Mwandishi wa Gazeti la Majira ajiapiza ailaani CHADEMA

Tatizo la CHADEMA ni kwamba wakiambiwa ukweli huwa hawataki wao ni ubidshi tu. Kusema kweli kwa suala la mkuu wa wilaya hapa CDM wameboronga. Imenikumbusha bango moja lililosema "Vurugu zenu pelekeni huko Arusha." CHADEMA ni vema mkapgania haki lakini siyo kueneza vurugu zisizo na tija.
 
CHADEMA kwa hili mmechemka

Na Gladness Mboma

ALHAMISI ya wiki iliyopita wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walimkamata Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario kwa
madai kuwa walimkuta akifanya kikao na viongozi wa vijiji na kata ndani ya ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Isakamaliwa.

Kwanza kabisa kwa mtazamo wangu CHADEMA walichofanya ni makosa lisha ya kwamba walimdhalilisha kiongozi wa wananchi kwa kumvuta huku na huko huku wakitambua wazi kwamba kufanya hivyo ni kosa la jinai.

Kosa ambalo ama hakika bila ushabiki wowote wahusika wote wanapaswa kushtakiwa na kuchukuliwa hatua za kisheria haraka iwezekanavyo.

Ni hoji kwanza, hivi hawa wahuni wanaojiita makomandoo wa CHADEMA wameenda Igunga kwa misingi ya kumnadi mgombea wao ama kumdhalilisha kiongozi aliyewekwa madarakani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Awali nilikuwa ninawakubali CHADEMA kutokana na sera zao za kuleta maendeleo lakini kwa uhuni huu uliofanywa na wanachama hao Igunga katu siwezi kusita kutamka kwamba wakipata nafasi ya kutawala nchi hii awachelewi kuwanyanyasa Watanzania kijinsia.

Tuzingatie kwamba, Bi. Kimario ni kiongozi wa nchi hawakustahili kumdhalilisha kiasi hicho, tena kibaya zaidi wanaume ndio waliohusika kumvuta mama huyo huku na huko kama mwizi.

Haiwezekani hizi ni vurugu ambazo zinatakiwa kupigwa vita na kukemewa kwa nguvu zote ina maana kiongozi ana mipaka ya kufanya mikutano?

Huyu ni kiongozi ana haki ya kufanya kikao mahali popote muda wowote na wananchi wake bila kubuguziwa ili mradi asivunje sheria.

Ina maana wakati huu kampeni za uchaguzi mdogo unaoendelea Igunga kiongozi yoyote wa serikali hatakiwa kufanya kikao na wananchi wake kwa kuhofia kuwa anapanga njama za ushindi wa chama fulani.

CHADEMA sasa mnakoelekea ni kubaya mlikuwa mnakwenda vizuri sasa vurugu zenu na ubabe wenu ndio utakaowakosesha kura na wala si vinginevyo.

Kwani mkifanya siasa na kampeni za ustaarabu hamtaonekana ndani ya jamii ama hadi kila siku muwe na jambo jipya linaloonesha udhalilishaji kwa ili nidhiriki kutamka kwamba wapumbavu siku zote huwa wanajitwalia makaa ya moto wenyewe hivyo siwafichi kwa stahili hii mnajiangusha wenyewe na mnajiua wenyewe.

Vurugu hazipendezi hata kidogo, huyu Mkuu wa Wilaya ana haki ya kufanya mkutano au kikao na viongozi wake kwa sababu kwa ni haki yake ya msingi ili kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Katika suala hili hakuna ubishi ni lazima mchukuliwe hatua, watu waliomkamata na kumdhalilisha ni lazima sheria ichukue mkondo wake huu ni ukosefu wa nidhamu.

Hii ni hatari kwa maana hiyo kiongozi yoyote wa serikali wa Wilaya ya Igunga asifanye chochote kwa kuhofia vyama vya upinzani, jamani tuacha mawazo mgando huu ni uhuni kama siyo ujinga katika vichwa vya watu walioelimika.

Hata kama huyo mama alikwenda kinyume, lakini hakustahili kufanyiwa kitendo hicho hata kidogo ni udhalilishaji.
Acha comments za "kitumwa" ni nani raia mwenye haki kuliko mwenzake tz? wale waliopigwa risasi kama nguruwe pori huko arusha, tarime na kwinginepo walikuwa raia nusu au robo!??. wale wawakilishi wa wananchi waliopigwa kama majambazi Arusha walikuwa raia robo?! kwako wewe mteuliwa wa Rais ndiye raia zaidi ya wengine. I HATE YOUR THINKING!!! THIS IS PURE SLAVERY!
 
Mwandishi kazungumza ukweli kabisa.Kama uko mpinzan ukikosea nawe ukubali kukosolewa.Watz hawapaswi kusamehe upuuzi wa CDM wa kujichukulia sheria mkononi hasa vijana wa kiume kumshambulia na kumkamata mama wa kike.Chama cha siasa tangu lini kikawa na makamanda?,hapo mwandishi ndio anasema CDM mnakoelekea ni kubaya.Kumvua mama hijabu mmedhihirisha kuwa padre anachuki na uislam na waislam hatutawasamehe kamwe labda mtuombe radhi.
Mkuu unauliza chama kuwa na makamanda? waulize magamba wenzio wale makamanda wenu siku hizi mmewapa jina lingine?
 
Mwandishi kazungumza ukweli kabisa.Kama uko mpinzan ukikosea nawe ukubali kukosolewa.Watz hawapaswi kusamehe upuuzi wa CDM wa kujichukulia sheria mkononi hasa vijana wa kiume kumshambulia na kumkamata mama wa kike.Chama cha siasa tangu lini kikawa na makamanda?,hapo mwandishi ndio anasema CDM mnakoelekea ni kubaya.Kumvua mama hijabu mmedhihirisha kuwa padre anachuki na uislam na waislam hatutawasamehe kamwe labda mtuombe radhi.

Wewe na huyo mwandishi mna akili fupi sana. Mtu ambaye ni great thinker anangalia pande zote mbili na kusimama katikati lakini ukilalia upande mmoja na kuunyonga mwingine huna tofauti na kipofu. Kwani mbunge wa CUF alifanywaje na polisi na kukaa rumande kwa siku 9 kisa kaenda kusikiliza matatizo ya wananchi huko Urambo. Tatizo serikali na CCM wanahhaha kuficha aibu na polisi wanafanya kazi kwa maagizo ya CCM na serikali yao legelege.

Fikiria kwanini mbunge wa CCM aliyetuhumiwa kwa mauaji polisi waliogopa kumhoji mpaka waombe ruhusa kwa Spika hata baada ya rhusa kutolewa mpaka leo hajahojiwa kwa kukingiwa kifua na DCI Manumba. Kabla ya kuandika muwe mnafikiria mambo mengi na kuwa na uelewa na fikira pana zaidi. Hivi ndivyo great thinker anavyopaswa kubehave
 
Tatizo la CHADEMA ni kwamba wakiambiwa ukweli huwa hawataki wao ni ubidshi tu. Kusema kweli kwa suala la mkuu wa wilaya hapa CDM wameboronga. Imenikumbusha bango moja lililosema "Vurugu zenu pelekeni huko Arusha." CHADEMA ni vema mkapgania haki lakini siyo kueneza vurugu zisizo na tija.

Ukweli upi ndugu wa kulalia upande mmoja tu, ukweli unakuwa na kusema makosa ya kila upande sio kusema kwamba fulani tu ndo kakosea mbona kabla ya maagizo kutoka juu polisi waliwaachia wabunge wa Chadema? Kwa sababu waliona hata DC alikuwa kachemka kwenye hiyo move. Baada ya maagizo kutoka juu ndiyo DC akaanza kusema uongo oo walitaka kunibaka, ooo niliibiwa mkufu wakati kwenye picha anaonekana kauvaa, oo simu ili mradi tu ionekane kakosewa yeye tu.

Na hizo barua za wasimamizi wa uchaguzi alikuwa anazipeleka wapi? kwani hiyo ni kazi yake kama DC? Nafikiri yapo mambo mengi ya kuhoji upande wa DC na alichokuwa akifanya na wazee wa CCM na wajumbe wa nyumba 10 kuliko unavyofikiri ndugu. Sio lazima yule anayekwenda kinyume na DC au serikali basi ni Chadema wengine haturidhishwi na nchi yetu inavyoendeshwa. Tukubaliane kwamba kama tungekuwa na maDC na maRC ambao ni impartial nina uhakika hata kwa tume ya uchaguzi tuliyo nayo matukio kama haya yangeweza kuepukwa kabisa, lakini kwa maDC na maRC makada wa magamba nchi itatumbukia kwenye hali mbaya huko tuendako.

Tumwombe Mungu atupe kiongozi na si watawala wabinafsi na mbumbumbu kama tilio nao sasa, pia atuepushe na mabaya yote yanayoweza kusababishwa na wajinga wachache wanaoitwa viongozi walioshindwa kuongoza
 
Ni maoni ya mtu binafsi ama yanayokera au kufurahisha (kulingana na mtazamo/itikadi wa/ya msomaji). Mwanzoni nilipoona headline ya thread hii nilidhani haya maoni yako kwenye Editorial (Tahariri), nilipoifungua nikakuta ni maoni ya mwandishi binafsi na jina lake ameweka, na wala hii siyo habari (news Story) ni maoni tu, hivyo ingekuwa vizuri maoni haya yakachambuliwa kama yalivyo, na kama kuna mwenye maoni tofauti akaandika kuyajibu hapa au kwenye gazeti husika. Nadhani hakuna mhariri takayekataa kuchapisha majibu hayo. Na huu ndiyo utaratibu mzuri wa kujadili hoja badala ya kuunganisha kila kitu na kukitupa kwa mhariri na gazeti lake. Tukumbuke kuwa haiwezekani, mhariri akakaa kwenye dawati lake kama Katibu Mwenezi wa Chama, nikimaanisha kuwa akakaa pale kuzuia maoni ya watu wote yanayokwenda kinyume na chama chochote au anachopenda yeye, labda hii inawekana kwenye magazeti ya vyama vyenyewe, kulingana na sera zao za kutetea wamiliki wake.
 
Wewe na huyo mwandishi mna akili fupi sana. Mtu ambaye ni great thinker anangalia pande zote mbili na kusimama katikati lakini ukilalia upande mmoja na kuunyonga mwingine huna tofauti na kipofu. Kwani mbunge wa CUF alifanywaje na polisi na kukaa rumande kwa siku 9 kisa kaenda kusikiliza matatizo ya wananchi huko Urambo. Tatizo serikali na CCM wanahhaha kuficha aibu na polisi wanafanya kazi kwa maagizo ya CCM na serikali yao legelege.

Fikiria kwanini mbunge wa CCM aliyetuhumiwa kwa mauaji polisi waliogopa kumhoji mpaka waombe ruhusa kwa Spika hata baada ya rhusa kutolewa mpaka leo hajahojiwa kwa kukingiwa kifua na DCI Manumba. Kabla ya kuandika muwe mnafikiria mambo mengi na kuwa na uelewa na fikira pana zaidi. Hivi ndivyo great thinker anavyopaswa kubehave

Nakubaliana nawe mkuu.Huyu mwandishi namjua vizuri sana.Kimsingi gazeti la majira kwa sasa halina mhariri wala waandishi.Waandishi wake wengi ninaowajua wamemaliza cheti pale Ilala sharifu shamba,hawawezi kuandika story au makala kwa maana ya kukuconvice kwa facts za kufikirisha.Kwa ujumla gazeti limepoteza mwelekeo sana kwa sababu ya aina ya waandishi hawa.

Kwa uwezo wa aikli za huyu dada na njaa aliyonayo,sijashangaa sana kuiona hii habari.Narudia tena kuwa namjua vizuri tu huyu mwandishi kwa hiyo Great thinkers msitumie nguvu nyingi sana kumjadili kwani ninahakika hatawaelewa.
 
Ukweli upi ndugu wa kulalia upande mmoja tu, ukweli unakuwa na kusema makosa ya kila upande sio kusema kwamba fulani tu ndo kakosea mbona kabla ya maagizo kutoka juu polisi waliwaachia wabunge wa Chadema? Kwa sababu waliona hata DC alikuwa kachemka kwenye hiyo move. Baada ya maagizo kutoka juu ndiyo DC akaanza kusema uongo oo walitaka kunibaka, ooo niliibiwa mkufu wakati kwenye picha anaonekana kauvaa, oo simu ili mradi tu ionekane kakosewa yeye tu.

