Mwanaume mtaalamu jikoni

Kwa nini asiwe na hobby za kiume?
Huoni tatizo hapo?
Kesho akija kasuka tatu kichwa akwambia ni hobby utashangaa?(kwa mnaosuka ipotezeeni nimetoa tu mfano hapa)

A man is a man
a woman is a woman
japo tunajitahidi kuweka politics kulingana na tunayoyataka
lakini kila gender ina nafasi yake

Upishi ni hobby kama nyingine tu.
 
Kumbe reference point yako ni mijini
more than 80% ya watanzania wanaishi kijijini

mie reference point yangu ni Tanzania

eti baba anaenda chota maji kisimani, chochea kuni, bandika maharage, subiri hadi yaive, pepeta mchele, pembua, pika wali

duh, binti na mama yao wako wamekaa, siielewi.
wanaume wanaotetea hapa hawatumii kuni kongosho.........ila kila mwanaume lazima apike siku moja.
sidhani km kupika ni kuficha udhaifu ,,,,,,anyway hii kitu imekaa zaidi kwny mtazamo wa jamii na mtu binafsi.
 
Watu hujiuliza pale unapokua na mtu kwaajili ya kazi ya sekretari halafu unazifanya kazi kazi zote wewe halafu bado unamlipa sekretari!
 
Miimi huwa napika sana tu............. nakumbuka hata nilipokwenda ukweni kwa mara ya kwanza niliingia jikoni kupika, mama mkwe akamfokea mke wangu sana kwa kuniacha nipike, lakini nikafanikiwa kumtuliza na maisha yakaendelea......

Hahahahahaah naona ilikuwa varangati la kukata na shoka....kupika kwa Mwanaume hata siku moja hakuwezi kupunguza status yako kama Mwanaume mahali popote pale duniani, lakini ukiwa na mtu ambaye bado ameganda katika mawazo ya mwaka 47 basi inaweza kuwa kasheshe ya hali ya juu hata kusababisha mahusiano yafikie tamati. Hakuna mahali popote pale ilipoandikwa kwamba kupika ni majukumu ya mwanamke. Tamaduni hubadilika pia kutokana na wakati. Katika nchi nyingi za Afrika miaka kama 30 au hata zaidi iliyopita ilikuwa ni nadra sana kumkuta mwanamke engineer, pilot au doctor au anayeendesha gari leo wamejaa tele baada ya kuelewa kwamba hata mwanamama anaweza kabisa kuwa engineer, doctor au hata kuendesha gari au kuwa rubani wa ndege.
 
....aaaaahhhhh, kamanda huko mbona umeenda mbali bana,
hujawahi kula mahanjumati ya mzee Ali Mapilau nini wewe?

m3.jpg

hahaha naona hili picha mpaka mzee wenger mwenyewe kaja kukugongea like lol, uskute na yeye yupo kwenye hiyo food chain hapo anasubiria
 
mila zinatuharibu,mi kupika sijui na ni mvivu but sioni tatizo kwa wenzangu wanaojua na wenye kupenda kupika kufanya hivyo...ukiangalia hata the best chefs in the world are men

Mila zilizopitwa na wakati tuachane nazo lakini zile za kukataa ushoga pamoja na shinikizo la wakubwa akina 'Bama na 'Roun tuendelee kuzipinga kwa nguvu zetu zote.
 
Kusema kweli ni ujinga tu na kung'ang'ania yale ya 47.
Kuna rafiki yangu mmoja tulikutana masomoni, alikuwa mpishi
mzuri sana. Tulipomaliza kila mmoja akarudi kwao.
Yule jamaa akaoa, mwaka fulani nikaenda kumtembelea, wiki mbili.
Sikuona hata siku moja kuingia jikoni (na kwa kweli alivyokuwa anapika
mke wake havikuwa vitamu kama nilivyozowea kula vyake). Nilipomwuliza
kwa nini hapiki, aliniambia mwanzo alijaribu lakini ikwa ugomvi na mke wake
hataki kabisa akaribie jikoni. Sasa nahisi huu mgando wa mawazo kuwa
mwanamume na jiko ni kama paka na maji.
 
Watu hujiuliza pale unapokua na mtu kwaajili ya kazi ya sekretari halafu unazifanya kazi kazi zote wewe halafu bado unamlipa sekretari!
Ndio maana wengine hua mnao ili "mfuliwe". . . siuajiri mfanyakazi?
 
hahaha naona hili picha mpaka mzee wenger mwenyewe kaja kukugongea like lol, uskute na yeye yupo kwenye hiyo food chain hapo anasubiria

Ha ha ha, Mkuu hio picha lazima uipe like, umeona reli hio imekamilika alafu dogo kachuchumaa kabisa anaangalia treni kama inakuja ua vipi lol.

Mtaji wa ccm huo.
 
Unaishi mwenyewe weye?
Nije nikupikie?
Ndizi na samaki
na senene kidogo
bila sahau kabalagala na lubisi

kwetu uhayani mwanaume anayeishi mwenyewe anaitwa 'nyeite' meaning 'suicidal' kama mimi bishanga abashaija.
 
