Mwandishi Charles Mullinda "MCHOKONOZI" na Ushushu wa CCM ndani ya gazeti la Dira

Jun 8, 2011
52
19
Kwanza kabisa napenda kumpa pole mwandishi mwenzangu Charles Mullinda ambaye tumewahi kufanya kazi pamoja pale Tanzania Daima mimi niliondoka mwenyewe ili kujikita na shughuli zangu za ujasiriamali ila takribani week tatu zilizopita nimepata taarifa kuwa Mullinda ambaye amewahi kuvuma na safu ya MCHOKONOZI kwenye Tanzania Daima kafukuzwa kutokana na kununuliwa na chama cha magamba CCM pia taarifa zikadai Alex Msama kamwajiri pale Dira Media mitaa ya kinondoni Biafra kama mhariri wa gazeti la Dira linalotoka kila jumatatu.
Mwanzoni nilidhani mwandishi huyo kaonewa ila leo nimelipata gazeti la Dira kutoka kwa rafiki yangu aisee nimekuta makala ya Mullinda ikiwa na kichwa cha habari cha MCHOKONOZI na ndani yake nilichokisoma nikabaini ilikuwa ni haki kwa Tanzania Daima kumtimua , kwani makala yake ni kama mipasho ya taarabu tena na vijembe ya wana CCM huku akitupiana mipasho na mwana CCM mwenzake Hashim Sagaf aliyewahi kuwa mbunge wa Dodoma, ajabu zaidi makala ya Mullinda inaonyesha jinsi gani mwandishi huyo kachuja kiasi cha kujipendekeza kwa Kikwete...teh teh teh! naona jamaa kaenda kuliua gazeti la Dira bilashaka anafanya kazi ya ushushu kwa niaba ya mafisadi wa CCM.....NAWASILISHA
 
Hyu hana lolote. Anatumwa na mafisadi kuchafua watu. Ni huyu Mulinda ambaye alikuwa anamchafua kamanda Sitta na wenzake. Akiwa Mwanza alichukua rushwa na kuponea chuchupu kkamatwa. Alipkuwa Tanzania Daima akachukua rushwa kwa John Komba na kuponea chupuchupu kukamatwa na PCCB.
 
NDUGU yangu Alex Msama huna tena gazeti............. Ulianza kufuata nyayo za Kubenea hasa ulipochapa ile stori ya "Gazeti la Rai lapanga kumpindua Kikwete." Lakini kwa kumpa huyo mla rushwa gazeti, basi nakutakia safari njema ya akhera.
 
Sasa akale wapi kama amefukuzwa huko Tanzania daima?

huo ni unyanyasaji wa kivyama, yaani kwa vile yeye ni magamba ndio asifanye nao kazi? kwani hilo Tanzania Daima limesajiliwa kama gazeti la chama cha chadema? kama ndiyo aliyemfukuza hana kosa na kama siyo aliyemfukuza hajamtendea haki, wizara ya kazi tunaomba wamsaidie.
 
Ulikuwa hujui? Soma makala zake kwenye Tanzania Daima jinsi alivyokuwa akimshambulia Sitta na kupigania Dowans ilipwe.
 
Sasa hivi ni mhariri wa Mtanzania Jumatano. Soma maandiko yake. Ni ya aina ya ki-Mwingulu mwingulu na Kinchemba nchemba.....! Yeye ni Kelele dhidi ya Chadema! Chadema! Chadema! Hana zaidi ya hilo. Soma hata gazeti la Jumatano ijayo. Hukosi habari ya kuishambulia Chadema.
 
Back
Top Bottom