Mwanaume wa kileo ni kichwa cha mke wake au ni miguu?

Nimekuwa nikiangalia jinsi wnaume wa sasa hivi wanavyowaachia wake zao majukumu yote nauliza nyie wanaume mnaopenda kulelewa na wake na wapenzi wenu nyie ni vichwa au miguu?

Wakati mwingine watu waache ujinga, hebu tujikumbushe maisha ya wazazi wetu siku za nyuma hasa huko vijijini

1. Mume na mke wote wanaelekea shamba kulima mazao ya biashara n chakula, mfano pamba na mpunga huko shinyanga. Msimu wa mauzo ukifika, baba anapeleka mazao sokoni na kurudi na pesa. Hapo ananunua mahitaji mbalimbali ya familia yakiwemo ya mkewe. Swali je, mme anamtunza mke, mke anamtunza mme ama wanatunzana?

2.Baba mvuvi na mama mkulima wa mazao ya chakula. Baba anapata kitoweo na mama analeta nafaka. Sehemu ya mazao ya uvuvi (samaki) baba anauza kwa ajili ya ada za watoto, tiba, nguo za mkewe. Swali je, mme anamtunza mke, mke anamtunza mme ama wanatunzana?

MJINI
1. Baba meneja na mama Mkurugenzi. Baba anachangia mahitaji ya familia na mama naye pia. Swali je, mme anamtunza mke, mke anamtunza mme ama wanatunzana?

2. Baba meneja na mama Mkurugenzi. Baba anachangia mahitaji yote ya familia na mama anabana mshahara wake kwa kuwa mme ni kichwa cha nyumba. Swali je, mama si anamyonya mmewe?
Kwanini aende kazini ilihari mshahara wake hautumiki kwa malengo ya familia, anafanya kazi ili iweje? Kwanini asiache kazi akalea watoto wakapata afya njema na malezi bora kuliko kumwachia house girl

BINAFSI NILISHACHIMBA MKWARA, MKE WANGU AKIINUA MGUU KWENDA KAZINI LAZIMA MCHANGO WAKE UONEKANE. UKIDUME WAKATI ANANINYONYA NI UJINGA MTUPU. GARI NINUNUE, MAFUTA NIWEKE, HALAFU MSHAHARA APELEKE ANAKOJUA!

Normally huwa nahiitaji 40% t0 50% ya mshahara wake achangie kwenye familia, then mengine nayabeba mwenyewe

Sorry kwa kuwachosha


2
 
Back
Top Bottom