Mwandosya na Lipumba wafanyiwa upasuaji India

Kama Lipumba yuko India kwa operesheni
Kama Malecela alikuwa UK kwa operesheni

Hayati Nyerere alitibiwa na kufia UK
Hayati Diria alitibiwa na kufia Germany

Inamaana baada ya miaka 50 ya uhuru,tuna madokta/maprofesa feki hapo Muhimbili kama hata viongozi wetu hawawaamini.

Sasa Muhimbili wanatibu watu weak,poor na ni walala hoi.
Howa many botched operations ambazo hatujui?

Kazi yao kwenda kutibiwa South Africa na huko South Africa kuna madokta kibao wa tanzania wanapiga mzigo vizuri tu.
tatizo vitendea kazi hakuna madokta wapo tena wazuri ila tatizo lipo serikalini hawataki kununua vifaa vya mahospitalini
 
Ukweli halisi ikiwa hospital zetu zitapatiwa vifaa vinavyohitajika na wataala wake wakilipwa vizuri huwezi kumsikia mtu kwenda kutibiwa nje. tatizo ni kuwa serikali imezitelekeza hospital hizo na hakuna anayejali iwapo huduma zinazotolewa zinaendana na idadi ya wataalam waliopo wala utaalam waliosomea. Wengi wanafanya kazi chini ya kiwango kutokana na upatikanaji wa vitendea kazi. So tusiwalaum kuwa wanafanya kazi mbaya
 
Tupo pamoja nanyi wazee na tunawaombea kwa mola mpone haraka, mpate nguvu, mrudi muendelee kulitumikia taifa letu.
 
Waugue tu mbona sisi ndugu zetu wanalazwa mzungu a nne kule mwananyamala?? keshokutwa utawasikia wanasifia et tumeboresha huduma zaafya....thubutu mbona hakuna alienda hata basi KCMC? sie twende Mwananyamala tukamaliziwe kabisa na wao waende huko kwa kodi zetu tena. ningefurahi sana kwamba yule Dokta wa Muhimbili angempasua huyo mmoja pafu badala ya figo na huyo mwingine angepasuliwa kichwa badala ya uti wa mgongo ndio wange-feel the pain familia zile ilipata kipindi kile. Tena chozi linanitoka, sitaki wapone kwanza wakae huko huko na kodi zetu wazile tu ziishe
 
Ee bwana toa pole bila hiana.
Utajashangaa unakufa wewe au ndugu yako wa karibu kutokana na roho mbaya.
Kumbuka , hata adui yako muombee isije kupata balaa unayofikiria wewe haiwezi kukupata.
Wagonjwa viongozi poleni sana na wapone haraka.
kuna wakati waweza fanya hivyo na ikawa ina maana lakini kuna nyakati ambazo unaomba huyo adui yako atoweke kabisa...haya wapone haraka warudi waendeleee kutunyonya hadi tukakuke
 
MJIMPYA said:
Tatizo kila kitu kimekuwa siasa, ulimwengu wote hauwezi kuwa sawa ndg. Kuna specialisation of labour.
Mfalme wa Saudi Arabia juzi alikuwa matibabu New York, rais wa Venezuella kwa sasa yuko Cuba kwa matibabu.
Sasa unashangaa nini wao kwenda India?
Mungu atawaponya.
Poleni sana

MJIMPYA,

..hapana bwana. ifike mahali ukweli usemwe.

..kama suala ni "specialization" kama unavyodai, mbona hatuoni hata kiongozi wa Comorro akija kufanyiwa upasuaji Muhimbili?

..huduma wanazokwenda kupata viongozi wetu huko nje ni za kawaida sana ambazo tulipaswa kuwawezesha Madaktari wetu wenyewe ili waweze kuzifanya.

..huyo Mfalme wa Saudia aliyekwenda Marekani bila shaka is looking for a cutting edge/very rare procedure ambayo iko hapo New York na si mahala pengine.

kuna wakati waweza fanya hivyo na ikawa ina maana lakini kuna nyakati ambazo unaomba huyo adui yako atoweke kabisa...haya wapone haraka warudi waendeleee kutunyonya hadi tukakuke
Mola hakosi kukusikia ndugu, nina uhakika kesha kuingiza kwenye diary yake.
 
Wote uliowata ni wanasiasa ndio waliotusabishia umaskini. Wanajua vipimo hapa kwetu ni tatizo, dawa ndo hivyo hata vyumba godoro na kitanda shida. Wameamua wapate huduma bora nje ya nchi wakitumia hela nyingi walizotuibia watanzania huku watanzania maskini tukifa kwa njaa, umaskini na maradhi. Hata kama tuna maprofesa bila dawa na vifaa ni sawa na rubani akiwa hana ndege hivyo haitumii elimu yake kwa manufaa ya taifa.
 
Aaaa,wataalam wa muhimbili,bugando na kwingnwko wa nini?????ndio maana watumishi wa afya,walimu na wataalam wengine hawalipwi ipasavyooooo......mzee malecela alienda UK now amepumzka USA,nyerere alienda UK,

Ina maana kikombe cha babu kimeshindwa mpaka waende India?
 
Mola hakosi kukusikia ndugu, nina uhakika kesha kuingiza kwenye diary yake.
kwani nimesema vibaya hadi unichanganishe na Mola?? nimesema ukweli wangu tu naomba sana usinichonganishe na Mola namuogopa sana na kesho jumapili naenda kutubu. Enjoy ur weekend hata kitu/kiti moto siendi kula tena naondoka zangu na simu nazima mshaanza kunichonganisha na Mungu
 
Kweli jamaa hakutakii mema, anakuchonganisha na .........., hata hivyo kesho fanya kweli mkuu.
 
Wataalamu wapo wenye ujuzi wa kutosha,kama mazingira yangeboreshwa kina mwandosya wasigeenda nje, tatizo ni kutelekeza yetu twaenda kwa watu
Madaktari wa tanzania wakivuka boda wananganganiwa kwa sababu ya uwezo wao
 
Wamefanyiwa upasuaji(operation) katika hospitali moja nchini India ijulikanayo kama Apollo iliyopo mjini Hyderabad.
Prof Lipumba ana tatizo la figo na keshafanya upasuaji na alishindwa KUELEZEA hali yake kwakuwa dawa za usingizi
zilikuwa bado hazijaisha, akashindwa kuongea.
prof Mark Mwandosya anaumwa uti wa mgongo na kuna pingili moja ya mgongo imeoza, keshafanyiwa upasuaji na
yupo huko wiki ya pili sasa. Tatizo lilianza wakati yupo kwenye kikao cha bunge. Kapelekwa muhimbili lakini wapi.

Mungu awape baraka zake mpone haraka mje kutumikia taifa.

sosi: Gazeti(Mtanzania kama sio Tanzania Daima)

Hivi kwa mfano mimi nikiumwa magonjwa kama hayo...kuna chance za kwenda India? Anyway Mungu awajalie afya njema...
 
Kama Lipumba yuko India kwa operesheni
Kama Malecela alikuwa UK kwa operesheni

Hayati Nyerere alitibiwa na kufia UK
Hayati Diria alitibiwa na kufia Germany

Inamaana baada ya miaka 50 ya uhuru,tuna madokta/maprofesa feki hapo Muhimbili kama hata viongozi wetu hawawaamini.

Sasa Muhimbili wanatibu watu weak,poor na ni walala hoi.
Howa many botched operations ambazo hatujui?

Kaka, yaani unaamini na sie wengine ni watu kama wao? Siku zote kwa ishu ya matibabu huwa najihesabu kama panya wa majaribio tu. Kama unadhani na wewe katika watu umo kama wao, unaidanganya nafsi yako.
 
Aaaa,wataalam wa muhimbili,bugando na kwingnwko wa nini?????ndio maana watumishi wa afya,walimu na wataalam wengine hawalipwi ipasavyooooo......mzee malecela alienda UK now amepumzka USA,nyerere alienda UK,

- UK ilikuwa ni matibabu na US ni kwa watoto, jamani si hata mchwa huwa wanambeba kiongozi wao, I mean mengine ni fact of life wote hatuko sawa na hatukuzalwia sawa, na besides ni kila mahali duniani, au?

Willie @ NYC, USA.
 
Wamefanyiwa upasuaji(operation) katika hospitali moja nchini India ijulikanayo kama Apollo iliyopo mjini Hyderabad.
Prof Lipumba ana tatizo la figo na keshafanya upasuaji na alishindwa KUELEZEA hali yake kwakuwa dawa za usingizi
zilikuwa bado hazijaisha, akashindwa kuongea.
prof Mark Mwandosya anaumwa uti wa mgongo na kuna pingili moja ya mgongo imeoza, keshafanyiwa upasuaji na
yupo huko wiki ya pili sasa. Tatizo lilianza wakati yupo kwenye kikao cha bunge. Kapelekwa muhimbili lakini wapi.

Mungu awape baraka zake mpone haraka mje kutumikia taifa.

sosi: Gazeti(Mtanzania kama sio Tanzania Daima)
ALMIGHTY GOD awaponye mapema warudi kwenye kazi za kujenga taifa
 
Back
Top Bottom