Delegate
JF-Expert Member
- Jan 4, 2012
- 331
- 201
Nimeona single mothers wakistruggle kulea watoto wao wa kiume peke yao bila baba za hao watoto kuwepo.
Je unaweza kumjua mwanaume aliyelelewa na mama peke yake? Je tabia zake zinakuwaje? Anaweza kuwa mwanaume halisi yaani roho ngumu?
Ninachojua watoto wa kiume wanatakiwa kuwa karibu na baba zao ili wakopy mambo kadhaa kwa baba zao. Je kwa aliyelelewa na pande zote mbili yaani baba na mama na aliyelelewa na mama peke yake wana tofauti???
Je unaweza kumjua mwanaume aliyelelewa na mama peke yake? Je tabia zake zinakuwaje? Anaweza kuwa mwanaume halisi yaani roho ngumu?
Ninachojua watoto wa kiume wanatakiwa kuwa karibu na baba zao ili wakopy mambo kadhaa kwa baba zao. Je kwa aliyelelewa na pande zote mbili yaani baba na mama na aliyelelewa na mama peke yake wana tofauti???
ndugu mtoa mada na kwa faida ya wanajamvi wengine, naomba niseme hivi.
Siku mtoto anazaliwa hachagui kuzaliwa kwenye aina yeyote ile ya maisha bali ni nature ina mchagulia so hana makosa hata kidogo kwa maisha atakayojikuta amezaliwa/amelelewa iwe ni single or awe na wazazi wote. kosa kubwa hapa naliona kwa sisi wazazi wenyewe ingawa muda mwingine mtu unaweza kukosa jinsi basi inabidi ukubaliane na hali halisi ya kuwa mzazi pekee. kwangu mimi kuwa na wazazi wote au mmoja haina mashiko sana iwapo tu mtoto huska atajitambua basi.
sipendi kuongelea sana jinsia za hawa watoto kwa kuzitengenisha bali nitaziongelea kiujumla wake.
mzazi wa kike anapolea watoto peke yake anaweza kupata matokeo mawili kwamba ama awalee vizuri na watoto atoke wakiwa watu wazuri kwenye jamii ama walee kimayai watoto watoke wakiwa sio watu wema kwenye jamii.
Mimi ni mama ila kuna jambo ambalo huwa linaniumiza sana juu ya jinsi tunavyolea watoto mara nyingi.
Iwapo umejikuta unalea mtoto peke yako kwanza jua kabisa kuwa maisha hayanaga upendeleo hata siku moja so kuwa mzazi pekee isiwe ni sababu ya kumlea mtoto kimayai. Jua kuwa hakuna excuse anazopewa mtoto kwa kuwa alilelewa na mzazi mmoja hata siku moja siku zote maisha yanatoa vitu vyote kwa binadamu wote ila uwezo na uwajibikaji wako ndio unaokufanya upate baadhi na vingine ukose. sijawah kuona eti labda gari limetengenezwa kwamba hili liendeshwe na walio lelewa na mama pekee au baba pekee. vyote hutoka kwa ajili ya wote na juhudi zako binafsi na uwezo ndivyo vitakavyo kupatia.
Akin mama wengi huwa tunafika mahali tunayasahau haya huku tukijua kuwa maisha hayanaga upendeleo kwa yyte yule. watoto wengi wanaolelewa na baba huwa wanaish kigumu naweza sema na mwishowe wanakuwa very prosperous ingawa siyo wote ila hii ni kwasababu baba siku zote maisha anavyomlea nayo mtoto ni ya kumuwajibisha na kumuonyesha sura halis ya maisha tofauti na sisi akina mama ambao siku zote hupenda kumuonyesha mtoto sura nzuri tu ya maisha na kusahau upande wa pili.
wamama wachache sana waliweza kumudu maisha ya kulea watoto peke yao wakawa prosperious kama aliyetuonyesha Mtambuzi na huyu ilitokana na ukweli kuwa mama yake alimuonyesha mwanae sura ya pili ya maisha kuwa kuna juhudi binafsi na wewe kulelewa bila baba haikupi excuse ya kutokuwajibika. alimnyima mwanae kuangalia TV na kumpa homework nyingi ili kumjengea dhana ya uwajibikaji na hii ilimtoa huyu mtoto. binafsi nimependezwa sana na aina ya mama kama huyu ambaye kwake yeye maisha yako fair kwa kila mtu, ila uwajibikajai tu ndio unoleta tofauti.