Na hizo barua za wasimamizi wa uchaguzi alikuwa anazipeleka wapi? kwani hiyo ni kazi yake kama DC? Nafikiri yapo mambo mengi ya kuhoji upande wa DC na alichokuwa akifanya na wazee wa CCM na wajumbe wa nyumba 10 kuliko unavyofikiri ndugu. Sio lazima yule anayekwenda kinyume na DC au serikali basi ni Chadema wengine haturidhishwi na nchi yetu inavyoendeshwa. Tukubaliane kwamba kama tungekuwa na maDC na maRC ambao ni impartial nina uhakika hata kwa tume ya uchaguzi tuliyo nayo matukio kama haya yangeweza kuepukwa kabisa, lakini kwa maDC na maRC makada wa magamba nchi itatumbukia kwenye hali mbaya huko tuendako.

Tumwombe Mungu atupe kiongozi na si watawala wabinafsi na mbumbumbu kama tilio nao sasa, pia atuepushe na mabaya yote yanayoweza kusababishwa na wajinga wachache wanaoitwa viongozi walioshindwa kuongoza

Mkuu kumbe polisi wako impartial kwa maana hiyo ingekuwa vema kama CHADEMA wangewataarifu Polisi ili wachukue hatua. Nchi haiwezi kuendeshwa kwa kutumia mabaunsa. Nadhani unakumbuka yaliyotokea Chasimba baada ya mabaunsa kuvamia na kutaka kuvunja nyumba za watu. Mimi binafsi sikubaliani na hatua ya CHADEMA kumdhalilisha mkuu wa wilaya tena Mwanamke. La kushangaza ni kwamba Ananilea Nkya naye yupo kimya!!
 
Hivi hili gazeti mhariri wake ana taaluma? Yaani mwanindishi anatoa hisia zake binafsi yeye kama yeyena Mhariri anapitisha? Jazba zote za nini? Lets us stick on proffesionalism.
 
CHADEMA kwa hili mmechemka

Hii ni hatari kwa maana hiyo kiongozi yoyote wa serikali wa Wilaya ya Igunga asifanye chochote kwa kuhofia vyama vya upinzani, jamani tuacha mawazo mgando huu ni uhuni kama siyo ujinga katika vichwa vya watu walioelimika.

Hata kama huyo mama alikwenda kinyume, lakini hakustahili kufanyiwa kitendo hicho hata kidogo ni udhalilishaji.

Wakati nasoma hii makala nilijiaminisha kuwa mwandishi wake alikuwa hajui taratibu za nchi na haki sa kisiasa za vyama vya siasa, kutokana na alivyotetea kuwa mkuu wa wilaya alikuwa na haki ya kufanya 'mkutano ule'.

Lakini hapa mwisho amenishangaza alipomalizia na maneno 'hata kama huyo mama alikwenda kinyume'... Maneno haya yameonyesha dhahiri kuwa mwandishi alikuwa na kitu akilini mwake kuhusiana na uhalali wa alichokifanya mkuu wa wilaya. Hata hivyo, kwa sababu pengine za kishabiki, au chuki binafsi, mwandishi aliamua kujifanya limbukeni na kuishambukia CDM moja kwa moja na kumtetea mkuu wa wilaya, kabla ya kuufunua kidogo upumbavu wake mwishoni kwa kuonyesha alijua anachokiandika sio sahihi.

To me... just a simple crap...
 
mhari amechemka wakuu,kama unataka kutoa judgement kuhusu pande mdili jadili upande wa kwanza na wapili then fanya ufananisho badae angalia chanzo n nani ndo ulaum,laana ya kuku haimpati mwewe.nenda google soma rockingbird project ya CIA ILI MJUE WA HARIRI MNAVO TUMIKA KWENYE MAMBO YA UKWELI KWA JAMII
 
Mwandishi kazungumza ukweli kabisa.Kama uko mpinzan ukikosea nawe ukubali kukosolewa.Watz hawapaswi kusamehe upuuzi wa CDM wa kujichukulia sheria mkononi hasa vijana wa kiume kumshambulia na kumkamata mama wa kike.Chama cha siasa tangu lini kikawa na makamanda?,hapo mwandishi ndio anasema CDM mnakoelekea ni kubaya.Kumvua mama hijabu mmedhihirisha kuwa padre anachuki na uislam na waislam hatutawasamehe kamwe labda mtuombe radhi.

naona unataka kulipa hili swala sura mpya pale unapoingiza swala la udini,kama makamanda ata ccm wapo tatizo la ccm ni mnataka kufanya mambo nyie wakifanya wengine mnakuja juu kama moto wa kifuu,mara ngapi mmekua mkiwakamata na kuwadharirisha wabunge wa upinzani na mnaona sawa sasa dc kukamatwa tu imekua tabu.acheni hizo achieni jimbo mjipange upya
 
Tatizo la CHADEMA ni kwamba wakiambiwa ukweli huwa hawataki wao ni ubidshi tu. Kusema kweli kwa suala la mkuu wa wilaya hapa CDM wameboronga. Imenikumbusha bango moja lililosema "Vurugu zenu pelekeni huko Arusha." CHADEMA ni vema mkapgania haki lakini siyo kueneza vurugu zisizo na tija.

Another simple crap...
 
Mwandishi kazungumza ukweli kabisa.Kama uko mpinzan ukikosea nawe ukubali kukosolewa.Watz hawapaswi kusamehe upuuzi wa CDM wa kujichukulia sheria mkononi hasa vijana wa kiume kumshambulia na kumkamata mama wa kike.Chama cha siasa tangu lini kikawa na makamanda?,hapo mwandishi ndio anasema CDM mnakoelekea ni kubaya.Kumvua mama hijabu mmedhihirisha kuwa padre anachuki na uislam na waislam hatutawasamehe kamwe labda mtuombe radhi.
Tuondolee upuuzi wako hapa,mbunge wa CUF aliposachiwa na wanaume ilikua halali?Idiot we!!
 
Mwandishi kazungumza ukweli kabisa.Kama uko mpinzan ukikosea nawe ukubali kukosolewa.Watz hawapaswi kusamehe upuuzi wa CDM wa kujichukulia sheria mkononi hasa vijana wa kiume kumshambulia na kumkamata mama wa kike.Chama cha siasa tangu lini kikawa na makamanda?,hapo mwandishi ndio anasema CDM mnakoelekea ni kubaya.Kumvua mama hijabu mmedhihirisha kuwa padre anachuki na uislam na waislam hatutawasamehe kamwe labda mtuombe radhi.
<br />
<br />

Masaburi kakamata wengi sana. Udini unaingiaje hapa? Umesahau kikundi cha kigaidi cha ccm kinachoitwa "GREEN GUARD" kinachoendelea na mazoezi ya 'ukakamavu' kwa ajili ya uchaguzi wa Igunga?
 
ongelea hoja acha kuleta upuuzi wako hapa waislam hamtamsamehe nani?na unawakilisha waislam wangapi?
waislamu wote wameshagundua ccm ndiye adui wa uislam kupitia bakwata wewe na umbumbumbu wako unakuja na mambo ya kichochezi hapa.kila mtu najua cdm kwa namna moja au nyingine wamefanya kosa kama ambavyo polisi wanafanya makos,ccm anafanya makosa,serikali inafanya makosa,wananchi wanafanya makosa ni mfumo mbaya ulioasisiwa na ccm kila mpenda amani anatakiwa kulaani.
mbunge wa cuf alipekuliwa na askari wa kiume ni kosa,dc kakamatwa na vijana wa cdm ni kosa.sasaewe unakuja na ushabiki wako uliopitwa na wakati wa kidini sisi tunataka kila mtu katika nchi hii awe chini ya sheria.

Umenifurahisha sana kwa maneno yako,umeandika vzr kuliko huyo mhariri na upuuuzi mtupu.
 
Mkuu kumbe polisi wako impartial kwa maana hiyo ingekuwa vema kama CHADEMA wangewataarifu Polisi ili wachukue hatua. Nchi haiwezi kuendeshwa kwa kutumia mabaunsa. Nadhani unakumbuka yaliyotokea Chasimba baada ya mabaunsa kuvamia na kutaka kuvunja nyumba za watu. Mimi binafsi sikubaliani na hatua ya CHADEMA kumdhalilisha mkuu wa wilaya tena Mwanamke. La kushangaza ni kwamba Ananilea Nkya naye yupo kimya!!

Ningependa kusikia kauli ya TAMWA juu ya hili jambo.
 
Back
Top Bottom