Mwanasheria atekwa, apigwa, aachwa porini

Status
Not open for further replies.
Hii habari iko kwenye gazeti gani zaidi ya Habari Leo? Au ni yale yale ya Mkenya na Kova?
 
mwisho haya yote umekaribia ikiwa serikali ya ccm imeshindwa kulinda raia wake Mungu atatulinda na mwaka2015 watavuna wanachopanda
 
Sio kila kitu kinakwenda hivyo mkuu, naona ushaathirika na matukio

Sina imani na serikali na vyombo vyake vya usalama!! Naamini wanaweza kufanya lo lote kwa maslahi yao. Sisi wananchi hatuna thamani tena mbele ya serikali yetu na vyombo vya usalama. Nasisitiza, sina imani nao!!
 
:spy: Najaribu kusoma, kutafakari, kusikiliza na kujifunza nabaki njia panda sielewi nishike lipi au niamini kipi, je Vyombo vya Habari, wasemavyo wadau? Au niamini yasemwao na Viongozi? Nasimamia yafuatayo nikiamini yatanipa amani kwa sasa wakati nikiendelea kuiombea nchi yangu iliyokuwa ikisifika kama nchi ya kisiwa cha amani lakini kwa sasa nasitika kuendelea kuyaamini hayo kutokana na sitofahamu zinazoendelea nchini hivi sasa hali ambayo sikuzoea kuiona miaka ya nyuma.

sitaki niamini kuwa fujo, vurugu, kutokutii sheria kunafanywa na wendawazimu? la hasha bali kunafanywa na baadhi ya watu wanaotaka kusihi kwa kuburuzwa/ kushurutishwa kutii sheria? hainiingii akili Waziri aliyetoa tamko zaidi ya mwaka kuwa watu waliojenga maeneo yasiyostahili wavunje wenyewe na kuwapa muda wa kutosha kutekeleza hilo na wao kukaidi ili hali wakijua wamemwaga mamilioni ya fedha eneo lisilostahili leo wanajitokeza kifua mbele kuilaumu serikali eti inawaonea na tena kuwatisha wanaotekeleza sheria ili kutunza mazingira? Hapa kunatatizo?

Huenda wanaopelekwa mirembe sio wanaostahili ila hao wanaovunja sheria ili kupima nguvu ya serikali ndio wanastahili kwenda kupimwa uwezo wao wa kufikiri na kutenda?

Jamani hakuna kitu chenye thamani duniani kama amani? Watanzania wenzangu tunaenda wapi? Mungu ametupa akili na hekima za kujua mema na mabaya kwanini hatutaki kutumia akili zetu na kupima hili ni jema kweli leo hii tunaona yanayojiri Tanzania leo utasikia katekwa huyu katupwa mabwepande, kesho katishiwa huyu kuuwawa, kesho huyu katukanwa, mtondogoo huyu kashambuliwa, mara huyu kachoma kanisa, mara kakashifu dini ya mwingine, mara kalawiti,mara migomo, mara maandamano yasiyokuwa na vibali, mara ajali, mara kabaka, mara kaiba, mara kabambikiwa kesi kweli tutafika kwa kuendekeza haya?

Ndio watu tumekosa uzalendo na nchi yetu au ndio elimu tunayoipata inatupeleka puta? maana sitaki kuamini kuwa haya yote yanatendwa na wasiokuwa na elimu? hata polisi tukiwalaumu watashika mangapi jamani? serikali nayo inazidiwa? mimi naomba kila mtu aamue kuchukua hatua kwa kufanya yafuatayo:-

1. kusema moyoni mwake na kutenda anachokiamini yaani Kutii sheria bila shuruti.
2. kuiombea Tanzania amani.
3. kujipenda mwenyewe na kuwapenda wengine kwa kutenda mambo sahihi na mahali sahihi
4. kutimiza wajibu wake
5. kutokushadadia mambo tusiyoyajua au ambayo huna ushahidi nayo
6. kupenda kufanya kazi kuliko kukaa bila kazi
7. kupenda kujisomea vitabuu vya maarifa sio habari za udaku mf. sijui nani kafumamniwa hata ukijua hazitakusaidia.
8. kusaidia wengine wenye shida na kupeana ushauri kwa staha pale inapobidi.
9. kujiheshimu, kuheshimu uhuru wa wengine, na kuheshimu utawala unaoongoza nchi.
10. kuwa mzalendo kwa nchi yako kwa kusema mambo yenye kujenga na kuepuka kusema mambo yenye kubomoa.
11. kusema kweli daima na kuusimamia ukweli.
12. tembelea wagonjwa mahospitalini ili ujue thamani ya uhai ili uone umuhimu wa kutunza amani kwa afya uliyonayo ujue kunawanaoteseka kwa uzembe wa watu wachache waonaosababisha ajali zisizo za lazima, migomo inavyoondoa uhai,.nk

Naipenda nchi yangu, najipenda na nimeamua kuwa wa kwanza kuchukua hatua za kuishi kwa mujibu wa sheria za nchi bila shuruti wewe je wasubiri nini? tuachane na bendera fuata upepo. kunyoosheana vidole sana hakujengi ndugu yangu, badilika kubali kupokea ushauri na kuufanyia kazi kila inapobidi. najua wapo watakaosoma na kunidhihaki ila wapo wenye busara watakaosoma na kuchukua hatua chanya.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
 
hawa watakuwa magamba wenzao waliowavunjia zile nyumba sasa wanalipizia kisasi cha kuwatoa kafara kwa kuvunja nyumba zao.
 
Wakuu bado kuna walakini katika hili. Sitaki kabisa kuamini kauli ya Waziri mpaka tuone picha za huyu Mwanasheria na kama alijeruhiwa tuone. Tena atutajie kama polisi wanaendelea na uchungozi au la. Isije ikawa ni kutafuta justification ya kutekwa kwa Dr Ulimboka ili ionekane ni kitu cha kawaida kwa Wananchi. Bila haya maelezo bado sitaweza kuamini kama kweli Mwanasheria wa NEMC anatekwa tena bila polisi especially Kova kufuatilia wala kutoa statement ya kufanya uchunguzi. Hizi siasa za bono zitatuharibia TZ yetu tunayoipenda.
 
Hii habari iko kwenye gazeti gani zaidi ya Habari Leo? Au ni yale yale ya Mkenya na Kova?

Hamna iliyetekwa hapa mkuu..tena naona hili dili Kova ameamua kulipiga chini maana ameshashtukia tumekuwa wajanja sasa!! Usanii mtupu hapa!!!
 
Itafika stage tutasikia waziri pia kafanyiwa wanayofanyiwa watu hawa sijui tunaenda wapi nchi hii.
 
kazi kweli kweli, hii hali inatisha usalama wa maisha yetu. Hata ukiona mambo yanafanyika kinyume na sheria unakaa kimya kwa sababu ya woga wa kutupwa mabwe pande na kuingiliwa kinyuma na maumbile.

Mungu wetu! tushike mkono peke yetu hatuwezi.
 
SAKATA la ubomoaji majumba ya kifahari yaliyojengwa katika fukwe za Dar es Salaam limechukua sura mpya baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk Terezya Huvisa kufichua siri ya uhalifu.

Waziri amesema mbali na yeye kutishwa kuuawa, pia Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Heche Manchare ametekwa na watu wasiojulikana wakiwa wameficha nyuso zao kwa vitambaa na kumpiga kisha kumtelekeza eneo ambalo hakulitaja.

Tunaomba waliobomolewa majumba yao wachunguze haraka na waje na majibu ili tujue nani amehusika na ukatiri huu
 
Liwalo na liwe potelea mbali,...serkali yenye wafanyakazi wanaolipwa na kodi za wananchi wamekaa tu maofisini wanasubiri watu watumie mamilioni ya fedha waje wabomoe!...hatakama wanatumia sheria kiukweli inauma sana!!
 
SAKATA la ubomoaji majumba ya kifahari yaliyojengwa katika fukwe za Dar es Salaam limechukua sura mpya baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk Terezya Huvisa kufichua siri ya uhalifu.

Waziri amesema mbali na yeye kutishwa kuuawa, pia Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Heche Manchare ametekwa na watu wasiojulikana wakiwa wameficha nyuso zao kwa vitambaa na kumpiga kisha kumtelekeza eneo ambalo hakulitaja.

hii ndio Tanzania zaidi ya uijuavyo.
 
wala siwalaumu hao watu...kuvunjiwa nyumba sio kitu kidogo..mtu aende akaishi wapi saivi..
 
Waziri wa mambo ya ndani ameshindwa kazi aachie ngazi!

Kwa kweli serikali yetu aina mipangilio endelevu na sera imara kwani waziri akibadilishwa tu mwingine anakuja na sera yake yenye nguvu za soda,mbona serikali ya ccm mnatuchanganya sisi wenye nia njema na Tanzania?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom