Mwanaume wa kizungu amkata mrembo wa kitanzania uingereza

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Mrembo wa Tanzania Aolewa na Kibabu cha Kiingereza, Anusurika Kukatwa Mikono Yake

Sunday, December 04, 2011

Mwanamke mrembo wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 25 tu amekiona cha moto baada ya kukubali kuolewa na babu wa Uingereza mwenye umri wa miaka 69 na matokeo yake kujeruhiwa kwa kisu alipolalamika pafomansi mbovu ya babu kitandani.

Mwanamke wa Kitanzania aliyejulikana kwa jina la Saada Mwiazimu mwenye umri wa miaka 25 amenusurika maisha yake baada ya kujeruhiwa kwa kisu na mumewe mfanyabiashara wa Kiingereza mwenye umri wa miaka 69 anayejulikana kwa jina la William Porter.

William anamiliki saluni maarufu ya masuala ya urembo inayojulikana kwa jina la Tan Express iliyopo kwenye mji wa Scarborough, kaskazini mwa Uingereza.

Kasheshe la Saada kujeruhiwa kwa kisu lilitokea mwezi juni mwaka jana wakati Saada na mumewe walipokuwa kitandani wakiangalia DVD.

Mazungumzo yao yalipelekea Saada kuzungumzia pafomansi mbovu ya William kwenye malavi davi na kupelekea William kukasirika sana.

William alimdondosha chini Saada na baadae kumjeruhi kwa kisu mikononi huku akitishia kuikata mikono ya mke wake huyo aliyemleta toka Tanzania.

Kesi ya William kumjeruhi Saada ilifikishwa mahakamani na wiki iliyopita ndiyo hukumu ilitolewa ambapo William alipatikana na hatia ya kufanya shambulio la kudhuru mwili na kuhukumiwa kwenda jela miezi 15.

Mwanzo wa yote ilikuwa mwaka 2009 wakati William aliposafiri kuja Tanzania kuonana na Saada ambaye alimjua kupitia dada yake ambaye yupo Uingereza na kuanza kuwasiliana naye kwa kutumia email.

Kukutana kwao kulipelekea kuanza kwa uhusiano wa mapenzi ambapo William alimualika Saada Uingereza ili pia aje akutane na dada yake. Ujio huo haukudumu muda mrefu kwani Saada alikamatwa akiishi Uingereza akiwa amepitiliza muda wake wa kuruhusiwa kuishi Uingereza. Alirudishwa Tanzania na maafisa wa uhamiaji wa Uingereza.

William aliamua kutumia njia ya kumuoa Saada ili waweze kuishi pamoja Uingereza. William kwa mara nyingine alikuja Tanzania na kumuoa Saada mwezi januari mwaka jana na kuanza mikakati ya kumtafutia viza ili aruhusiwe kuishi Uingereza. Baada ya vipingamizi vya hapa na pale hatimaye Saada alipewa viza na kuwasili Uingereza mwezi mei mwaka jana.

Saada aliishi pamoja na William kwenye nyumba ya juu katika ghorofa linalomilikiwa William ambapo mke wa zamani wa William alikuwa akiishi nyumba ya chini.

Hatimaye mwezi mmoja baada ya kuhamia kwenye nyumba hiyo ndipo sakata hilo lilipotokea na kupelekea Saada abaki na makovu kwenye mikono yake.

Akijitetea kabla ya kuhukumiwa kwenda jela miezi 15, William aliiambia mahakama kuwa kesi hii ilipangwa na mkewe ili aweze kumkimbia aendelee kuishi Uingereza.

Mahakama ya York Crown Court ilimuona William ana hatia ya kumshambulia mkewe kwa kisu cha urefu wa inchi 12 na kumhukumu kwenda jela.
 
sasa...mbona Tarime wana katwa sana...!!huyo amekoswa koswa... si arudi kwenye pafomance..
 
sasa...mbona Tarime wana katwa sana...!!huyo amekoswa koswa... si arudi kwenye pafomance..

tarime wanakatwa na nani!? wanawake ndio wanakatwa? hii ji hatari tupe details wanaharakati
 
shuka tarime...nenda musoma...baada ya masaa 24...utatoka na hizo hadidhi zako za kutosha...wasiliana na mtangazaji wa TBC musoma atakupa michongo ya mtindo huo...
 
mange atawapoteza sana nyinyi dada zetu

Bora hata nyie kaka zetu mseme maana akisema mwanamke mara tunaambiwa wivu tu tutafute wazungu wetu blah blah blah lakini its not worth it. Umaskini ni kazi sana kwa kweli
 
Bora hata nyie kaka zetu mseme maana akisema mwanamke mara tunaambiwa wivu tu tutafute wazungu wetu blah blah blah lakini its not worth it. Umaskini ni kazi sana kwa kweli

Sahani nafikiri sio masikini....hao...ni masuala la nyege...manegiment
 
shuka tarime...nenda musoma...baada ya masaa 24...utatoka na hizo hadidhi zako za kutosha...wasiliana na mtangazaji wa TBC musoma atakupa michongo ya mtindo huo...

poa .. nimekusoma kaka.. lakini hawa labda ndio mila zao?
 
Bora hata nyie kaka zetu mseme maana akisema mwanamke mara tunaambiwa wivu tu tutafute wazungu wetu blah blah blah lakini its not worth it. Umaskini ni kazi sana kwa kweli

upo sawa dada yangu huu umaskini ndio unaleta haya yote .. elimu ndio solution ..
 
Bora hata nyie kaka zetu mseme maana akisema mwanamke mara tunaambiwa wivu tu tutafute wazungu wetu blah blah blah lakini its not worth it. Umaskini ni kazi sana kwa kweli

Sahani nafikiri sio masikini....hao...ni masuala la nyege...manegiment
sio nyege kaka ni umaskini
 
hayo ni matokeo ya kina Mange na wenzie kuhamasisha kigori wa miaka 25 aolewe na babu wa kizungu....life is all about choices...
 
25 kwa 69...alitegemea nini wakati anakubali kuolewa nae? Viagra?
Tena ana huruma sana huyo mzungu.
 
Tarime?!, mbali kote huko!, nenda kitunda, kivule, nyantira et al uone kazi yake- kila siku polisi post wanakesi kibao za aina hiyo.
shuka tarime...nenda musoma...baada ya masaa 24...utatoka na hizo hadidhi zako za kutosha...wasiliana na mtangazaji wa TBC musoma atakupa michongo ya mtindo huo...
 
Back
Top Bottom