Mwandosya alifuata nini Butiama?

Picha ilipigwa 1992 Mwandosya akiwa Katibu Mkuu Wizara ya Biashara. Alikuwa ziarani Musoma akaona ni heshima kumsalimia Mwalimu. Wakati huo sidhani alikuwa na mawazo yakuwa mwanasiasa. Hivi watu wote waliyopiga picha na Nyerere au kumtembelea Butiama walikuwa na ndoto za kuwa maraisi??
 
Wote hao hawana mpango ,hivi hapo wangemulika pale nyuma yao si wangekaona kale katoto kamevaa kafulana ka mtumba na kakapu na miguuni hamna kiatu,Yaani kama wengempima hali ya mtoto yule na kuutumia utajiri huu ambao leo hii umepata wajanja naona tungekuwepo mbali sana.Kwa kweli inatia huruma sijui Waafrika tumekosa nini kwa Bwana Mungu.
Ila naona hao haijambo , ila kwa viongozi wetu wa leo wale watoto wa walala hoi pale nyume wangekwisha kuvamiwa na FFU na kupigwa na kugalagizwa kisha kuwekwa kwenye rova na kwenda kufunguliwa mashtaka.
 
Ama Mwalimu alikuwa fit sana au ni basi ukoo una miili midogo midogo. Maana mpaka anakufa, alinawiri kwa wastani sana.

Lakini angalia walimfuatia, hasa Mkapa na sasa Kikwete, wamenawiri kupita kiasi! Mkapa ndio kazidiwa kabisa na unono!
 
Ama Mwalimu alikuwa fit sana au ni basi ukoo una miili midogo midogo. Maana mpaka anakufa, alinawiri kwa wastani sana.

Lakini angalia walimfuatia, hasa Mkapa na sasa Kikwete, wamenawiri kupita kiasi! Mkapa ndio kazidiwa kabisa na unono!

Mwinyi naye yuko fiti.....
 
Ila jama kusema kweli Mwalimu alikuwa na personality kali sana, jinsi alivyokuwa kuwa tu unahisi kabisa kuwa yule ni mtu aliyekaa kiuongozi, ongozi. hata akiwa katika kundi la watu wengine, macho yanampin point kwamba " that must be their leader"... hii kitu ndo inaitwa Charisma au?
 
Kweli hapo NIDHAMU YA WOGA ILIKUWA WAZI!
Yani ni kama wako na MUNGU MTU!
Haswa haswa huyo mwenye suti nyeupe ya kijamaa!
Mwalimu alijitwisha mzigo wote wa kuliongoza Taifa na ndio maana baada ya kufa kwake linayumba!
Lakini mwishowe utakuwa mzuri kwani sasa ni wadau wote wa nchi watashirikishwa kwenye ujenzi wa TAIFA!
NB:Huyo aliyeko kulia kabisa ni MUSEVENI,CHEYO...Ama macho yangu?
Maana Kinana ni light skin zaidi!

Huyo unayemsema mwenye suti nyeupe ya kijamaa alikuwa mdogo wake na Mwl. Nyerere aliitwa Joseph Nyerere. Siamini kama alikuwa na nidhamu ya woga, sema Mzee mambo ya JKT yalikuwa akinili sana. Alikuwa hana sababu ya kuogopa chochote.
 
View attachment 1798

miaka kadhaa iliyopita Mwandosya alikwenda kumtembelea mwalimu Nyerere nyumbani kwake Butiama. Mwandosya alifuata nini kwa mwalimu?

Baada ya Mwalimu kustaafu, viongozi mbalimbali waliomuheshimu walikuwa wakienda ku-pay courtesy calls. Huenda hii ni moja ya safari za kiongozi huyo (Mwandosya) kwa ajili hiyo. Watatu ni nduguze Mwalimu - Joseph, Muhunda na Ihunyo. Waliosalia wanaweza wakawa wasindikizaji na viongozi wa Mkoa wakati huo. Na mazungumzo kwa kawaida yalikuwa ya kawaida tu na wakati mwingine kucheza bao na Mwalimu kwa wale ambao walipenda kukaa muda mrefu ama walialikwa kula chakula na Mwalimu.

Kuhusu suala la wasaidizi kushindwa kumwangalia Mwalimu usoni kama si kumsingizia Mzee Lusinde kwamba alitamka hivyo, basi ni uchekeshaji tu wa Mzee Lusinde maana ni mtu mcheshi sana. Mwalimu hakutoa mwanya wa wasaidizi wake kumuogopa! Kama aliogopwa na viongozi basi ni kutokana na msimamo wake wa kuwakemea bila kuwaonea haya viongozi waliodhihirisha kwamba hawafai.
 
..labda Mwandosya alikwenda kushtaki na kumueleza Mwalimu mambo yaliyomfika mpaka akahamishwa toka wizara ya nishati.

..Mwalimu alikuwa na mwili mzuri sana na nafikiri alikuwa mwangalifu na diet yake.

..Mkapa ana mwili wa kuumuka-umuka. nadhani hata akiwa na shida anaweza kunenepa zaidi.

NB:

..kuna kipindi Joseph Nyerere alikuwa naibu waziri.
 
Ni kama Mwalimu wanasema:

Mwalimu:Unaonekana una Busara sana na akili za kuchambua mambo,Embu Yule kijana ambaye alikuwa juu yako kama waziri unamuonaje anavyofanya kazi?

Mwandosya:hayuko serious,mambo anayofanya wakati mwingine huwa nashanga sana,Mwali wewe unamuonaje?

Mwalimu: Mie aliniambia ana ndoto ya kuwa kiongozi,nikamuulizi wa namna gani na wapi anataka kuongoza,akaniambi atakuja tuongee,ile nimesikia sikia ana rafiki mmoja na wana mipango na Urais.Rafiki yake ni bepari na sijui katoa wapi pesa alizonazo

Mwandosya: agh agh ha ha,

Mwalimu: Nimeshamaliza,kuweni makini na hawa watu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom