Mwanaume Mwenye Bahati Mbaya Kuliko Wote Uingereza

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,079
4354390.jpg

Mick akiwa hospitali baada ya ajali mbaya hivi karibuni Wednesday, April 14, 2010 9:49 PM
Mkulima wa nchini Uingereza Mick Wilary ambaye anadaiwa kuwa ndiye mtu mwenye bahati mbaya kuliko wote nchini Uingereza kutokana na ajali kibao zinazomkumba, amepata ajali kwa mara nyingine tena iliyoivunja miguu yake yote miwili. Mick Wilary, mwenye umri wa miaka 58 anadaiwa kuwa ndiye mtu ambaye hana tabasamu kutokana na bahati mbaya zinazomkumba na kumfanya akumbwe na ajali mbaya zinazoyatia maisha yake hatarini.

Mick ameishakumbwa na ajali mbaya zaidi ya 30 na ajali hizo zimepelekea kuvunjika kwa mifupa ya viungo vyake 15.

Katika tukio la hivi karibuni, Mick anaendelea kupatiwa matibabu hospitalini baada ya miguu yake kupondwa na tingatinga.

Katika tukio hilo dereva wa tingatinga akiliendesha tingatinga hilo modeli ya JCB bila ya kuwa mwangalifu, alimgonga Mick na kumbamiza ukutani.

Katika tukio hilo mguu wa kushoto wa Mick ulivunjika na kupinda kuelekea mabegani wakati mguu wake wa kulia ulijeruhiwa na kugeuka ukiangalia nyuma.

Hata hivyo pamoja na ajali hiyo mbaya ya kutisha, madaktari katika hospitali ya Newcastle wamefanikiwa kuiokoa miguu yake na wamesema kuwa ndani ya miezi sita Mick ataweza tena kuitumia miguu yake kutembea.

Ajali ya kuvunjika kwa miguu yake imetokea ikiwa ni miezi michache baada ya kuvunjika kwa enka za miguu yake yote miwili baada ya kuteleza na kuanguka chini alipokanyaga kiazi mviringo.

Miongoni mwa ajali mbaya zilizowahi kumkumba Mick ni kupasuka kwa fuvu la kichwa chake kwenye sakafu alipopigwa mweleka na paka.

Mick pia ameishawahi kuvunjika mbavu, shingo na mikono katika mfululizo wa ajali mbaya zinazoendelea kumkumba ambazo zimeifanya sura yake ikose tabasamu wakati wote.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4354390&&Cat=7
 
Ni kweli inabidi akabidhi maisha yake kwa mola ..ajali zaidi ya 30 ananusurika lakini pia ana bahati ya pekee
 
Ni kweli inabidi akabidhi maisha yake kwa mola ..ajali zaidi ya 30 ananusurika lakini pia ana bahati ya pekee
Na mie nadhani ana bahati nzuri kuliko wote.kupata ajali mara 30 na kupona sio jambo la kawaida.Ni Mungu ana mpenda anatakiwa akaombewe fasta.
 
Na mie nadhani ana bahati nzuri kuliko wote.kupata ajali mara 30 na kupona sio jambo la kawaida.Ni Mungu ana mpenda anatakiwa akaombewe fasta.

akaombewe tena wakati ana bahati ya pekee na Mungu anampenda???

halafu nyie mnaosema watu waombewe, kwani wamekufa? kwani wao kuomba hawajui?
Utegemezu tuuuuhadi kwenye kusali tunataka watu wengine watusaidie!!
 
Yeye anahitaji kutoa shukrani na sadaka kwa mungu kwa kumnusuru na kumlinda katika ajali hizo 30 . Na inaelekea ni mcha Mungu ndio maana amenusurika zote hizo !!! Shindwa ktk jina lake !!!
 
Back
Top Bottom