Mwanaume Abakwa na Wanawake 10

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
Mwanaume Abakwa na Wanawake 10

Kijana mwenye umri wa miaka 17 wa nchini Papua New Guinea amelazwa hospitali akipatiwa matibabu baada ya kubakwa genge la wahuni wanawake wapatao 10.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa Southern Highland, nchini Papua New Guinea, Teddy Tei, kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 alikumbana na zahama hilo siku ya ijumaa wakati alipovamiwa na kundi la wahuni wanawake wapatao 10.

Wanawake hao wakiwa na visu walimshambulia kijana huyo kabla ya kupokezana kumbaka kwa zamu.

"Hii ni kesi tunayoifualia kwa ukaribu zaidi, tunawatafuta wanawake waliofanya unyama huu", alisema kamanda huyo wa polisi.

Taarifa ya polisi ilisema kwamba wanawake 10 wakiwa na visu walimshambulia kijana huyo na wanawake wanne kati yao walimuingilia kinguvu kijana huyo.

Kamanda Tei aliongeza kuwa kijana huyo aliwahishwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Kijana huyo ambaye jina lake limewekwa kapuni, anafanyiwa uchunguzi ili kujua kama ameambukizwa magonjwa ya zinaa au la.

"Ugonjwa wa ukimwi ni tatizo kubwa hapa Papua New Guinea, ninahofia huenda baadhi ya wanawake waliombaka huenda wakawa ni waathirika", alisema Kamanda Tei na kuongeza.

"Nimekuwa nikiwaonya wanawake wawe waangalifu sasa inanibidi nianze kuwaonya na wanaume nao wawe waangalifu mitaani".

Yawezekana habari hii ni ya zamani, lakini ni bora kukumbushana na kuwataadharisha Vijana wetu wa Kiume nao wawe na taadhari, yasije yakawakuta yalio mkuta mwenzao!
 
Hii imekaa ki-april fools day. Unless walimfanyizia kinyume kutumia vifaa vilivyomuumiza hadi kupelekwa hospitali.
 
ni kipi hasa kilichopelekea kulazwa hospitalini!?kubakwa au maumivu ya kushambuliwa?!maanake kama ni kubakwa sidhani kama aliumia kihivyo,watu wenyewe wanne tu!!!
 
Duh huyu kijana kifaru,watu kumi?watu mmoja tu hawamuwezi,ila aombee wasiwe na ngoma yani atakuwa amechota strain za virus za aina zote
 
Sipati Picha au walimnywesha dawa ya kuhakikisha bendera haishuki mlingoti? Kama wote waliingia basi alitaka mwenyewe kwani nijuavyo ukiwa katika tukio la mtafaruku huyu jamaa yetu hujificha kabisa huwa hapendi taabu..
 
Mwanaume Abakwa na Wanawake 10

Kijana mwenye umri wa miaka 17 wa nchini Papua New Guinea amelazwa hospitali akipatiwa matibabu baada ya kubakwa genge la wahuni wanawake wapatao 10.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa Southern Highland, nchini Papua New Guinea, Teddy Tei, kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 alikumbana na zahama hilo siku ya ijumaa wakati alipovamiwa na kundi la wahuni wanawake wapatao 10.

Wanawake hao wakiwa na visu walimshambulia kijana huyo kabla ya kupokezana kumbaka kwa zamu.

"Hii ni kesi tunayoifualia kwa ukaribu zaidi, tunawatafuta wanawake waliofanya unyama huu", alisema kamanda huyo wa polisi.

Taarifa ya polisi ilisema kwamba wanawake 10 wakiwa na visu walimshambulia kijana huyo na wanawake wanne kati yao walimuingilia kinguvu kijana huyo.

Kamanda Tei aliongeza kuwa kijana huyo aliwahishwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Kijana huyo ambaye jina lake limewekwa kapuni, anafanyiwa uchunguzi ili kujua kama ameambukizwa magonjwa ya zinaa au la.

"Ugonjwa wa ukimwi ni tatizo kubwa hapa Papua New Guinea, ninahofia huenda baadhi ya wanawake waliombaka huenda wakawa ni waathirika", alisema Kamanda Tei na kuongeza.

"Nimekuwa nikiwaonya wanawake wawe waangalifu sasa inanibidi nianze kuwaonya na wanaume nao wawe waangalifu mitaani".

Yawezekana habari hii ni ya zamani, lakini ni bora kukumbushana na kuwataadharisha Vijana wetu wa Kiume nao wawe na taadhari, yasije yakawakuta yalio mkuta mwenzao!
Makala ya msingi inaeleza hao wamama walikuwa na visu, hivyo yaweza ikawa amelazwa tokana na majeraha ya visu ati

Back
Top Bottom