Mwanaume Muuaji wa Wanawake aibuka Dar

Freestyler

Senior Member
Dec 15, 2010
198
9
Hali ya hatari imejitokeza hivi karibuni jijini Dar es Salaam baada ya kuibuka mwanaume mmoja anayedaiwa kuua wanawake.

Mwanaume huyo ambaye anasakwa na polisi, anadaiwa kuwa ndiye aliyewaua wanawake watatu kwenye nyumba za kulala wageni huku mwanamke mmoja akinusurika kufa.

Vifo hivyo vya kusikitisha vilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo Jumatano ya Februari 23, mwaka huu, aliyekuwa anadaiwa kuwa ni mwanafunzi wa Ubungo Islamic High School, Amina Ramadhani aliingia na mwanaume anayetuhumiwa kwa mauaji hayo kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Mkomboni iliyopo Kinondoni Mkwajuni.
Baada ya muda mfupi mwanaume huyo aliondoka. Wahudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni (gesti) walimkuta msichana huyo kwenye chumba namba sita akiwa amekufa huku akichuruzika damu mdomoni.

Wakati mwili wa marehemu ukichukuliwa kwenye gesti hiyo, wahudumu na baadhi ya watu walidai kumwona mwanaume anayetuhumiwa kwa mauaji hayo kabla ya tukio hilo. Waliuelezea mwonekano wake kuwa ni mwembamba, mrefu, mweusi na anapenda kuvaa kofia ya kufunika uso ‘kapelo'. Walieleza kuwa haikuwa siku yake ya kwanza kulala kwenye gesti hiyo.

Mwili wa marehemu Amina ulitambuliwa na ndugu zake katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar, Februari 26, mwaka huu ambapo waliuchukua kwa ajili ya kwenda kuuzika.

Wakati Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni likijipanga kumsaka muuaji huyo, kesho yake mwanamke mwingine alikutwa amekufa kwenye gesti nyingine.

Mwanamke huyo ambaye mpaka jana Jumatatu mwili wake ulikuwa bado haujatambulika ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Temeke, alikutwa amekufa kwenye chumba namba 108 ndani ya ‘gesti' ya Four A iliyopo Tandika Transformer jijini Dar.

Inadaiwa kuwa marehemu huyo naye aliingia chumbani na mwanaume aliyekuwa amevaa ‘kapelo' anayeshukiwa kuwa ndiye aliyefanya mauaji ya awali.

Baada ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi wa awali eneo la tukio, ulikutwa umekatwa sehemu za siri huku ukivuja damu nyingi puani, hali iliyoonesha kuwa kulikuwa na imani za kishirikina katika tukio hilo.

Inaelezwa kuwa baada ya kifo cha mwanamke huyo, mtuhumiwa alitokomea kusikojulikana ambapo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke kwa kushirikiana na wenzao wa sehemu mbalimbali wanaendelea na juhudi za kumsaka mtuhumiwa.

Katika tukio hilo, wakazi walioshuhudia marehemu akitolewa kwenye gesti hiyo walionekana kuchanganyikiwa na kukumbushia tukio lingine la mauaji lililotokea hivi karibuni.

Katika tukio hilo, mwanamke mwingine aliyetajwa kwa jina moja la Hadija ambaye aliingia kwenye nyumba ya kulala wageni ya Ngekewa akiwa na mwanaume mweye wajihi kama wa yule anayevaa ‘kapelo' na baada ya muda mfupi akakutwa amefia chumbani katika mazingira ya kutatanisha.

Mwili wa Hadija ulikutwa umelala kitandani kwenye chumba namba sita cha ‘gesti' hiyo huku mwanaume aliyeingia naye ambaye anatuhumiwa kwa mauaji hayo akitokomea kusikojulikana.

Baadhi ya watu waliowaona wauaji kabla ya matukio hayo wameeleza kuwa watuhumiwa hao wanaonekana katika mwonekano unaofanana na wengine kudai huenda ni mtu mmoja.

Inaelezwa kuwa mwanamke aliyenusurika kufa baada ya kutoka mbio chumbani akiwa na kanga moja, aliwaambia wahudumu wa nyumba moja ya kulala wageni ya Mkomboni iliyopo Kinondoni Mkwajuni, Dar kuwa alichokiona chumbani humo hajawahi kukiona maishani mwake.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke, David Misime, amewaomba wananchi kutulia wakati wakiendelea na uchunguzi na ametoa wito kwa mtu yeyote aliyepotelewa na ndugu yake ambaye ni mwanamke afike Hospitali ya Temeke kuutambua mwili wa mwanamke huyo.

Source

Napata shida kutofautisha 'facts' na 'udaku'...mwenye upande wa pili wa hii habari atujuze!
 
Heaven Forbid this......!!! inauma kweli na kutia hofu,sasa itabidi tuwe tunachukua vibali polisi kabla ya kwenda guest na mtu aache vitambulisho vyake pale,mkimaliza mnaenda kuvichukua kila mmoja akiwa salama...!!!
 
Inaelezwa kuwa mwanamke aliyenusurika kufa baada ya kutoka mbio chumbani akiwa na kanga moja, aliwaambia wahudumu wa nyumba moja ya kulala wageni ya Mkomboni iliyopo Kinondoni Mkwajuni, Dar kuwa alichokiona chumbani humo hajawahi kukiona maishani mwake. Aulizwe vizuri huyo dada atuambie nini alichoona ili tufanikishe kumpata Mr. Kapelo. Kwa ujumla hii ni hatari kwani tabia ya serial killer ndo hiyo
 


MAUAJI WANAWAKE 7 GESTI, DAR YATIKISIKA
  • Posted by GLOBAL on May 3, 2011 at 8:00am
Na Makongoro Oging'
Jiji la Dar es Salaam lipo katika mtikisiko mkubwa kufuatia kuibuka kwa wimbi kubwa la mauaji ya wanawake katika nyumba za kulala wageni (gesti), Uwazi halijaacha kitu.

Hali hiyo imejitokeza siku chache baada ya kuongezeka kwa vitendo hivyo ambapo mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Rafaela Joseph (28), mkazi wa Kurasini jijini Dar kukutwa ameuawa chumba namba nane, kwenye gesti moja iliyopo Keko Machungwa.

Habari za kipolisi zinasema kuwa, mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Ayubu anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kilwa Road jijini Dar kwa mahojiano zaidi kufuatia vifo hivyo.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, huku jeshi hilo likiwa limejipanga kukabiliana na wimbi hilo la mauaji, pia limefanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa mwingine aliyetajwa kwa jina la Paskal Nesto akiwa na maiti chumbani.

Nesto alitiwa mbaroni wilayani Kinondoni baada ya kuhisiwa kuhusika na tukio hilo.
Katika hali ya kushangaza, ndani ya kipindi cha miezi mitatu jijini Dar, tayari wanawake saba wameuawa, mmoja wao akikutwa amenyofolewa sehemu zake za siri, hali inayoashiria kuwa mtandao huo ni mkubwa na kuna ushirikina ndani yake.

Mauaji ya mwisho ni ya Rafaela ambaye anatajwa kuwa ni mwanafunzi wa Chuo cha Uuguzi cha Princess cha jijini Dar es Salaam. Yeye baada ya kuuawa, muuaji alimkunja na kumficha chini ya uvungu wa kitanda katika chumba walichopanga.

Maiti ya msichana huyo ilikutwa ikiwa na damu sehemu mbalimbali za mwili kama masikioni.
Gazeti hili lilizungumza na mmoja wa ndugu zake, Victor Uisso ambaye alikuwa na haya ya kusema: "Kifo cha mama mdogo Rafaela ni cha kusikitisha sana. Tulielezwa kuwa, saa 12:00 jioni, Jumatatu iliyopita alimtaarifu rafiki yake (hakutajwa jina) kuwa aliitwa na mwanaume aliyemtaja kwa jina la Ayub ili akachukue fedha.

"Alipokwenda hakurudi, ilipofika saa moja walimpigia simu lakini ikawa inaita tu bila kupokelewa, baadaye ikazima.

"Jumanne saa 3:00 asubuhi mpangaji mwenzangu akanieleza kwamba, kuna binti amekutwa amekufa gesti. Tulikwenda, tukakuta mwili umechukuliwa na polisi kwenda Hospitali ya Temeke. Tulipofika kule tukakuta ni yeye.

"Sisi hapa nyumbani huyo Ayubu tulikuwa hatumtambui kama alikuwa na uhusiano na Rafaela bali tulimjua rafiki yake mwingine wa kiume na ndiye alikuwa karibu naye kwani alishafika nyumbani mara kwa mara, " alisema Uisso.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa rafiki wa kike zinasema kuwa, Siku ya Pasaka akiwa na marehemu walikwenda kukutana na Ayubu ambapo walikaa naye kwa muda mrefu.
Akasema baadaye Ayubu alimpa marehemu shilingi 5,000 za sikukuu na kumwahidi kumuongezea nyingine kesho yake (Jumatatu).

Akasema, Jumatatu baada ya kuwasiliana kwa njia ya simu ya kiganjani, marehemu alikwenda tena kwa Ayubu lakini hakurudi wala kuonekana hadi ilipopatikana maiti yake.

Vyanzo vingine vya habari vinadai kuwa, kipindi cha nyuma Ayubu alikuwa akifika karibu na maeneo aliyokuwa akiishi Rafaela. Alikuwa akiwaambia watu kwamba marehemu alichukua shilingi 200,000 zake na simu ya mkononi. Alikuwa akitishia kumsomea Albadiri au kumfanyia jambo baya.

Mjumbe wa Nyumba Kumi wa eneo la tukio, Christian Michael aliliambia gazeti hili kuwa, alishuhudia mwili wa binti huyo ukiwa katika hali mbaya na baada ya muda ulichukuliwa na polisi.
Baadhi ya wananchi ambao wanaishi jirani na gesti yalikotokea mauaji hayo waliiomba serikali kutoruhusu nyumba za kulala wageni kuwa karibu na makazi ya watu kwa kuwa walevi wanapoingia humo na wapenzi wao, hupiga kelele na kubughudhi majirani hasa wenye watoto wadogo.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, David Misime alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo alikiri na akasema mtu mmoja ambaye hakupenda kumtaja jina ametiwa mbaroni kwa uchunguzi.
Matukio mbalimbali ya mauaji ya wanawake:

Februari 23 mwaka huu, Amina Ramadhan aliyekuwa mwanafunzi wa Ubungo Islamic High School aliuawa na mwanaume katika Gesti ya Mkombozi, iliyopo Mkwajuni, Kinondoni.

Machi 9 mwaka huu, Elizabeth Swai aliuawa Kawe, Gesti ya My Fair Club, chumba namba 310. Mwanaume aliyeingia naye hapo aliandika jina la Prosper Sichale katika kitabu cha wageni.
Machi 26 mwaka huu, Zubeda Rashid aliuawa katika Gesti ya Lil Wizo Rest, Mbezi ya Kimara, chumba namba mbili. Marehemu alisikika akipiga kelele kabla ya kukata roho.

Mlinzi alipokwenda alikuta ameshakufa huku akiwa na mwanaume aliyekuwa uchi aliyekwenda naye gesti hiyo ambaye alikamatwa na polisi walioongozwa na Mkuu wao, Mwita Mrefu. Mwanaume huyo alipohojiwa na polisi alisema anaitwa Prosper Simon lakini katika kitabu cha wageni aliandika Paschal Westo.

Aprili 23 mwaka huu, Asha Shamila, mkazi wa Vingunguti, Dar alikutwa amekufa katika Gesti ya Mkombozi, Buguruni kwa Mnyamani.

Machi, mwaka huu mwanamke mwingine ambaye jina lake halikutambulika, alikutwa ameuawa katika chumba namba 108, Gesti ya Four A iliyopo Tandika Transformer. Sehemu zake za siri zilikatwa.

Machi 2, mwaka huu, Hadija alikutwa amekufa katika Gesti ya Ngekewa, Tandika chumba namba sita.

Haijajulikana sababu za wanawake hao kuuawa na uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, vifo vyao vinahusishwa na mapenzi au mambo ya kishirikina.

Wiki iliyopita Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova aliitisha mkutano wa makamanda wote katika ‘zoni' yake ili kujadili suala hilo la mauji na aliwatahadharisha kuwa makini na mtandao wa wanaume wanaowarubuni wanawake kisha kuwaua.

Kwa picha nenda hapa

.........
....AND THE SERIAL KILLING CONTINUES!....

 
Hatimaye muuaji wa wanawake Dar akamatwa........

MTUHUMIWA WA MAUAJI..

Hivi karibuni umati wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ulifurika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kumshuhudia mtuhumiwa wa mauaji ya wanawake kwenye nyumba za kulala wageni, Protas Massawe aliyefikishwa mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi mkali.

Mtuhumiwa huyo alipandishwa mahakamani hapo Jumatano iliyopita na kusomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Flora Mushi.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, mshitakiwa Protas mnamo Machi 27 mwaka huu alikutwa ndani ya nyumba ya kulala wageni iitwayo Wazo iliyopo Mbezi Mwisho jijini Dar akiwa amemuua Zubeda Rashid.

Kutokana na uzito wa kesi hiyo, Hakimu Mushi alisema mshitakiwa hatakiwi kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kuendesha kesi hiyo ya mauaji na ikaelezwa kuwa, imeletwa kwa hatua za awali kabla ya kufikishwa Mahakama Kuu.
Kesi hiyo iliahirishwa na itatajwa tena leo mahakamani hapo na mshitakiwa alirudishwa rumande baada ya dhamana yake kufungwa.

Wakati mshitakiwa akitoka kizimbani, baadhi ya watu waliofurika mahakamani hapo kumshuhudia walipandwa na jazba na kutaka kumpiga, hali iliyosababisha askari waliokuwa wakimlinda kuwatuliza.
Askari wa Jeshi la Magereza walilazimika kuutawanya umati huo uliokuwa na jazba na kumuingiza mtuhumiwa kwenye karandinga lililokuwa chini ya ulinzi mkali.

Licha ya kukamatwa kwa mtu huyo polisi wanaendelea kufanya uchunguzi baada ya wimbi la wanawake kuuawa gesti kushamiri ambapo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, David Misime aliiambia Uwazi hivi karibuni kuwa, uchunguzi wao tayari umefikia hatua nzuri baada ya wanawake zaidi ya watano kuuawa katika eneo lake.
Misime alisema kuwa, wanawake wote waliouawa wanaonesha kuwa walivunjwa shingo kutokana na kukabwa baada ya kufanya nao mapenzi.

Kamanda huyo aliwataka wamiliki wa nyumba za kulala wageni kuwaandikisha wageni wao majina kamili, kuomba vitambulisho na hata kuomba hati zao za ndoa kabla ya kuwaruhusu kuingia vyumbani.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alisema mpaka sasa katika eneo lake kuna tukio moja la kuuawa kwa mwanamke katika nyumba ya kulala wageni ya Milambo, Vingunguti lililotokea Aprili 23, mwaka huu.

Kamanda Shilogile alisema mtuhumiwa wa mauaji hayo ni mwembamba mweusi ambaye anafanana pia na aliyeua wanawake wengine katika nyumba za kulala wageni wilayani Temeke. Alisema mpaka sasa mtuhumiwa huyo hajakamatwa, lakini upelelezi unaendelea na kwamba huenda wakamkamata hivi karibuni.

Chanzo: Global Publishers
 
Back
Top Bottom