Mwanaume wa aina tumwiteje

Nahisi jamaa kazoea miteremko kabla hata hajaoa. Isije ikawa ni side B!..

Ndiyo tukisema ndoa ni ngumu inategemea na mtu uliyekutana nae ndoani..kama huyo jamaa ni presha! Mwambie bibie aongee nae kwa kina kuhusu hiyo tabia.
 
Jamani umeolewa na mwanaumwe hataki kazi.
Asubuhi adi jioni anashinda home na housegal na mtoto wake.
Hatoki ajishungulishi yeye akiamuka anakaa kwenye kochi akichoka anaeingia kulala ndani.
Ni kula kulala kudhurula mtaani na kusema uongo mbele za watu yeye ana pesa yeye alienda ulaya na masifa ya kijinga.

Huku mkewee ndo kila kitu nyumbani kuanzia kulipa hs gal gardener kulipia bill za maziwa watoto
i mean kila kitu ni mwanamke.mafuta ya gari yani kila kituuuuuu namaanisha mwaswala yote ili maisha yaaendee na watu waendee chooni kutoa shukurani zao.

Siku akitoka mwanaume huyuu akitoka ataenda kudhurula kwenye ofc za washikaji zake akirudi ni usiku kalewa chakariiiiii.
Na matusi anatukana kama katumwa na Matusi mie nina nyumbaa nikichoka nauza nyumba narudi kijijini.Mkewee akimuuliza unatoka wapi saa nane usiku huu atajibu alikuwa anatafuta kazi jamani jamani ni ugomvi kila kukicha.

sasa nyie wanaume mwenzie tusaidie jamani huyu mwanaume amesoma ana Bachelor degree.Inakuwaje asitafute kazi jamani ili amusaidie mkewe mzigo wa familia jamani.mama mwanamke nae anatakiwa ajirembe avae vizuri NK.maisha yanakuwa magumu ugomvi ndani auishi.
Tusaidie jamani akina baba wa leo ndo mwanaume watakiwa kuishi hivyo au huyuu mwenzenu anamatatizo gani.
Tujuzeni ili tujiandaee kwa maisha ya ndoa na sie akina nungayembee.

Ndio shida ya wanawake kupenda mabraza men. Unataka bonge la handsome, misheni town bila kufikiria hiyo ni sehemu ndogo tu ya ndoa. Any way kama ni mmeo mvumilie kama sio mmeo na hujaolewa jifunze. Kama sio mmeo na umeshaolewa hayakuhusu.
Mimi ni mwanaume, ninaamini sehemu kubwa ya sista du au mwanamke mrembo sana si mtu wa kuoa, spend naye then sepa.
Pole kama nimekuboa
 
simpo..chuku avyeti vyake mtafutie kazi kama kweli wampenda mumeo.......akikataa kazi utapata majibu una mme wa aina gani..mtaftie ata tempo tu!!.....

Mkono wa paka nimesha chukua vyeti vyake nimeomba kaziii weee akipigiwa simu haijui hapokei simu itaaita adi kesho.
 
Loh! Mzigo huo anauwekea nini? Asimjazie choo mwambie akae nae chini amwambia atafute kazi au ajipange,imetosha alivyo mfunga...
 
" Bora ukichaa wa mwanaume kuliko Wema wa Mwanamke."

Hivi wanawake mna nini mbona huko Nyuma hamkulalamika kwanini 2nahudumiwa kila kitu. Mwanaume anakuletea kila kitu we unaweka tumboni.
Leo kumuhudumia mwenzako imekuwa kero,mbona huko nyuma Tuliwavumilia na kutokutusaidia ki2 ila kupika,umbea na kulea watoto. Ci ndo tunatoka jasho, we lako umeliacha mwilini.

Leo jasho lako kukutoka unaona kero, mvumilie na kama kumtafutia kazi mtafutie.. Hata cic 2likuwa tunawapa mitaji ya Nyanya mnauza.. Sasa mwanamke magar unayo kila ki2 unacho. Eti akili ya kumpa mtaji huna. Araaaa

Basi mkataka Haki sawa tukawasupport mmeipata, leo Mwenzako yupo tena anadegree yake anasubiri kazi atapata wapi, we umeshamchoka mpewe nini ilimridhike, kwenye mapenz hamridhiki, mmepewa haki hamridhiki mnataka nini sasa.
 
ndo maana mi nakagua hadi ukucha? je ni wa kiume kweli? watu wanadhani wanaume woote ni wanaume.kuna mwanaume akikuangalia tu unajua huyu sio wa kiume mbona macho tu unajua hii bidhaa ya kichina hii.
selection up to infinite


Inabidi tufanye survey kati ya wanaume na wanawake zipi ni bidhaa za kichina zaidi! Kwani Beijing ilikuwa inahusika na nini?
Halafu huyo mama anajua ugumu wa kupata ajira? Kama yeye kabahatika asifikiri kwa wote ipo hivyo. Kuna watu wanasota hadi miaka mitano no ajira.
Na huko maofisini anakozunguka anajuaje kama haulizii chance za ajira. Kulewa pombe ni matokeo ya hizo frastuations!
 
huyo mwanaume ni goaldiger au opportunist, wapo wengi sana now days hapa mjini hata silelewi ni pepo gani anawasumbua wanaume jamani
 
Akina dada timing muhimu. Kipindi kile una 22,23, 24,25 kuna watu wa ukweli wanakuja wanakuwaga washamba hawafanani nawe yaani hata kuwatambulisha kwa washikaji ni ngumu "" Wanaume"". Basi mvumilie huyo Sharobaro ( Aliyeuza sura hata kitanda aliazimaga) cha msingi siku akienda ukweni mwache peke yake halafu waambie kakazo wampeleke akachote maji na kuokota kuni la sivyo atoe pesa.
 
huyu hata akipata kazi anaweza asiwe na msaada wowote nyumbani - sana sana anaweza kuongeza kasi ya kupiga kinywaji, kumaintain nyumba ndogo mitaani na kurudi home alfajiri - probably dada alimzoesha hivyo tangu awali, so jamaa ameshapinda na itakuwa ngumu kumnyoosha tena
 
Hapo kazi ipo na nna wasi wasi na hy bachelor yake. Kama c ya kuzawadiwa basi aliimunua na kama ni ya kweli ''njoo ufanyiwe maombi''
 
We mbano...
Divorce siyo solution..
Wala kutafuta kuajiriwa siyo solution..
Solution mpe mtaji,na msaidiane kuendesha maisha yenu kwa biashara ambayo mtaiamua wenyewe,si lazima ya mtaji mkubwa..

Wajua Bachelor si kitu siku hizi,kazi inategemea mengi siku hizi.. Ulichosoma,uzoefu,referee,influence,etc.
Pengine kazi zipo,ila anaona zinamdhalilisha,au zina mshahara mdogo kwa maoni yake..
 
ndo maana mi nakagua hadi ukucha? je ni wa kiume kweli? watu wanadhani wanaume woote ni wanaume.kuna mwanaume akikuangalia tu unajua huyu sio wa kiume mbona macho tu unajua hii bidhaa ya kichina hii.
selection up to infinite

Mchagua nazi , uchagua koroma !!!
 
Tatizo hapa ni mitazamo tofauti katika maisha ya pamoja,siamini mtu aliyekaa darasani amue kukaa nyumbani bure.maisha ya leo sehemu kubwa yametawaliwa na fedha,dharau inayojitokeza kwa mume ni kwa kuwa hana kipato na amekuwa tegemezi kwa mkewe.mume akiamua kujiajiri na akapata kipato heshima itarudi.tatizo la ajira ni kubwa na wasomi wengi wakimaliza shule wanaamua kujiajiri.
Tatizo wamama wengi wanadhani wanaweza kupata security kwa mwanaume aliye na ajira,kuna mtu anakesha kazini lakini kipato hakitoshelezi nyumbani.
Ni vyema kushirikiana katika kutafuta njia ya kusaidiana kuliko kuweka tofauti za kipato.mke ampe kujiamini mume.
Mume akija kufanikiwa kutakuwa na furaha ya pamoja na kulea familia bora.
 
kazi za police wa chuo hapa pale udsm zimetoka afanye application atapata kazi asiwe mjinga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom