Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hataki Katiba Mpya

Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
17,276
17,983
Taarifa za vyombo vya habari leo ni kwamba Werema hataki katiba mpya. Anazungumzia kuweka viraka wakati wanasheria wenzake wanasema viraka vimefika mwisho.
Ukifuatilia mabadiliko ya katiba yaliyofanyika Kenya utajua kwa nini hataki katiba mpya. Moja ya mambo yalibadilisha na ambayo pia Tanzania tunayataka ni kupunguza madaraka ya Rais. Katiba mpya ya Kenya imeweka utaratibu wa kuwapata watu kama Jaji mkuu, Mkuu wa majeshi, mwanasheria mkuu wa serikali nk. Na inabidi hawa waliopo madarakani waondoke ili utaratibu mpya wa kuwapata utumike. Wao wamefanya hata kwa majaji wa mahakama ya rufaa. Inabidi waombo kazi upya kwa muundo mpya.
Werema anaelewa fika kuwa hilo linakuja Tanzania na huenda ana wasiwasi na sifa zake kuwa mwanasheria mkuu wa serikali. Kwenye utaratibu wa wazi wa kuzingatia sifa wengi wa wateule wa jamaa wasingeliona jua.
 
Werema hawezi kukubali bila msukumo wa umma kama alivyofanya mnyika, werema ameshachuakua chake mapema na ana kazi alyokabidhiwa kulinda sirikali zilizofichwa ukisema katiba mpya kuna watu wanapata pressure yeye ni mmoja wapo, utasikia wanakwambia wananchi , wnanchi gani hao tofauti na waliokwisha kuongea?? Maaskofu wanataka katiba mpya, cwt wanataka katiba mpya, waislamu wanataka katiba mpya, tucta/wafanyakazi wataka katiba mpya, wanazuoni wanataka katiba mpya, wanasheria na wanaharakati mbalimbali wanataka katiba mpya, jaji samata, jaji warioba, jaji kisanga, jaji manento, jaji ramadhani wanataka katiba mpya , media wanataka katiba mpya, yeye ag ni nani hasa kuzuia katiba mpya na kwa malsahi ya nani hasa??? Anaogopa nini kuandikwa katiba mpya????? Je hofu hii inatoka wapi???
 
Who is werema to take this country to hell? Ukisema katiba mpya kuna watu wanapata pressure yeye ni mmoja wapo, utasikia wanakwambia wananchi , wananchi gani hao tofauti na waliokwisha kuongea?? Maaskofu wanataka katiba mpya, cwt wanataka katiba mpya, waislamu wanataka katiba mpya, tucta/wafanyakazi wataka katiba mpya, wanazuoni wanataka katiba mpya, wanasheria na wanaharakati mbalimbali wanataka katiba mpya, jaji samata, jaji warioba, jaji kisanga, jaji manento, jaji bomani,jaji ramadhani wanataka katiba mpya , media wanataka katiba mpya,chadema, cuf, nccr,tlp, udp wote wanataka katiba mpya, yeye ag ni nani hasa kuzuia katiba mpya na kwa malsahi ya nani hasa??? Anaogopa nini kuandikwa katiba mpya????? Je hofu hii inatoka wapi???
 
Taarifa za vyombo vya habari leo ni kwamba Werema hataki katiba mpya. Anazungumzia kuweka viraka wakati wanasheria wenzake wanasema viraka vimefika mwisho.
Ukifuatilia mabadiliko ya katiba yaliyofanyika Kenya utajua kwa nini hataki katiba mpya. Moja ya mambo yalibadilisha na ambayo pia Tanzania tunayataka ni kupunguza madaraka ya Rais. Katiba mpya ya Kenya imeweka utaratibu wa kuwapata watu kama Jaji mkuu, Mkuu wa majeshi, mwanasheria mkuu wa serikali nk. Na inabidi hawa waliopo madarakani waondoke ili utaratibu mpya wa kuwapata utumike. Wao wamefanya hata kwa majaji wa mahakama ya rufaa. Inabidi waombo kazi upya kwa muundo mpya.
Werema anaelewa fika kuwa hilo linakuja Tanzania na huenda ana wasiwasi na sifa zake kuwa mwanasheria mkuu wa serikali. Kwenye utaratibu wa wazi wa kuzingatia sifa wengi wa wateule wa jamaa wasingeliona jua.

Ninasikitika kusema kwamba Werema amekuwa ni kiongozi mkubwa waserikali anayetokea mkoani kwangu ambaye nasikitika kumuita mpuuzi. Yani wananchi kila kada wanazungumzia umuhimu wa kuwa na katiba mpya lakini yeye anazungumzia kuweka viraka. Jana nilipokuwa namsikiliza anasema watu wanaodai katiba mpya watoe madai yao bila kutishana nikashindwa kumuelewa kabisa. Yani wananchi tutake katiba yetu kwa kumbembeleza? Unajua mtu akipata madraka makubwa ambayo hakuyatarajia na pengine hakuwa na uwezo au upeo na vigezo vya kushika madaraka hayo anakuwa kama amepagawa hivi. Hata hivyo kwa upande mwingine siwezi kumshangaa, niliwahi kukutana nae mara kadhaa kwenye vikao vya bodi ya taasisi moja ya elimu ya juu, akitakiwa kutoa ufafaunizi masuala fulani fulani ya kisheriani anakuwa mtu fulani hivi mbabe mbabe.
 
Hii imekaaje, hebu tuijadili katika mtazamo huu. Waziri Mkuu amesema atapeleka mapendekezo kwa Raisiya kuwa na katiba mpya. At the same time AG ambaye ni mshauri mkuu wa serikali ( pamoja na PM) anaropoka kuwa katiba sanasana itarekebishwa haitabadilishwa.

Kwa kifupi hapa ni kuwa AG anapingana na PM kwenye issue ambayo PM keshaitolea msimamo in public.

Kiutendaji hii imekaaje, sio sababu ya mmoja kati yao kijiuzulu na au mwingine kufukuzwa kazi? Waziri mkuu, kujiuzulu, kwa kudharauliwa au AG, kufukuzwa kazi, kwa kumdharau PM
 
Huyu AG ni muumini mzuri sana wa dini inaitwa mafisadi na walafi wa ccm, nani hajui harakati zake alizozifanya kipindi cha uchaguzi cha kuitetea ccm dhidi ya upinzani na kutishia kushitaki upinzani as if yeye ni mwanasheria au meneja kampeni wa CCM
hana jipya huyu na anastahili kuangaliwa kwa umakini kwani kawekwa hapo kwa maslahi ya mabwana zake. "mbwa hawezi kumg'ata bwana wake labda apandwe na kichaa." tusitarajie jipya kwa huyu kibaraka, tukomae kudai katiba mpya itakayo tukomboa sisi na watoto wetu toka kwa huu modern pololitical colonialilsm unaondeshwa na kushabikiwa na ccm.
 
Lakini alisema, kwa mtizamo wangu, jamani si kila mtu ana nafasi ya kutoa maoni yake? Mimi binafsi naunga mköno undwaji wa katiba mpya, na yeye kasema anadhani katib mpya kwa sasa haihitajiki, nakumbuka jaji mstafu Aliwahi kuchomekewa na waandishi wa habr siku ile walipotoa hukumu ya mgombea binafsi, akasema nadhani katib mpya kwa sasa haihitajiki, leo anatumbia ni muhimu, haya ni mawazo ya watu, yasituyumbishe, tusipoteze wakati kuyajadili.
 
Huyu AG ni muumini mzuri sana wa dini inaitwa mafisadi na walafi wa ccm, nani hajui harakati zake alizozifanya kipindi cha uchaguzi cha kuitetea ccm dhidi ya upinzani na kutishia kushitaki upinzani as if yeye ni mwanasheria au meneja kampeni wa CCM
hana jipya huyu na anastahili kuangaliwa kwa umakini kwani kawekwa hapo kwa maslahi ya mabwana zake. "mbwa hawezi kumg'ata bwana wake labda apandwe na kichaa." tusitarajie jipya kwa huyu kibaraka, tukomae kudai katiba mpya itakayo tukomboa sisi na watoto wetu toka kwa huu modern pololitical colonialilsm unaondeshwa na kushabikiwa na ccm.

PM is harmless, stick to what Werema said ok!
 
Werema ni kiazi hakuna mfano, anafaa kutupiwa mayai viza kila anapotoka nyumbani kwake.
 
Back
Top Bottom