Mwanaume Mzee Kuliko wote Duniani Afariki Akiwa na Umri wa Miaka 113

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
2550746.jpg

Henry Allingham Sunday, July 19, 2009 2:35 AM
Mwanaume aliyekula chumvi nyingi kuliko wanaume wote duniani Henry Allingham amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 113. Mzee Henry Allingham wa nchini Uingereza alishiriki katika vita vyote viwili vya dunia.

Allingham alilitumikia jeshi la anga la Uingereza katika vita ya kwanza ya dunia na alishiriki katika vita ya pili dunia kama mtaalamu wa mabomu.

Mbali na kuwa mwanaume mzee kuliko wote duniani, Allingham alikuwa pia ndio mtu wa mwisho kunusurika katika vita ya kwanza ya dunia kutoka kikosi cha jeshi la anga la Uingereza.

Kufariki kwa Allingham kunamaanisha kuwa Uingereza imebakia na mtu mmoja tu aliyenusurika kwenye vita ya kwanza ya dunia Harry Patch ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 111.

Harry alipigana katika vita hivyo katika eneo la Passchendale mwaka 1917. Eneo hilo ndilo ambalo damu ilimwagika sana kuliko maeneo yote ya vita hivyo. Wanajeshi 70,000 wa Uingereza walifariki katika eneo hilo.

Akielezea siri ya maisha yake marefu Harry Patch alisema kuwa yeye havuti sigara, hanywi pombe na hachezi kamari na kwa kuepuka madhambi hayo matatu ameweza kuwa na maisha marefu.

Henry Allingham yeye alikuwa tofauti kabisa na Harry kwani yeye alikuwa ni mtu anayependa sana sigara, kunywa pombe kali na kujirusha sana na mademu.

Mke wa Henry, Dorothy alifariki mwaka 1970 baada ya miaka 53 ya ndoa yao wakiwa na watoto wawili wa kike, wajukuu sita, vitukuu 16 na na vilembwe 21.


nifahamishe.com
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom