Mwanaume KAMILI

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,806
59,286
Mwanaume kamili ni yule anaejiamini. .
Anaelewa thamani ya mwanamke na kumthamini!

Mwanaume kamili ni yule anaefahamu majukumu yake. .
Aliye tayari kusaidia, bila kusubiri mpaka atake!

Mwanaume kamili ni yule anaejielewa. .
Anaerudi nyumbani bila ya kulewa!

Mwanaume kamili anajua muda wa kurudi nyumbani. .
Hasubiri mama na wana wakamtafute kilabuni!

Mwanaume kamili anajua anapohitajika. .
Hujitahidi 'kuwepo' hata akichoka!

Mwanaume kamili anatambua umuhimu wake katika malezi. .
Anajua kuzaa pekee hakumfanyi mzazi!

Mwanaume kamili anajitahidi kuwa mwaminifu. .
Na hamwachi mwenzie atoke bila kumsifu!

Mwanaume kamili hufikiri kabla ya kutenda. .
Hafanyi makusudi kuumiza anaowapenda!

Mwanaume kamili hutumia neno 'samahani'. .
Hana makuu na kujikweza asilani!

Mwanaume kamili hupendeka. .
Hufanya iwe rahisi kwa mwenzi kucheka!!

Hongereni "wanaume kamili" wote ndani ya JF na uraiani. Kwa niaba ya wote wanaowakubali TUNAWAPENDA SANA. . Y'all are deeply appreciated!
 
1. Umenena sawa ila mfano tukirudi wote mimi na wewe tumelewa hapo imekaaje nakuwa si mwaume kamili?
2. Na mwanaume anae kubonda mara kwa mara ukikosea huyo ni kamili, robo,au moja na nusu ?
 
mbona si jaona ukisema mwanaume libamia, mwanaume mwendo kasi......au sio uanaume huo...
 
Mwanaume kamili lazima awe na afya nzuri, kuhimili changamoto zinazo wakabili wanaume.
 
Safi sana LizzY..waache ..wanaume wajiulize wana-angukia wapi kwenye vigezo vya hapo juu. Na ukweli ubaki ndani ya mioyo yao!...
 
1. Umenena sawa ila mfano tukirudi wote mimi na wewe tumelewa hapo imekaaje nakuwa si mwaume kamili?
2. Na mwanaume anae kubonda mara kwa mara ukikosea huyo ni kamili, robo,au moja na nusu ?
1. Ukamili hauletwi kwa mashindano kati ya mume na mke.
2. Mwanaume suruali.
 
Hii nimeipenda kwa kweli, nimepata picha the type of mwanaume wapenda.... Ulie mdiscribe yupo Perfect, In reality ni ngumu saana kumpata but wenye bahati zao wanapata, na hopefully utawa mmoja wao.....

Kwa upande wangu Mwanaume kamili ni yule ambae ananielewa ipasavo na on top of that ananijali mno hata kama hajanipenda mno! akinielewa ipasavo atajua nini nataka, wakati gani nataka hicho kitu; Atanijua tabia zangu zoote, nikiwa sad/emotional/sensitive/happy/horny/depressed - na atatafuta njia mbadala wa kunifanya niwe normal. In short on one to one... Atanifanya nijiskie I am special and Woman indeed. Atakua baba mzuri wa watoto wangu na kutimiza wajibu wake kama baba na Mume. Ana Utu kwa wanadamu woote sio tu wakaribu wake.....

Mwanaume kamili huendana na mazingira yoote, hana mtindo wa kuuza sura, wakati wa kazi ni wakati wa kazi! Wakati wa kuuza sura ni wakati wa kuuza sura! He is at home anywhere... iwe shamba, iwe kazini (ofisini), iwe kijiweni, iwe kwa wakwe, iwe nyumbani kwake na hasa kila chumba (i.e jikoni), iwe mbele ya kundi kubwa, iwe mkutano, He rules..... either by being a low key player or high key player.... Awe anajua ana madhaifu na asiwe muoga wa kuonesha hayo madhaifu (walau kwangu kama mpenzi wake). Ajue kua yeye ni mwanadamu kama wengine, ili a-appriciate wanadamu wali mzunguka regardless hali zao...

Mwanaume kamili ni yule mwanaume hata his fellow men wish to be like him.....
 
2. Mwanaume kamili ni yule mwenye nyumba ndogo
3. Mwanaume kamili ni yule anayemzalisha mwanamke watoto zaidi ya watano
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom