mimi nimetumia hapa kutokana na maelezo ya Profesa mwenyewe na JK alipokuwa ziarani Mbeya mwaka jana.

Sasa kama wataalamu wetu dio kikwazo, kosa la waziri hapa liko wapi, nitaomba kusaidiwa!
 
Mwandosya angalikuwa Rais wa Tanzania basi mambo ya JK na mabarabara tunayo lia leo ingalikuwa ni mara 10 jamaa ni mkabila na kiburi sana mwache ashinde kwenye maji .Abakie kuwa Rais wa Mbeya tu .

Una ukweli, lakini ana busara za kuwa akiwa Rais wa Tanzania atajua kuwa si Rais wa Mbeya, ni kweli ana kibiri na ni jeuri lakini ana uwezo wa kuwa Kiongozi wa Taifa na si mbabaishaji na mzugaji. Hawezi kuendesha nchi ki-ushkaji.
 
Mwandosya anaweza kuwa rais mzuri sana wa Tanzania lakini anayo mambo mengi ya msingi anayopaswa kubadilika haraka sana.
1.Ukosefu wa umakini,Mwandosya ndie aliekuwa waziri wakati ttcl ikiuzwa na alishindwa kuutumia uprofesa wake mpaka hali ambayo mnaiona kwa sasa,watu wengine wanahusisha jambo hili na rushwa kitu ambacho mimi binafsi sikiamini bali nahisi ni uwezo wake wa kazi.
2.Ukabila,uwanja wa ndege alipokuwa mawasiliano akaupeleka mbeya.akateua kina davd Ngonya kwenye bodi,akateua Mwaitenda kwenye bodi na alipowekwa tu mazingira akamteua mbungw wa viti maalum wa kyera Hilda Ngoye kuwa mwenyekiti wa nemc
Hapana mnaompenda mwambieni abadilike.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom