Mwanasheria wa Halmashauri ya Korogwe ana 'Digrii ya chupi' - DC Mrisho Gambo

Status
Not open for further replies.
Siku zote ukiwa unataka watu wajue kuwa wewe unafanya kazi na wenzako hawafanyi matokeo yake ndiyo haya ya kutumia lugha ambayo mwisho wa siku utajutia tu!
 
Mkuu wa wilaya korogwe ndugu Mrisho Gambo amemwambia mwanasheria wa wilaya hii kuwa ana degree ya
chupi kufuatia majibu ya mwanasheria huyo dhidi ya kesi kati ya wafanyabiashara na halmashaur.
Mwanasheria huyo alishindwa kutoa maelezo ya kina juu ya sakata hilo ndipo dc akaamua amchane ......, source: mwananchi
Wakuu wa mikoa na wa wilaya wanatekeleza ilani ya chama alishasema Mtoto wa Mkulima.
 

Kufuatia habari iliyochapishwa katika Gazeti la Majira la tarehe 29-08-2012, na mwandishi, Yusuph Mussa, Korogwe, DC wa Korogwe aliyetamka maneno hayo ataburutwa kortini. Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, Bwana Mrisho Gumbo, anatarajiwa kufikishwa kizimbani wakati wowote kwa madai ya
kumdhalilisha Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bi Najum Tekka.

Bi Tekka alifikia uamuzi huo baada ya Bwana Gambo kumwambia Shahada yake ni ya nguo za ndani pamoja na kumuweka chini ya ulinzi wa polisi ili ahojiwe bila kujua kosa lake. Akizungumza na gazeti la MAJIRA jana, Bi Tekka alisema kutokana na udhalilishaji huo, anatarajia kufungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda
ya Tanga na kudaia fidia ya Sh 90 milioni.

Alisema Juni 14 mwaka huu Bwana Gambo alimwita kwenye kikao cha kamati ya Ulinzi na Usalama cha Wilaya, ambacho kilifanyika ofisini kwake ambapo kikao hicho, pia kilihudhuriwa na baadhi ya Madiwani pamoja na viongozi wa soko la Manundu Mjini Korogwe. Sababu ya kuitisha kikao hicho ilikuwa ni kutafuta muafaka kwa njia ya mazungumzo ili kama tutakukubaliana na wafanyabiashara wa soko la hili ambao wanapinga ongezeko la kodi ya vibanda kutoka 2,000/= kwa mwezi hadi 20,000/= kwa mwezi ifutwe.

"Majibu yangu katika kikao hiki ndiyo yalimfanya Bwana Gambo kunidhalilisha kwani mimi kama mwanasheria sina uwezo wa kuzungumza kesi ambayo ipo mahakamani," alisema Bi Tekka.

Alisema baada ya kuzungumza maneno hayo Bwana Gambo alianza kusema, "Huyu Mwanasheria Digrii yake ni ya Chupi, sina imani naye kabisa, kesi zote za halmashauri anazisababisha yeye, hana msaada wowote
kwetu."

"Kimsingi amenidhalilisha mimi mwenyewe pamoja na taaluma yangu kwa maneno aliyoyatumia, pia amenidhalilisha kwa kuniweka chini ya ulinzi wa polisi ili nihojiwe wakati kosa langu mimi silijui hata mahakamani sijapelekwa" alisema Bi. Tekka.

Bi Tekka alisema pamoja na kumpa bwana Gambo siku 14 awe amefuta kauli yake kwa kuitisha kikao kama alichokiitisha awali bado alipuuza, mbali na kushauriwa na wakuu wenzake wa wilaya. "Nafungua kesi Kesho (jana) Mahakama Kuu kanda ya Tanga, ili aweze kunilipa Milioni 90 kwa kunidhalilisha" alisema

Bwana Gambo alipofuatwa na MAJIRA alikiri kumualika Bi. Tekka kwenye kikao hicho ili aweze kutoa ufafanuzi kwanini wameshindwa kufikia muafaka na wafanyabiashara. "Kabla ya hapo mimi niliwaita wafanyabiashara wakakubali kwenda kufuta kesi, lakini huyu mwanasheria sijui ana maslahi gani na kesi hii,
tulishafikia mwafaka na waende mahakamani kuifuta lakini walipofika akawakimbia.

Hadi sasa kesi haijafutwa lakini wafanyabiashara
wamekubali kulipa sh. 10,000/= badala ya sh.20,000/=, kweli aliandika notice ya kuomba radhi kwa kumdhalilisha lakini nilimwambia aende mahakamani hata leo, tutakwenda kupambana " alisema Gambo.

Bwana Gambo alipongeza kuwa, kama Bi.Tekka anadai alidhalilishwa, mbona hakuandika madai hayo polisi badala yake anakaa na watu wake na kudai amedhalilishwa?


Prosper R Mushi
 

Tatizo la KUCHAGUA Marafiki ya Watoto Wake... DC ni IT Specialist... LINI SIASA ya U-DC?
 
mi nashangaa watu wanashindwa kujadili kama kweli degree ya huyo mama ni ya chupi au la..wao wanaleta ufuasi wa siasa..hizo degree zipo nyingi sana na ndo zinazoleta matatizo kwenye jamii.unaona mtu msomi lakini maamuzi yake hayaendani na cheti chake,tukijadili vizuri hiyo mada tutapata mengi kuliko kuhamishia lawama kwa DC.

Sijui kama unaelewa hoja inayojadiliwa hapa! Kama unataka tujadili degree za chupi anzisha uzi wako.
 
Huyu jamaa ni bonge la gebwe kama prince aliemsaidia kupata udc huo,yani hii nchi walai 2015 ni mbali sana,we need to take action kama wamisri na tunisia.
 
atakuwa anamfahamu, hawezi kusema tu hivyo. labda alipokuwa chuo alikuwa akiuoan akigawa uroda kwa lecturer ili afaulo.. ndio maana utendaji mbovu... hahaha
 
Huenda walisoma wote, hivyo anajua alivyokuwa akipata alama zake kwa njia hiyo ya chupi, ingekuwa serikari makini siyo dhaifu, huyu hakutakiwa kuwa DC hadi muda huu, angekua kishaachishwa na yuko mahakamani kujibu kesi ya kudhalilisha.
gambo kasoma Uhasibu Arusha ambako hakuna kozi ya sheria
 
Tatizo la watanzania ni kupima umakini wa mtu kwa maneno anayoongea au porojo badala ya actions za mtu. Mtu aliye makini hawezi kufanya udhalilishaji wa kijinsia kama huo

Nakubaliana na wewe,mtu makini na mweledi hawezi tamka maneno ya udhalilishaji wa jinsia,ingekua hata enzi ya Uongozi wa Mwalimu Nyerere,huyo DC angekwisha tupiwa virago!
 
Hivi vijana wa CCM wote ni wazuri sana kwa matusi? Huyu mkuu wa wilaya si ni yule aliyewahikuwa na mvutano na UVCCM mkoani Arusha na wakatangaza kumvua uanachama? Kama ni yeye wote wanaonekana ni wazuri kwa matusi. Rejea kauli za akina Rusinde kwenye kampeni na hata kwenye vikao vyao. Kauli za akina Nape kule Mwanza Kirumba. Kauli ya hivi karibuni ya Shigela na nyingine nyingi.
Lakini kubwa kwangu ni vijana kukosa maadili na kuwa na tabia za ajabu kama hizi a kuwakosea wazee. Hiyo sentensi alitamka kikaoni kukiwa na watu wa aina gani? Vijana mnapopewa uongozi msituangushe.
 
Yawezekana alisoma nae na aliona alivyokuwa akigawa uloda kwa malecturer, UDSM mbona ndo mchezo? maana personally nawajua madada walokuwa wakija na maswali tnayasolve na next day yanaappear kt exam, atatoa ushaid na mtashika midomo kwa aibu

Heeh! kumbe wenye degree za chupi wengi.

Mantiki ni rahisi tu hapa. Ukipokea maswali ya mitihani kwa mtindo wa kichupichupi ukayafanya kabla ya mitihani kisha ukafaulu mitihani yenyewe basi hata wewe unakuwa umepata degree ya chupi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom