Mwanasheria mkuu ampinga Dk Hoseah

Hosea ni mnafiki na muongo mwenye lengo la kujitafutia cheap popularity. Kwa mwanasheria wa kiwango chake, anapaswa kujua nini maana ya separation of powers and duties. Pia sio kweli kwamba sheria inamruhusu kuprosecute makosa madogo tu bila ya kibali cha dpp. Kwani wajibu huo ni kwa makosa yote. Naanza kuhic kuwa naye kaingia kwenye ukanda na kama sio udino.
 
Kama Hosea ni mwanasheria kama alivyo werema, na wote wameisoma sheria ya kuanzishwa kwa TAKUKURU na wana maoni yanayotofautiana, hii bila shaka inatosha kuashiria kuwa sheria husika ina utata. Bila shaka anaependekeza ipitiwe upya atakuwa na point
 
huyu si ndio alisema katiba ya jamhuri iko vizuri kabisa haiitaji kutengezwa upya.? Nchi ya vituko,rais kituko,pm kituko,madam spika kituko,AG kituko.!!

Idawa
You are quite right . Werema is a disaster yeye na Yule mama Celina Kombaini walisema Katiba iliyopo inatosheleza but Dhaifu begged to differ and decided to go ahead with tume fake ya kukusanya maoni in a sexed manner. This is comedy in acttion ambayo Werema hajui now I don't know why is he still the AG? He is a very myopic Judge who can only see in one colour which is green. Hatujawahi kuwa na Mkuria type hii he keeps on hopping just like a kangaroo . Feleshi the DPP is another disaster hata huyo Hosea nasikia they are related in a syndicate from Mwanyika and Chenge make no mistake about that. Why do you need DPP's consent kwa Kesi kama ya Rada?
 
Bado iko njia mbadala, tunamuomba Mh. Lissu aandae hoja juu ya marekebisho ya sheria hii, ambamo ataelezea upungufu na vikwazo ambavyo inakuwa rahisi kumhukumu mwizi wa kuku na kushindwa kumhukumu mwizi wa EPA wakati ushahidi upo lakini mkulu anawasamehe na kusema tukiwahukumu tutayumbisha uchumi (what a nonsence!)

Inawezekana, kwa serikali ambayo kazi yake ni kupinga kila kitu, lakini angalau wengi wananchi wa kawaida watapata mwanga zaidi juu ya udhaifu wa serikali na kuwaach¡a wao kuwahukumu kidemokrasia visandukuni.
 
Mkuu hapa huelewi nini rushwa kubwa ni ile ambayo GAMBAZ wakikamatwa nayo, hapo consent ya DPP ni lazima. Lakini mimi na wewe tukikamatwa ni rushwa ndogo, HAPA HATUHITAJI CONSENT YA DPP
Off cause hiyo Rushwa kubwa ina MGAWO {Inazalisha mifereji hadi kwa DPP} Hapa inabidi aulizwe kama hakupata basi [LNL]
Na ile Rushwa Ndogo haina MGAWO {Ya walala hoi na wenye mabawa tofauti na wao (ANT SYSTEM) katika kuliibia taifa}
 
Ama kwa hakika hapa wamethibitisha kuwa maneno ya Mh. Tundu Lisu kuhusu uteuzi katika hii idara ya sheria ni tope tupu.

Sasa ina maana Werema uelewa wake wa maana ya kuwepo TAKUKURU ni kushindwa kuchukua hatua baada ya uchunguzi kufanyika na kubainka kuwepo rushwa tena kubwa? Na je hizo checks and balance, ni kwa rushwa ndogo ndogo tu ndiko zinatumika? Na kama tunafuata sheria hiyo hiyo moja nchi nzima iweje mwanasheria wa TAKUKURU ashindwe kabisa kufungua kesi hata moja kubwa tangu kuanzishwa kitengo hicho?? Wakati huo huo habari zinaanza kuvuja kuwa wapo watu wana mabilioni yamefichwa Uswisi? Yamefika je kule kama siyo rushwa hizo?
Dalili zote za rushwa kubwa zipo wazi kabisa, Waziri wa nchi anapokumbwa na shutuma za kupewa rushwa ya Dola milioni halafu akadiriki kuziita fedha hizo kwa kejeli kuwa ni vijisenti, je hiyo inaashiria nini kama si kuwa anafahamu waliopata zaidi sana kuliko yeye ndiyo kupelekea zake kuziita vijisenti?

Werema anajua anachokitetea na anajua anafanya kazi aliyoombwa aifanye, kulinda na kunyamzisha watu wasiendelee kuhoji. Alichoahidiwa anakijua mwenyewe.

Hosea anasikitisha sana kwa sababu kama tangu ameanza kuiongoza taasisi hii hajaweza ku-achieve kitu chochote cha maana na leo hii anakataliwa wazi wazi na AG pamoja na DPP na zaidi ya hapo anabezwa kwa madharau kiasi hicho, kwanini hajiuzulu? Wananchi watakapokuja kuujua ukweli kuwa hizo rushwa kweli zilikuwepo na alizijua vizuri undani wake ila alibakia kupiga piga kelele tu bila kuchukua hatua stahili anadhani kikauli chake dhaifu kitamtoa kitanzini? La hasha! He better come out and take action now!

AG na DPP wanadharau umma mzima wa watanzania, kuwa labda hawaelewi wala kuona. Lakini wanjidanganya. Kama kweli mafaili yaliyopelekwa kwa DPP yana mapungufu kitaalamu, je ni hatua gani wamechukua kuwaelewesha na kuwasaidia TAKUKURU ili waboreshe kazi zao?? Ushauri gani wametoa kwa TAKUKURU? Au wamekalia tu mafaili ili watu wasahau? kama kawaida ya serikali yetu kukalia hata ripoti za tume ilizoziunda yenyewe bila maelezo yoyote kwa walipa kodi?

Hapa kuna uzembe wa hali ya juu ambao hautaisaidia nchi kusonga mbele hata kidogo.

Mungu ibariki TANZANIA.
 
Werema amenyoosha maelezo, though inaweza kuonekana anawakingia kifua lakini ukweli unabaki palepale, haiwezekani ukatuhumu, ukapeleleza na kushtaki bila mtu mwingine kucheki kama ni majungu, visasi au kweli kuna kosa in terms of ushahidi, haiwezekani.

Jiulize hao Pccb wanaong'ang'ania kufutwa kipengele cha conset ya Dpp wameshinda kesi ngapi? ukicompare na walizoshindwa? na zile za disign ya Liyumba? Sometimes watu tunakuwa mashabiki zaidi.

Sheria iko poa tatizo labda ni dhamira tu, Hosea aache visingizio na siku zote serikali huwa ina kauli moja na msimamo 1

Mjenda Chilo naomba kukuuliza dhana nzima ya "Checks and Balance" unaijua???labda ngoja nikujuze...katika Legal context "Checks and Balance" ni kwa mihimili 3 ya dola (Bunge, Mahakama na Executive) kuangaliana mmojawapo usionekane una nguvu kuliko mwingine. Sasa DPP na TAKUKURU ni vyombo ambavyo vyote vipo chini ya mhimili wa "Executive" unataka kutuambia "Checks and Balance" hata kwa watoto mliozaliwa tumbo moja???Haiwezekani...halafu inaonekana wewe sio mtu wa "kuperuzi na kudadisi" mambo currently yanayoendelea...nashauri ukitaka kuona TAKUKURU wameshinda kesi ngapi na kushindwa ngapi tembelea website yao wameweka midata yao kibao mle...halafu nionavyo wewe dizaini ndio mshabiki hapa...weka hoja ya maana!!!
 
Back
Top Bottom