Mwanaume mwezini.

Nilikuwa msomaji na mpenzi mkubwa wa gazeti la Jitambue ambalo kwa muda mrefu sasa halipatikani mtaani.Katika gazeti hilo mambo mengi kuhusu saikolojia yalizungumzwa na kutolewa ufafanuzi.Moja ya jambo ambalo liliwahi kuniacha hoi katika moja ya makala ya gazeti hilo,ni ile iliyokuwa inazungumzia kuhusu wanaume kuingia kwenye mzunguko wa hedhi kama walivyo wanawake.Gazeti hilo lilitaja baadhi ya dalili za kumgundua mwanaume kuwa yuko katika siku zake ni pale anapokuwa na hasira kupita kiasi au anaonekana kubadilika kabisa tofauti na tabia yake halisi.

Wenzangu imekaaje hii?!

Una umri gani vile? :fencing:
 
kwa namna zote, hakuna kitu kama hicho........nafikiri ndio maana gazeti hilo halitoki tena kama story zenyewe ndio kama hizo.
...Nadhani na mmiliki wa hilo gazeti Munga Tehenani alishakufa...Kuna baadhi ya habari kwenye hilo gazeti hata mimi zilikuwa zinanishangaza kama kweli ni tafiti za kisayansi au ni uchakachuaji tu...MOjawapo ndio hiyo ya mwanaume kuingia mwezini (sijui walikuwa wakielewa walichokuwa wanaandika??):tape::nono:
 
Nafikiri walikuwa wanafanya hivyo ili kuuza gazeti
 
NAHISI UPINZANI UNTOKANA NA MANENO YALOTUMIKA' MAZUNGUKOWA HEDHI...MWEZINI...' YANASABABISHA VDUME VIJAE UPEPO...LAKINI NAHIC KUNA UKWELI FLANI HAPO!!:smile-big:
 
NAHISI UPINZANI UNTOKANA NA MANENO YALOTUMIKA' MAZUNGUKOWA HEDHI...MWEZINI...' YANASABABISHA VDUME VIJAE UPEPO...LAKINI NAHIC KUNA UKWELI FLANI HAPO!!:smile-big:

Give us empirically verifiable scientific proof to support this tomfooleric claim
 
Gazeti lile lilikuwa linamilikiwa na Munga Tehnan (RIP) baada ya kufariki ndio maana halionekani tena.....mi nadhani kuna ukweli......teh teh teh

duh, sikuwa na habari kuwa huyu bwana ni marehemu. nilikuwa msomaji wake mkubwa na mara nyingi tulikutana mahali kujadili naye mamabo ya saikolojia na hata wakati fulani tulirekodi vipindi TVT ya enzi hizo... oooh RIP Munga, angalau amerudi kwa mola aliyemleta na kuacha kitu kama (hedhi kwa wanaume!) KIKIFIKIRISHA WATU..
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom