Mwandishi Dennis Msaki ajiuzulu "Nipashe"

Status
Not open for further replies.
Hata mimi nimeongea naye sasa hivi, hajawahi kuwaza sala hatohamia Mtanzania. Kwa kauli yake mwenyewe amesema, "siwezi mimi kuhamia gazeti la watuhumiwa wa ufisadi, nina hadhi yangu siwezi kuiharibu, watu wasubiri watasikia nini kitafuata."

Amesikitishwa sana na taarifa za yeye kuhamia Mtanzania na anasema kauli yake hiyo ni kamili na hatoweza kula matapishi yake. "Hata baadaye, sitokula matapishi yangu."

Kuhusu suala la siri za IPP, naamini hakuna mwandishi wa habari makini anaweza kuzungumza jambo lolote linalohusu mwajiri wake wa sasa ama wa zamani, huo ni UMALAYA (naomba radhi kutumia neno kali) ambao watu makini hata hao utakaowapa hizo siri watakudharau na hawatakuamini tena maana iko siku utatoa siri zao kama ulivyowapa za mwenzao. Lakini pia, waandishi wa habari si wafanyabiashara na hivyo hawana nafasi ya kujua siri za mwajiri wao na mara nyingi huwa mbali sana na hizo zinazoitwa SIRI.

Mwisho, Denis Msaki ni mtu makini sana na hata alipotajwa kuwa na mahusiano na watu fulani, uhusiano wake haukuathiri hata chembe utendaji kazi zake za kila siku, aliendelea kuwa makini hadi leo nilipozungumza naye. Alitenganisha mahusiano binafsi na yale ya kikazi na marafiki zake walimheshimu kwa hilo. Kama atabadilika, huo ni UBINADAMU na tutajadili.

Wanandugu Nimeongea na Denis Msacky ana kiri kuacha Nipashe lakini AMEKANUSHA kujiunga na Habari Coopeartion!Amenieleza amemua kuacha kazi kwa hiari yake mwenyewe bila kishawishi cha mtu yeyoyote!

sasa haya ndio mambo tunayoyataka JF.....yaani safi kweri kweri....kama ni kweli katamka msacky
 
Kaazi Kweli kweli.

Yoyo unakubali kuajiriwa na RA kweli??? hehehehe
 
Wakuu,

kwa wenye data naomba taarifa, hivi suala la malipo kwa wafanyakazi kwenye kampuni za Mengi likoje? Je yeye analipa tofauti ukilinganisha na waajiri wengine wakubwa?

Ningetaka kujua hasa kwa wale wafanyakazi wa ngazi za chini, kwa mfano kwenye viwanda vyake.

Kuna neno linajirudia mara nyingi kwamba hawalipi wafanyakazi vizuri, ni vizuri tukapata data kama kuna ukweli au ni vita tu vya Mapapa na Manyangumi.

Itakuwa vizuri kupata data toka kwa wale wanaofanya kazi huko au wenye habari sahihi.

Mkuu Mtanzania, umenena kwa umakini mkubwa kama kawaida yako. SI vyema kuzungumza bila data ama hata ushahidi wa mazingira. Lakini hapa utakapozungumzia maslahi katika vyombo vya habari ama kampuni, ni vyema ukaangalia mhusika ana kampuni ngapi na kama anakuwa na direct link na kazi za kila siku. Mfano ni Mengi ama Rostam. Pamoja na matatizo yao, watu hawa wana watendaji wanaoshughulika na kampuni zao na hivyo ni mara chache sana maslahi ya watumishi wao yakahusishwa nao. Inatokea tu kwa mfano mtu maalumu (mhariri/mwandishi/mtumishi) ambao wamechukuliwa moja kwa moja kwa makubaliano na mwajiri, lakini wengineo wanawajibika ama kufanya kazi kutokana wakuu wa maeneo yao ya kazi.

Mara nyingi udhaifu wa wakuu wa maeneo yao, mfano Habari Corpo (wakati wa Bobi) ama IPP Media (waliopunguzwa) husababisha matatizo kwa wafanyakazi na wamiliki huwa waoga kuwaingilia mara kwa mara na hadharani watendaji wao na wanapoingilia huwa too late.

Kwa ufupi labda kama kuna special case, wafanyabiashara wakubwa hawapendi sana kuwaingilia waliowakabidhi management, na wakifanya hivyo hufanya siri sana kuepuka kuharibu utendaji wao kwa kuwa hawana muda wa kufuatilia kila kampuni kwa wakati wote.
 
Mimi naamini hilo bado sio pigo kubwa kwa familia ya The Guardian, fisadi papa akidhamiria kuleta pigo kubwa, anaweza kupiga pigo kuu takatifu mpaka fisadi nyangumi akayumba.

Kuondoka kwa mtu mmoja, issue ndogo tuu za marekebisho ya rasilimali watu, likiondoka kundi ndipo unaweza sema pigo kubwa.
Mbona walishakuwepo watu kibao wa maana, wameondoka na IPP media inaendelea, atakuwa huyo mmoja?!.
 
Habari zaidi zinaeleza kwamba Msaky yumo katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa MwanaHalisi, Saed Kubenea, mazungumzo yanayotarajiwa kuhitimishwa leo usiku, katika hoteli moja iliyopo maeneo ya Mwenge, Dar es Salaam.
 
akienda huko poa, maana ataendeleza mapambano dhidi ya ufisadi, lakini Kubenea awe makini.
 
Mkuu Halisi,

Asante sana kwa Data. Ila mimi niseme mawazo yangu, baada ya kulisoma Mwanahalisi kwa muda sioni kama ni gazeti makini kama nilivyokuwa nalidhania huko nyuma. Kunakuwa na mambo mengi sana ya kupikwa kuliko ukweli.

Nayaheshimu Thisday na Kulikoni kama magazeti imara na ambayo wakiamua kuandika habari basi wanakuja na data ambazo zinasimama kwa nguvu zake zenyewe.

Kwa mwandishi wa Nipashe kuhamia Mwanahalisi itakuwa sawa maana atatoka gazeti moja ambalo data sio muhimu sana na kwenda lingine karibu sawa na hilo.

Magazeti yetu mengi yanahitaji mabadiliko makubwa hasa kwenye suala la kuandika mambo ambayo yanajengwa na data nyuma yake.

Gazeti lingine ambalo lilikuja kwa nguvu lakini kwa mimi limeni dissapoint ni Raia Mwema. Jamaa wanakuja kuchota hapa JF kisha ndio data zao kwenye magazeti husika.

Kwa magezeti ya Watanzania ningelikuwa na tuzo basi ningewakabidhi Thisday na Kulikoni.

Siko kumshambulia mtu hapa lakini hayo ndio maoni yangu baada ya kuyasoma karibu magazeti yote ya TZ.

Habari zaidi zinaeleza kwamba Msaky yumo katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa MwanaHalisi, Saed Kubenea, mazungumzo yanayotarajiwa kuhitimishwa leo usiku, katika hoteli moja iliyopo maeneo ya Mwenge, Dar es Salaam.
 
Nipashe linaendeshwa kibiashara na sio kisiasa...

Mwisho, Denis Msaki ni mtu makini sana na... na marafiki zake walimheshimu... kwa hilo.

NIPASHE is among the most putrid of tabloids, na Msaki sio makini hata kidogo.

Juzi tu hapa kachapisha mashudu kwamba Pinda kasema serikali itagawa ardhi kwa wawekezaji "bila kujali kelele za wananchi." Mwongo mkubwa. Good riddance, labda NIPASHE sasa litapunguza mipasho.
 
Mkuu Halisi,

Asante sana kwa Data. Ila mimi niseme mawazo yangu, baada ya kulisoma Mwanahalisi kwa muda sioni kama ni gazeti makini kama nilivyokuwa nalidhania huko nyuma. Kunakuwa na mambo mengi sana ya kupikwa kuliko ukweli.

Nayaheshimu Thisday na Kulikoni kama magazeti imara na ambayo wakiamua kuandika habari basi wanakuja na data ambazo zinasimama kwa nguvu zake zenyewe.

Kwa mwandishi wa Nipashe kuhamia Mwanahalisi itakuwa sawa maana atatoka gazeti moja ambalo data sio muhimu sana na kwenda lingine karibu sawa na hilo.

Magazeti yetu mengi yanahitaji mabadiliko makubwa hasa kwenye suala la kuandika mambo ambayo yanajengwa na data nyuma yake.

Gazeti lingine ambalo lilikuja kwa nguvu lakini kwa mimi limeni dissapoint ni Raia Mwema. Jamaa wanakuja kuchota hapa JF kisha ndio data zao kwenye magazeti husika.

Kwa magezeti ya Watanzania ningelikuwa na tuzo basi ningewakabidhi Thisday na Kulikoni.

Siko kumshambulia mtu hapa lakini hayo ndio maoni yangu baada ya kuyasoma karibu magazeti yote ya TZ.

Mkuu Mtanzania kwa mara nyingine nakuaminia katika hili. Kwa bahati umegusa magazeti yote uliyoyataja ninajua undani wake kwa hiyo nikizungumza kwa umakini kidogo.

Ni kweli kabisa MwanaHalisi si makini, lakini ni MUHIMU katika mchakato wa mapambano ya ufisadi na wengine wanasema ni kama wale Wapalestina wanaojilipua ama KAMIKAZE wa Kijapani.

Kwa Thisday na KULIKONI ni kweli wanakuwa makini mara nyingi, japo kwa sasa kuna kupwaya kidogo. Wanahitaji kurudi kwenye zile enzi za mwanzo.

Kuhusu Raia Mwema, kuna tatizo ambalo sioni kama ni kubwa sana, lakini linatokana na kutokuwa na staff wa kutosha na pia kwa kule kutaka kuwa makini kupita kiasi, wanajikuta wakiacha mambo mengi muhimu, ama kwa kukwepa lawama ama kwa kuwa na sababu za kitaaluma.

Kuhusu Raia Mwema kuchota JF, nadhani si vibaya sana kama JF itakuwa source kuu ya vyombo vya habari maana sisi humu ni sehemu ndogo sana ya Watanzania wengi. Wanaonunua magazeti wengi ni wale wasiopata wasaa wa kuingia katika intaneti na wanaoingia wachache wanaojua JF ni nini na wanaoingia JF hawana muda wa kusoma kila kitu kwa wakati, kwa hiyo bado ni muhimu tukachochea matumizi ya nukuu za JF, muhimu wawe wanasema wanachota wapi na pia muhimu pia wakahakiki (cross check) wasije wakabeba makapi ama wakalishwa kasa.

Otherwise, nyuma ya MwanaHalisi, Thisday/Kulikoni na RaiaMwema, kuna SIRI NZITO ambayo nadhani labda Invisible ama kale ka-inzi kanaweza kunusa. Ni siri njema sana na Mungu ataipa baraka zake.

.
 
Ni kweli kabisa MwanaHalisi si makini, lakini ni MUHIMU katika mchakato wa mapambano ya ufisadi na wengine wanasema ni kama wale Wapalestina wanaojilipua ama KAMIKAZE wa Kijapani.
Kubenea mwenyewe anajua kwua anatumika kama kamikaze?
 
Otherwise, nyuma ya MwanaHalisi, Thisday/Kulikoni na RaiaMwema, kuna SIRI NZITO ambayo nadhani labda Invisible ama kale ka-inzi kanaweza kunusa. Ni siri njema sana na Mungu ataipa baraka zake.
Sipati picha, Kubenea najua anaposimamia, hivi hata Jenerali nae?!.
 
Mwandishi mahili wa gazeti la nipashe mwenye cheo cha News Editor Ndugu Dennis Msaki ameandika barua ya kuacha kazi........................
kuna habari za kuaminika kuwa amekwenda kujiunga na gazeti la mtanzania la kampuni ya habari cooperation ..................................
Hili ni pigo kubwa sana kwa Mzee Mengi ........................................
......waandishi wote hapa news room ipp wanaonyesha kutoamini kilichotokea.

Hii vita ya Rostam na Mengi imeanza kuingia kwenye biashara zao lakini inaelekea wafanya kazi sasa wanatongozwa na kuhamia kambi ya mwenye pesa zaidi.Hata hivyo kwa huyu Ndugu Dennis Msaki kuweka pochi mbele ya uadilifu puts him morally in a very weak position.Kwa mswahili wa kawaida anaona ameshakuwa changudoa.
 
Msaki angalia majani mabichi yako wapi, wewe ni binadamu na una mahitaji na malengo yako. Huhitaji kujiingiza kwenye siasa zao wewe uandishi ndiyo kazi yako na ndiyo kula yako. Kama Habari Corp. kuna maslahi mazuri kwako, una haja gani ya kuendelea kukaa IPPMedia?
Hapa hakuna hata mtu anayekujulia shida zako sana sana tuna piiga porojo tu.
 
mkuu tupo pamoja mie namshauri aende habari corp.....unajua mkuu haya mambo watu wa nje wanaongea tu hawajui maisha ya bwana msacky......maisha yenyewe mafupi wakuu......
 
Msaki angalia majani mabichi yako wapi, wewe ni binadamu na una mahitaji na malengo yako. Huhitaji kujiingiza kwenye siasa zao wewe uandishi ndiyo kazi yako na ndiyo kula yako. Kama Habari Corp. kuna maslahi mazuri kwako, una haja gani ya kuendelea kukaa IPPMedia?
Hapa hakuna hata mtu anayekujulia shida zako sana sana tuna piiga porojo tu.

mawazo ya namna hii ni mawazo ya kitumwa! I'll deal with this next week. Ndio watu walio tayari kuuza utu wao kwa ajili ya njaa zao! Watu wangapi tunashida za maisha yetu ya kila siku na hatujui tutalala wapi the next day lakini hatupigi magoti kwa mafisadi kuganga njaa? Atakayesikiliza ushauri wa namna hii hatustahili!
 
acha wewe hujui life la bongo......msimchagulie jamaa pa kwenda.....
 
"Kwani wapi hawadhulumiwi?

Fatilia New Habari (2006) Limited wahariri na mabosi wengine wote hawana mikataba hawajaelewana na mwajiri wao baada ya kuja na mbinu chafu za kutaka kuwadhulumu na kukwepa kodi. Au unafikiri huku uraiani hatupati taarifa ?"
________________________

Shangazi:
Umenena. Pia hawalipiwi NSSF na walibadilishwa kutoka NSSF kwenda PPF kwa sababu ya kukwepa deni kubwa la NSSF. Ramadhani Dau anashindwa kumshughulikia Rostam simoply because "they a birds of a feather."

Magazeti ya Rostam, hasa yale ya Kiswahili (ukiacha Bingwa na Dimba) hayauzikani siku hizi hasa tangu Muhingo Rweyemamu kuwa Managing Editor kwa sababu stori zinazoandikwa ni zile zitokazo kwa RA za kutetea mafisadi na kuwaponda wale whistleblowers.

Mtanzania inauza nakala 1,900 hadi 2,300 kwa siku na siku hizi wahariri hawapewi taarifa za mauzo kutoka circulation dept (idara inayoendeshwa na huyo Bashe) kwa hofu ya kuwavunja nguvu wahariri.

Isitoshe, siku hizi kuna wadosi kibao wanaoajiriwa pale na inaonekana kama vile kuna ethnic cleansing inayoendelea -- kitu ambacho kinawakera wazalendo. Sijui kama immigration dept inalijua hili. Kuna transport Manager mdosi kaletwa na inasemekana mshahara wake ni 1.5m/- net per month lakini kuna magari 3 anayoyasimamia. Kazi hii angeweza kufanya mzalendo kwa chini ya hela hizo.

Kwa ufupi watu wanaokimbilia kwenda Habari Corp hawajui mambo ya humo ndani.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom