Mwanaume anapokuwa Irresponsible, nini anategemea?

Vituka

JF-Expert Member
Nov 9, 2011
2,257
1,247
Habari wajameni.

Nina dadangu kaolewa na wana watoto 2, mumewe yuko kamili tu, I mean viungo vyake havina tatizo. Shule kasoma, sio sana lakini kutokusoma sio sababu ya haya afanyayo.

Kila siku yeye hana hela anampatia mkewe 10,000 kwa mwezi na kila siku anataka chakula. sister kipato chake kidogo sana, lakini yeye ndo anahudumia familia including huyo mume wake. Ajabu jamaa pombe hanywi wala sigara havuti ila kila siku hana hela na 10,000 kwa mwezi anatoa. Kila siku asubuhi anatokaga, hasemi wapi anaenda, ila jioni hurudi home na akiombwa hela yeote, iwe ya umeme, maji yeye hana. Sister mpole sana ila anaumia mno na kukoromeana nae hawezi. Last week \ mtoto wao kagundulika ana pumu, jamaa anadai hana hela, ivi ni kweli?

Kaniomba ushauri, nami naomba niwashirikishe humu jamvini mnishaurije?
 
Labda hana kazi, maana mwenyewe umesema hua anatoka na hajulikani aendapo.
 
Unachoshangaa ninii? jamaa kukosa hela au dadako kutake care?Mbona yote yanawezekana. Mtu yeyote anaweza kukosa hela na pia mme au mke anaweza tunza familia. Labda kama jamaa anfanya makusudi but kama hana hela kweli hamna mgogolo. Na nakushauri kuacha kufuatilia ndoa za watu kisa eti dada anapata shida. That is someone's wife.
 
hapo ndo unajua kuna wanaume na boys..
mpe pole your sister kwanza na pili,nimeona wanawake wengi tu ambao waume zao wako hivyo.1..let her stand on her feet and get the family moving kwa wachagga(achacharike)..asikae akisubiri mwanaume ampe pesa ya kila kitu.
Second option ni kuongea na mumewe vizuri ajue shida ipo wapi,ikishindikana the first option to be taken
Thirdly,aongee na wazazi wa mume na wake pia kuhusu hilo tatizo,ikishindikana,FIRST OPTION AGAIN.
 
wana watoto wawili probably wana more than four years kama mume na mke.hiyo tabia ameianza tu hapo kati au alikuwa ni kawaida yake toka mwanzo?ushauri wa haraka sister atafute hela popote ikibidi akope ili amtibishe mtoto,mengine watayasolve badae.
 
Sijafuatilia ndoa ya watu, Invarbrass, haiwezekani baba wa familia ukashindwa kuhudumia familia yako kisa huna hela!Mjini hapa kuna kazi kibao!Wanaume wanabeba zege wapate pesa kuhudumia familia zao, iwe yeye daily hana pesa! Mi naona anafanya makusudi coz sie ndugu zake tunamsaidia mara nyingi litokeapo tatizo! Sikatai kuna kusaidiana ktk familia but yeye ni too much!Anabadili pamba daily na akipita kitaa akasimuliwa kuwa ndo huyu asiye na hela kila siku huwezi amini!
 
hapo ndo unajua kuna wanaume na boys..
mpe pole your sister kwanza na pili,nimeona wanawake wengi tu ambao waume zao wako hivyo.1..let her stand on her feet and get the family moving kwa wachagga(achacharike)..asikae akisubiri mwanaume ampe pesa ya kila kitu.
Second option ni kuongea na mumewe vizuri ajue shida ipo wapi,ikishindikana the first option to be taken
Thirdly,aongee na wazazi wa mume na wake pia kuhusu hilo tatizo,ikishindikana,FIRST OPTION AGAIN.

Keshaongea na wazazi pande zote, na jamaa jibu lake lipopale pale, sina hela! Nadhani first option is better, ila sidhani kama ni sahihi amhuudumie na yeye! Nilitaka kumshauri kitu ila ngoja nisikilize ushauri wenu kwanza.

Asnte kwa ushauri mzuri
 
wana watoto wawili probably wana more than four years kama mume na mke.hiyo tabia ameianza tu hapo kati au alikuwa ni kawaida yake toka mwanzo?ushauri wa haraka sister atafute hela popote ikibidi akope ili amtibishe mtoto,mengine watayasolve badae.

Mwanzoni alikuwa mkoani akifanya biashara, so mara chache alikuwa anakuja na kuondoka. By the time sister alikuwa na kazi yenye kumpa kipato kizuri na alikuwa hamtegemei kwa chochote, but now kaacha ile kazi na jamaa ndo kaja anakaa nae. Kwa vile sie kwetu tuna umoja, tumemsaidia kumpeleka mtoto hospitali, kinachoboa ni kuwa baba wa mtoto anadai hana hela, na naha mpango wa kutafuta, to be honest sielewi!
 
Labda hana kazi, maana mwenyewe umesema hua anatoka na hajulikani aendapo.

Huko aendako hupata hela ya kununua pamba na mipafyumu, ila ya kuhudumia familia hana, huyu ni mume na baba kweli? Nijuavyo mimi baba kama hana hela huwa anakopa hata ka marafiki zake, hasa lijapo suala la ugonjwa, yeye anaona simple sana! mtoto anaumwa, mie sina hela, lol!
 
Kwa kweli hata huyo mke wake amefanya makosa kwa sababu haiwezekani tokea wamefunga ndoa hajui mume wake anafanya kazi gani wala analipwaje. Kutokana na hali hiyo mimi siwezi kutoa ushauri wowote
 
Mazungumzo ni muhimu sana
kabya kutoa ushauri huyo dada atafute pesa kokote amhudumie kwanza mtoto apone hilo kwa sasa ndio la muhimu maana ukisema uzidi kukaa mtoto anaumia.
Pili mazungumzo yafuate baada ya mtoto kupona
Mke na mume wake pamoja wazungumze kisa ni nini kwa nini kila siku mume anasema hana pesa
Na huko aendako anafanya nini cha kuzalisha au kujitafutia kazi
Isije ikawa anaenda tuu kukaa kijiweni wanapiga story na kucheza karata
Na hata hiyo elfu kumi ya kuacha kila mwisho wa mwezi anaipata wapi kama hana shughuli ya kumuongezea kipato maana sidhani kama anasaidiwa kila siku na marafiki.
Haya ni mambo ya mume na mke kukaa pamoja na kujadliana na kutafuta njia ya kuinua kipato cha familia maana hii ya kusema mume kila mara anasema hana pesa hiyo sio solution ya matatizo yatazidi kuongezeka
Na hapo ashapata watoto wawili wanahitaji malezi na matunzo na ada za shule na mambo mbalimbali katika ukuaji wao.
Kwangu mimi ushauri ni mazungumzo ya pamoja kati ya wanandoa yatasaidia kujua tatizo liko wapi.
 
Kwa kweli hata huyo mke wake amefanya makosa kwa sababu haiwezekani tokea wamefunga ndoa hajui mume wake anafanya kazi gani wala analipwaje. Kutokana na hali hiyo mimi siwezi kutoa ushauri wowote

Alikuwa anafanya biashara mkoani, na biashara anaijua ila mume alikuwa mgumu kusema kipato anachopata ktk biashara zake na kwa kuwa sister alikuwa na kipato kilichomtosha kulea watoto, hakuhangaika sana kujua kiasi gani anapata. Alipokuja mjini, alinunua bajaj na pikipiki kisiri siri bila mke kujua. Alijua baada ya mwaka baada ya kukuta documents za kununulia na alimwambia kuwa zimeharibika hazifanyi kazi. Kama alikuwa na uwezo wa kununua hivyo vitu, kweli anakosa hela ya kuhudumia familia?
 
Kwa kweli hata huyo mke wake amefanya makosa kwa sababu haiwezekani tokea wamefunga ndoa hajui mume wake anafanya kazi gani wala analipwaje. Kutokana na hali hiyo mimi siwezi kutoa ushauri wowote
Kaaazi kweli kweli.

Basi atakua anaishi kiuhalisia zaidi maana hapa JF tu ukisema unataka mwanaume anaejua na kutimiza majukumu yake kwa familia utaambiwa unataka mwanaume wa kufikirika a.k.a Malaika.

Mpe pole sana ndugu yako. Maadam amejua kwamba huyo mwanaume hana msaada kwake basi agangamale kulea watoto wake, atafute kazi itakayomuongezea kipato ili maisha yasonge.
 
Mtu irresponsible ni yule mwenye uwezo lakini kwa sababu azijuazo yeye mwenyewe hatimizi majukumu yake.
 
wasiombane hela wakati wa shida tu. Wapangiane utaratibu. Dada amjulishe mahitaji ya nyumbani ni yapi. Yeye anatoa shilingi ngapi - na yeye anatakiwa atoe shilingi ngapi.

Hapa, lazima aelewe pia, mume ametoka familia gani maana makuzi huchangia sana watu kufanya wendawazimu. Kama mzee wake ndivyo alikuwa anafanya ni vigumu kubadilika. Na pia kama mkewe, amekuwa anamudu bila yeye ni vigumu sasa kuonekana anahitajika.

Haya mambo sio yakushikiana mipini ni ya kufundishana zaidi - ingawaji mafunzo yanaweza yakawa ya gharama sana. Lakini ni muhimu yafanyike kama wanampango wa kuendelea kuwa pamoja. Nanyi ndugu, hiyo misaada yetu isiwe wazi hivyo - waachieni wapambanue yao - na dada afikie maamuzi yake. kwani kaumoja kenu kakizidi kanawezavuka mipaka ya ndoa
 
Jamaa atakuwa hana hela kweli,mnataka akaibe. Hivi huyo mwanamke nae ameolewa wala hajui mmewe anapiga mishemishe pande zipi! Khaa! Msaidie tu huyo dada yako, au na we huna hela?
 
A man who can't be a father to his own kids, is not a real man! Period
 
Back
Top Bottom