Mwandishi wa habari jamboleo chupuchupu baada ya kumpongeza polisi aliemfetulia risasi raia

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Ni baada ya Polisi mmoja kumjeruhi mwanafunzi wa kidato cha 3 wa shule moja ya Morogoro kwa kumpiga risasi mguuni siku ya maandamano ya kupinga wanafunzi wa Ndanda , Mwandishi wa jamboleo aliekuwepo mita chache ya tukio katika barabara ya kuelekea Kwa mkuu wa mkoa alisikika kwa sauti kubwa kwa kusema"SAWA SAWA POLISI" kiliwafanya wanafunzi waliokuwa karibu na mwandishi huyo kuanza kupiga kelele za kulalamikia kitendo hicho cha kupongeza,baadae kundi kubwa la vijana waliokuwa wakinadamana waliingia hamasa za kutaka kumdhuru kwa kumvamia na kupiga

Ghafla kundi jengine la waandishi wa habari walaicha kazi yao na kuanza Kumnusuru mwandishi huyo kwakuchukua hatua za ziada za kuwasihi wanafunzi kutomdhuru na kumuondosha ktk tukio.

Kazi iliofanywa na waandishi wa Startv, Channel 10 ,TBC na wapiga picha wengine waliokuwepo katika tukio na jitihada binafsi za Jaffar Mponda wa Redio Imani na TV ziliweza kuzuia kupigwa kwa mwandishi huyo.

JEE KAZI YA MWANDISHI KATIKA MATUKIO KAMA HAYA KUMBE NI KUPONGEZA POLISI?BADALA YA KURIPOTI HABARI?
NINI TUTEGEMEE KWA VYOMBO VYETU VYA HABARI VILIVYOKUWA SIO VYA SEREKALI?

JEE KITENDO HICHI HAKIWEZI KUVURUGA AMANI NA UTULIVU KATI YA WAKIRISTO NA WAISLAM?

JEE JAMBOLEO INAWEZA KUJIVUNIA NINI KWA JAMII?
 
ndio maana leo jamboleo habari yao ya maandamano wameiopotosha? duh hili gazeti nilikuwa nalipenda sana. kumbe ni hatari kwa jamii
 
Hata mimi nimesikia hii ikizungumziwa kwa ukubwa zaidi hapo Redio imani leo. kwa bahati wao hawakutja gazeti. Jamboleo sasa litakuwa JAMBALEO tu
 
ni ngumu sana kwangu kuiamini habari hii kutokana na mazingira ya tukio, na vilevile kama ni kweli ni vigumu pia kujua huyo mwandishi ni wa imani gani i.e kama ni muislam,mkristo,mpagani etc.
 
hili ntukio ni la kweli. kazi ya ziada iliofanywa na waandishi wenziwe wa habari imesaidia sana.kama huamini jaribu kuwauliza waliokuwepo ktk tukio hasa wale wa Startv.
 
ni ngumu sana kwangu kuiamini habari hii kutokana na mazingira ya tukio, na vilevile kama ni kweli ni vigumu pia kujua huyo mwandishi ni wa imani gani i.e kama ni muislam,mkristo,mpagani etc.
imani sijui imani gani. lkn tukio hili limetia aibu sana tasnia ya habari. inatakiwa baraza la habari lilaani kitendo hichi
 
Huyu mwandishi anataka kuliharibia gazeti tu na hana nia nyengine. siamini kama jamboleo kuna udini kama huo
 
Kwa alilofanya alistahiki kupigwa na kuanzia sasa ameshatangaza vita na jamii yote akae chonjo.
 
Ni baada ya Polisi mmoja kumjeruhi mwanafunzi wa kidato cha 3 wa shule moja ya Morogoro kwa kumpiga risasi mguuni siku ya maandamano ya kupinga wanafunzi wa Ndanda , Mwandishi wa jamboleo aliekuwepo mita chache ya tukio katika barabara ya kuelekea Kwa mkuu wa mkoa alisikika kwa sauti kubwa kwa kusema"SAWA SAWA POLISI" kiliwafanya wanafunzi waliokuwa karibu na mwandishi huyo kuanza kupiga kelele za kulalamikia kitendo hicho cha kupongeza,baadae kundi kubwa la vijana waliokuwa wakinadamana waliingia hamasa za kutaka kumdhuru kwa kumvamia na kupiga
Ghafla kundi jengine la waandishi wa habari walaicha kazi yao na kuanza Kumnusuru mwandishi huyo kwakuchukua hatua za ziada za kuwasihi wanafunzi kutomdhuru na kumuondosha ktk tukio.
Kazi iliofanywa na waandishi wa Startv, Channel 10 ,TBC na wapiga picha wengine waliokuwepo katika tukio na jitihada binafsi za Jaffar Mponda wa Redio Imani na TV ziliweza kuzuia kupigwa kwa mwandishi huyo.
JEE KAZI YA MWANDISHI KATIKA MATUKIO KAMA HAYA KUMBE NI KUPONGEZA POLISI?BADALA YA KURIPOTI HABARI?
NINI TUTEGEMEE KWA VYOMBO VYETU VYA HABARI VILIVYOKUWA SIO VYA SEREKALI?
JEE KITENDO HICHI HAKIWEZI KUVURUGA AMANI NA UTULIVU KATI YA WAKIRISTO NA WAISLAM?
JEE JAMBOLEO INAWEZA KUJIVUNIA NINI KWA JAMII?

inategemea na tukio. mengine ndiyo na mengine hapana.
 
Back
Top Bottom