Kusema kweli ni ujinga tu na kung'ang'ania yale ya 47.
Kuna rafiki yangu mmoja tulikutana masomoni, alikuwa mpishi
mzuri sana. Tulipomaliza kila mmoja akarudi kwao.
Yule jamaa akaoa, mwaka fulani nikaenda kumtembelea, wiki mbili.
Sikuona hata siku moja kuingia jikoni (na kwa kweli alivyokuwa anapika
mke wake havikuwa vitamu kama nilivyozowea kula vyake). Nilipomwuliza
kwa nini hapiki, aliniambia mwanzo alijaribu lakini ikwa ugomvi na mke wake
hataki kabisa akaribie jikoni. Sasa nahisi huu mgando wa mawazo kuwa
mwanamume na jiko ni kama paka na maji.
Hehehehe,mama anaogopa kuambiwa "ahhh chakula cha leo mbona sio kizuri kama cha jana?" Kwahiyo ameona bora wazoee hicho hicho anachopika yeye.
 
Uanaume wa mtu hauna husiano wowote na kupika. Kama uanaume wa mtu ungekuwa unapunguzwa kwa kupika tusingekuwa na ma-chef wanaume kabisa.

Mwanamme kutopika imetokana na utamaduni wetu wa zamani kwamba mama zetu walikuwa hawafanyi kazi kwhaio walikuwa wanafanya kazi zote za ndani.

Mda umekwenda na maisha yamebadilika sasa; wakina mama nao wanafanya kazi nao na sio familia zote zinaweza kuwalipa wafanyakazi wa ndani.

Kwahio hakuna tatizo kama mwanaume kawahi kurudi nyumbani kabla mke
wake akaingia jikoni kutayarisha chakula. Mke akirudi nyumbani mnakula na mnakuwa mmeokoa mda ambao mngepoteza kumsubiri mama wa nyumba apike. Hapo mnakuwa mmepata mda mwingi wakutumia pamoja kujenga mapenzi yenu.

Kwahio Dada Lizzy mie sioni tatizo kuingia jikoni kabisa. Kama mke hafanyi kazi hilo mtu unaelewa lakini maisha ya sasa wote tunafanya kazi na ni vizuri kujaribu kugawana kazi za nyumbani kama hakuna mfanyakazi hili tupate mda mwingi wa kupumzika pamoja na kujenga uhusiano wetu.

Ahsante sana AW. Maneno mazito sana hayo.
 
baada ya muda si mrefu we will give in
kwani ni vitu vingapi tumevipokea?

Gender roles zipo tu
hata kama ni za 47 lakini zipo
sasa hivi kijana kusuka, toga maskio, zaa hereni, weka dawa kichwani, piga mkorogo jamii imeshanza kukubali

hata u.s.h.o.g.a tumeukubali japo tunashindwa kuukiri hadharani

Mila zilizopitwa na wakati tuachane nazo lakini zile za kukataa ushoga pamoja na shinikizo la wakubwa akina 'Bama na 'Roun tuendelee kuzipinga kwa nguvu zetu zote.
 
Ndio maana wengine hua mnao ili "mfuliwe". . . siuajiri mfanyakazi?

Tafsiri nzuri ya mke ni msaidizi,huwezi kutoka kwenye pilika umechoka halafu uje upike,na usiniambie na yeye alikua kwenye pilika kwani hilo sio jukumu la msaidizi,akishakuwa na pilika anakua sio msaidizi,ninapooa ninaoa coz nahitaji msaidizi na kupika ni moja ya majukumu yake!
 
baada ya muda si mrefu we will give in
kwani ni vitu vingapi tumevipokea?

Gender roles zipo tu
hata kama ni za 47 lakini zipo
sasa hivi kijana kusuka, toga maskio, zaa hereni, weka dawa kichwani, piga mkorogo jamii imeshanza kukubali

hata u.s.h.o.g.a tumeukubali japo tunashindwa kuukiri hadharani
Mada inahusu kupika, ushoga ni mjadala unajiotegemea.
 
Tafsiri nzuri ya mke ni msaidizi,huwezi kutoka kwenye pilika umechoka halafu uje upike,na usiniambie na yeye alikua kwenye pilika kwani hilo sio jukumu la msaidizi,akishakuwa na pilika anakua sio msaidizi,ninapooa ninaoa coz nahitaji msaidizi na kupika ni moja ya majukumu yake!
Kaaazi kweli kweli.
 
kuna wanawake mainginia pilot n.k
hata wasagaji nao wanaongezeka
ellen degenerate??alikuja na mkewe kwenye kipindi chake
anamhoji kuhusu maisha yake

baada ya muda si mrefu utakuta na tz tumefika huko
sababu tunajitahidi kuachana na ya 47
tunafuata ya kisasa kutoka magharibi

Ahsante sana AW. Maneno mazito sana hayo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom