The Finest
JF-Expert Member
- Jul 14, 2010
- 21,605
- 6,071
Kuna wanaume bila aibu huwa makuwadi na kukuwadia wapenzi wa rafiki zao/ndugu yake bila aibu wala hiana. Ni tofauti pale ambapo huyo mwanamke umemtamani mwenyewe na kujaribu bahati yako kwa njia ya usaliti kuliko ukuwadi. Kuna wengine ni makuwadi na hata hawajijui kuwa ni makuwadi kutokana na ukweli kwamba wameshazoea tabia hizo hadi wanaona ni kawaida kwa hilo jambo wanalofanya.
Mara nyingi hawa ni watu ambao hupewa au ununuliwa kwa vitu vidogo kama offer za bia na vihela vya hapa na pale hawa wanaume wa hivi hawana sifa alizotoa Asprin za kuwa Mwanaume Kamili.
Hata hivyo mwanaume anapomkuwadia mpenzi wa jamaa na hatimaye akafanikiwa kumuweka katika mstari na kutembea nae hapo kwa jamaa, nani alaumiwe zaidi? Yule kuwadi ambae wewe waona ni mtu wako wa karibu ila kakuzunguka ama yule mwanamke wako ambae anakubali kirahisi kabisa kuhamisha penzi hapo na kushawishika mara nyingi kutokana na pesa na kwenda kwa mwanaume huyo mpya?

Last edited by a moderator: