Mwandosya na Lipumba wafanyiwa upasuaji India

nashindwa kusema pole kwa mwandosyamaana yeye ni mmoja wa watanzania walioifikisha haposector ya afya na huduma zakemasikini wengi wamekufa na magonjwa madogo madogo hali waowakilipwa maposho makubwa kama waziri kila nakokwenda analipwa milioni 1.2kama posho, hata kama amekwenda kwenye semina ya wizara yake lazima walipwesasa hiyo pesa wanayokwapu tungeweza kuwa na hospitali za maana kwa ajili ya watanzaniawote, yeye sasa yuko india hapa nyumbani watu wanaendelea kufa hali wao ndio sababisho.augue kwa kadri mungu apendavyo
Duuuh!! Kamanda una mihasira!
 
Tatizo kila kitu kimekuwa siasa, ulimwengu wote hauwezi kuwa sawa ndg. Kuna specialisation of labour. Mfalme wa Saudi Arabia juzi alikuwa matibabu New York, rais wa Venezuella kwa sasa yuko Cuba kwa matibabu. Sasa unashangaa nini wao kwenda India? Mungu atawaponya. Poleni sana
Na wasio na uwezo waende wapi?? hapo ndio point ilivyo!!
 
Mbona sie wanatuacha tunapoteza ndugu hapa tz!!
RIP ndo kilichobakia
Mungu awasaidie. Yeye (Mungu) haangallii kama wewe una pesa au la, baraka na bakora yake huwafikia wote.
nashindwa kusema pole kwa mwandosya
maana yeye ni mmoja wa watanzania walioifikisha hapo
sector ya afya na huduma zake

masikini wengi wamekufa na magonjwa madogo madogo hali wao
wakilipwa maposho makubwa kama waziri kila nakokwenda analipwa milioni 1.2
kama posho, hata kama amekwenda kwenye semina ya wizara yake lazima walipwe

sasa hiyo pesa wanayokwapu tungeweza kuwa na hospitali za maana kwa ajili ya watanzania
wote, yeye sasa yuko india hapa nyumbani watu wanaendelea kufa hali wao ndio sababisho.

augue kwa kadri mungu apendavyo
Si vizuri kumtakia binadamu mwenzako mabaya. Hakuna hakimu wa haki kama Mungu.
 
Huyu mbumbu gani anashindw kutofautisha kati ya mwandosya na mwakyusa kwa kumpakazia mwandosya kuwa aliongoza wizara ya afya vibaya?.......mijitu mingine bana!

tuwekane sawa: Allah atamsaia lipumba na mungu wa kweli atamsaidia mwandosya
 
nashindwa kusema pole kwa mwandosya
maana yeye ni mmoja wa watanzania walioifikisha hapo
sector ya afya na huduma zake

masikini wengi wamekufa na magonjwa madogo madogo hali wao
wakilipwa maposho makubwa kama waziri kila nakokwenda analipwa milioni 1.2
kama posho, hata kama amekwenda kwenye semina ya wizara yake lazima walipwe

sasa hiyo pesa wanayokwapu tungeweza kuwa na hospitali za maana kwa ajili ya watanzania
wote, yeye sasa yuko india hapa nyumbani watu wanaendelea kufa hali wao ndio sababisho.

augue kwa kadri mungu apendavyo
Ee bwana toa pole bila hiana.
Utajashangaa unakufa wewe au ndugu yako wa karibu kutokana na roho mbaya.
Kumbuka , hata adui yako muombee isije kupata balaa unayofikiria wewe haiwezi kukupata.
Wagonjwa viongozi poleni sana na wapone haraka.
 
Mungu atawapa Afya njema na Kurudi Nyumbani Kuwatumikia Wananchi, hili si lakufanyia Kejeli kwani Binaadamu hajamaliza Kuumbwa, leo wao kesho kwa Viongozi wengine wanaotajika.
 
*Wanatibiwa hospitali ya Apollo nchini India
*Wafanyiwa upasuaji wa figo, uti wa mgongo

Na Mwandishi Wetu

VIONGOZI wawili, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba; na Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, wanaumwa.

Wamelazwa katika Hospitali ya Apollo iliyopo katika mji wa Hyderabad, nchini India.

Profesa Lipumba alifika hospitalini hapo siku tano zilizopita kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

Kwenye uchunguzi huo, kwa mujibu wa watu walio karibu naye, ilibainika kuwa anasumbuliwa na maradhi ya figo.

Juzi, Profesa huyo wa uchumi alifanyiwa upasuaji. Alipoombwa azungumzie maendeleo ya afya yake, hakuwa tayari kufanya hivyo kwa maelezo kwamba bado alikuwa akikabiliwa na ‘ulevi' wa dawa.

Aliahidi kuzungumza leo au kesho kadri afya yake itakavyoruhusu. Baadhi ya watu walio karibu na mwanasiasa huyo walisema maendeleo yake kiafya yanaridhisha.
Kwa upande wake, Profesa Mwandosya amelazwa hospitalini hapo kwa zaidi ya wiki mbili sasa.

Imeelezwa kwamba waziri huyo aliugua ghafla wakati akishiriki Mkutano wa Bajeti mjini Dodoma. Alikodishiwa ndege kwa dharura na kupelekwa Muhimbili. Hata hivyo, hali yake iliendelea kuwa mbaya na kulazimika kupelekwa nchini India.
Watu walio karibu na Profesa Mwandosya walisema kwamba anasumbuliwa na maradhi ya uti wa mgongo.

"Mheshimiwa Waziri anasumbuliwa na uti wa mgongo, kuna pingili imelika," kilisema chanzo chetu.

Ilielezwa kwamba Waziri Mwandosya ilikuwa arejee nchini jana ili awahi kusoma bajeti ya wizara yake, lakini hali yake ilibadilika ghafla kabla hajaondoka.

Kubadilika kwa hali yake kuliwalazimu madaktari wamshauri aendelee na matibabu.
"Hali ilibadilika ghafla, ikalazimu apelekwe katika chumba cha x-rays, ana maumivu makali, lakini wananchi wasiwe na wasiwasi," kilisema chanzo chetu.

Watanzania wengi wamekuwa wakienda kutibiwa nchini India. Hatua hiyo inatokana na upungufu wa vifaa uliopo nchini. Serikali imekuwa ikijitahidi kuhakikisha vifaa na wataalamu wanapatikana ili kupunguza mzigo kwa Serikali wa kugharimia matibabu ya raia wake.

Tayari mipango madhubuti imeshakamilika kwa ajili ya kufanya upasuaji wa moyo na usafishaji figo hapa hapa nchini.


 
Kama Lipumba yuko India kwa operesheni
Kama Malecela alikuwa UK kwa operesheni

Hayati Nyerere alitibiwa na kufia UK
Hayati Diria alitibiwa na kufia Germany

Inamaana baada ya miaka 50 ya uhuru,tuna madokta/maprofesa feki hapo Muhimbili kama hata viongozi wetu hawawaamini.

Sasa Muhimbili wanatibu watu weak,poor na ni walala hoi.
Howa many botched operations ambazo hatujui?
 
Bila kumsahau Mwandosya naeo huko India.

Hata mtoto wa mkulima health check up zake ni UK!
 
Viongozi ni wamhimu sana kuliko mwananchi wa kawaida.Ndio maana hata gerezan kuna magereza yao ya VIP.Hata kura huwa tunawapigia na kuwaita WAHESHIMIWA
 
Kama Lipumba yuko India kwa operesheni
Kama Malecela alikuwa UK kwa operesheni

Hayati Nyerere alitibiwa na kufia UK
Hayati Diria alitibiwa na kufia Germany

Inamaana baada ya miaka 50 ya uhuru,tuna madokta/maprofesa feki hapo Muhimbili kama hata viongozi wetu hawawaamini.

Sasa Muhimbili wanatibu watu weak,poor na ni walala hoi.
Howa many botched operations ambazo hatujui?

Swali zuri ila sioni kama kuna majibu
Wapo wazuri sana na waliobobea katika fani ila kutokana na malipo duni na maisha ya ajabu wanayoishi wamejikuta wanafanya kazi chini ya kiwango
Serikali kama imewatelekeza na imetelekeza huduma na hata upatikanaji wa vifaa malumu kuendesha hospitali zetu ndo maana wao wakiugua wanaenda kutibiwa nje maana wanajua wakiingia mle hawatapata kile walicho nacho wenzetu
 
Tatizo na availability ya vitendea kazi. Watalamu wapo wengi sana. Serkali imeshindwa ku-equip hospitali zetu na vitendea kazi muhimu. Unaweza ukaenda nje kusomea jinsi ya kutengeneza ndege na ukafaulu with flying colours. Ukija bongo utakuwa useless sbb hamna vitendea kazi. Ilaumiwe serkali siyo wataalamu.
 
Back
Top Bottom