Mwanaume wa kileo ni kichwa cha mke wake au ni miguu?

Ritakahama

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
758
408
Nimekuwa nikiangalia jinsi wnaume wa sasa hivi wanavyowaachia wake zao majukumu yote nauliza nyie wanaume mnaopenda kulelewa na wake na wapenzi wenu nyie ni vichwa au miguu?
 
hahahaha heading ya post yako inachekesha sana! hahaha

ngoja kwanza nimalize kucheka nitarudi kuchangia.
 
Nimekuwa nikiangalia jinsi wnaume wa sasa hivi wanavyowaachia wake zao majukumu yote nauliza nyie wanaume mnaopenda kulelewa na wake na wapenzi wenu nyie ni vichwa au miguu?

Tatizo ni nyie wanawake mmekiuka majukumu yenu kama vile
1.Badala ya kuzaa kwa uchungu siku hizi mnaomba operesheni
2.Badala ya kukaa nyumbani kulea familia mnakimbizana na miajira migumu badala ya kuwaachia waume zenu wawatafutie mkate wa kila siku
3.Mnataka haki sawa kwahiyo lazima wawaachie majukumu
 
kwani kule China walidai 50/50 kwenye makaratasi tu au na kwa vitendo? Mnalalamika wakati ndiyo kwanza mnaolea wanaume ni 5% wakati wanaume tunaowalea wanawake ni 95%. Je uwiano ukiwa sawa si ndiyo mtatuburuza mpaka basi, Mungu pishilia mbali.
 
We unaonaje? Hizo haki zenu mnazodai hamkufikiria hilo kama mshindo nyuma wa madai yenu.
 
Mi nahisi watakuwa ni miguu hao.
 
Tatizo ni nyie wanawake mmekiuka majukumu yenu kama vile
1.Badala ya kuzaa kwa uchungu siku hizi mnaomba operesheni
2.Badala ya kukaa nyumbani kulea familia mnakimbizana na miajira migumu badala ya kuwaachia waume zenu wawatafutie mkate wa kila siku
3.Mnataka haki sawa kwahiyo lazima wawaachie majukumu

he sasa kuzaa kwa operation we unakereka nini badala ya kufurahi mkeo antunza mwili wake?Nikaa nyumbani upo tayari kunipa kila ninalohijati na kusidia wanaohitaji msaada wangu?
 
kwani kule China walidai 50/50 kwenye makaratasi tu au na kwa vitendo? Mnalalamika wakati ndiyo kwanza mnaolea wanaume ni 5% wakati wanaume tunaowalea wanawake ni 95%. Je uwiano ukiwa sawa si ndiyo mtatuburuza mpaka basi, Mungu pishilia mbali.

Mpaka ninapoandika hapa nimekaa ofisi moja yenye zaidi ya watumishi mia tatu kwa miaka 5 ukweli ni dada mja tu amewahi kuniambia at least mume wake alimnunulia gari lakini matumizi yote nyumbani anatoa wengine wote wakikuhadithia unaetemeka sasa wewe hiyo 95% unayosema ni ipi
 
We unaonaje? Hizo haki zenu mnazodai hamkufikiria hilo kama mshindo nyuma wa madai yenu.

Na kama unaishi ndani na mkeo badalaa ya kumuangalia yeye kama mkeo unamwangalia kama mbeijing na kumwachia atunze familia jua kuna mwanaume mwenzako nyuma anakutunzia watoto wako if at all ni wako
 
Mpaka ninapoandika hapa nimekaa ofisi moja yenye zaidi ya watumishi mia tatu kwa miaka 5 ukweli ni dada mja tu amewahi kuniambia at least mume wake alimnunulia gari lakini matumizi yote nyumbani anatoa wengine wote wakikuhadithia unaetemeka sasa wewe hiyo 95% unayosema ni ipi

kama anafanya kazi ni lazima kuchangia gharama za matumizi nyumbani, kwa mawazo yako unataka fedha ya mshahara wake isitumike nyumbani kwake? chunguza hapo kazini kwako ni wanaume wangapi wanalelewa na wake zao na wangapi wanalea wake zao. Mwanaume humtegemea mwanamke pale tu anapokuwa hana kipato, lkn akiwa na kipato kamwe hawezi kumtegemea mwanamke. Kiasili mwanaume akimtegemea mwanamke hupungukiwa ujasiri kiasi fulani kitu ambacho wanaume wote hatupendi.
 
Umesoma mahali nimeandika mshara usitume?hii mada haihusu kabisa kusaidiana inahusu kuachia mke majukumu yote
 
umenichekesha, mke akiachiwa mujukumu yote ataweza? Kwa jinsi ninavyowafahamu wanawake, ikifikia hatua ya mke kuachiwa majukumu ya nyumbani kwa 100%, hapo piga ua lazima adai kuachika. Pia inaonekana umo kwenye mahusiano ya namna hii, umeleta uzi huu kupunguza stress au kujifariji, kama koti linakubana dada yangu, livue, litakuua.
 
Umenena vema mkuu,
 
Back
Top Bottom