Mwandosya: Kulikoni? Arudi tena India, Dr Mwakyembe achungulia ofisi

Jamani, nani anajua anaendeleaje afya yake Professor Mark Mwandosya Mbunge wa Rungwe Mashariki? Kimya ni kingi mno na alisemewa mengi akiwa ndani ya matibabu. Nilisikia alifanyiwa maombi ya shukrani Kanisani kwake Rungwe kwa kurejea salama kutoka India lakini picha zilionyesha kavishwa POP. Anayejua anaendeleaje atujuvye. Tunmtakia kheri kabisa.
 
Nimesikia karudi India, bt sijui anaendleaje. Wish him apate afya nzuri n arudi 2lijenge taifa
 
Tatizo nao waoga sana! Wanashindwa nini kuweka hadharani yaliyowasibu?? Wataendelea kuumwa na kurudi India mpaka lini huku watanzania hatujui kipi kinawasumbua?
 
Nafikiri tunapowaza mabadiliko ya katiba tuwaze pia muundo wa utawala katika wizara zetu...Waziri,Naibu,Katibu Mkuu,Naibu Katibu mkuu....kwa kazi zipi? Hapo kila mmoja kwa mwezi anatumia hela nyingi sana za posho,mafuta,matibabu,mshahara,mawasiliano na mengineyo....na tuweke utaratibu wa watu kulazimishwa kujiuzulu na sheria pale anaposhindwa majukumu yake kwa muda fulani.

Michelle, mawazo yako ni mazuri. Hata hivyo, mazingira ya kuugua kwa hawa jamaa - yaani yale yaliyotokea na yaliyosemwa kabla hawajaugua - yananifanya niwaze mengi. Mojawapo ni hili: mtu ukijitoa ili kupiganie wengine, yatakapokupata yakukupata basi ujue utakuwa peke yako. Hasa kama wale unaowapigania ni wa-tz.
 
walio wachezea mchezo mbaya wapo busy kufanya maandalizi ya urais 2015 kwa kuzunguka sehemu mbalimbali kuchangia maendeleo baada ya kubaini kuwa wapinzani wao wapo hoi.
 
Waziri wa maji mh. Mark Mwandosya amerudi tena nchini india kulikoni, serikali mpaka leo ipo kimya juu ya ungonjwa wake tatizo liko wapi? na Dr. Mwakyembe nae hajaenda ofisini hadi leo japo alichungulia ofisi siku moja?

Source majira ya leo

Namwamini sana Mwakyembe lakini hili la Serikali kukalia ripoti ya ugonjwa wake hadi sasa na yeye yuko kimya tu sitamwelewa, hajui kuwa anatafutiwa timing wammalize ili ripoti waifiche? hata kama Mwakyembe hajipendi lakini awatendee basi haki Familia yake ambayo akifa ndiyo itakayoteseka, pia awahurumie na kuheshimu kura za wananchi waliomchagua awawakilishe bungeni maana akisubiri hadi wamuue itakuwa ana dhambi kubwa sana ambayo itakuja kuwatesa Watanzania, awe wazi maana taarifa ya kuwindwa kwake aliipeleka Polisi wakafanya kimya hawakuitendea kazi, leo hii tena yaleyale. Kweli nampenda Mwakyembe lakini anayoyafanya yatanifanya nimchukie maana mimi huwa siwapendi watu wasio majasiri.
 
Circa 1992......JK akiwa waziri na Prof akiwa katibu mkuu..guess where?...maji,madini na nishati....ndio mwaka mgao wa umeme ulianza rasmi

Mwandosya alikuwa Katibu Mkuu chini ya JK, Mwandosya alijiuzuru ukatibu mkuu kurudi kufundisha kwa sababu hakukubaliana na mpango wa kununua mitambo ya fulani, kwa taaluma yake mitambi ilikuwa haifai lakini bosi wake alitaka mpango uendelea,Mwandosya akaachia ngazi alikuwa hana njaa.

IPTL ilipitisha kipindi gani?
 
Circa 1992......JK akiwa waziri na Prof akiwa katibu mkuu..guess where?...maji,madini na nishati....ndio mwaka mgao wa umeme ulianza rasmi

Mwandosya alikuwa Katibu Mkuu chini ya JK, Mwandosya alijiuzuru ukatibu mkuu kurudi kufundisha kwa sababu hakukubaliana na mpango wa kununua mitambo ya fulani, kwa taaluma yake mitambo ilikuwa haifai lakini bosi wake alitaka mpango uendelea,Mwandosya akaachia ngazi alikuwa hana njaa.

IPTL ilipitisha kipindi gani?
 
Watu wafukunyuku kweli, afya za watu ni mambo binafsi mnataka watu waogope siasa nini
 
Back
Top Bottom