Mwanangu Sema Amini

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,985
1,282
MWANANGU SEMA AMINI.
tanzania-590.jpg

1
Mwana ninaye kupenda, naomba sema amini,
Mungu anaye tulinda, akukinge na majini,
Wale wanao kuwinda, Rabi awabwage chini.
Namuomba Rahmani, akupe walau shinda.
2
Uvune ulichopanda, shuke moja themanini,
Kama ni nyavu watanda, uwe kingi baharini,
Iwe unafuga kunda, watotoe ishirini,
Namuomba Rahmani, akupe walau shinda.
3
Wanotaka kukuponda, wasiweze abadani,
Viumbe wafanya inda, hasa wale mafatani,
Mwanangu utawashinda, kwa uwezo wa Manani,
Namuomba Rahmani, akupe walau shinda.
4
Tazama unavyoenda, sema na wayo njiani,
Njia ni sawa kupinda, isikutoe imani,
Allah atakulinda, uishinde mitihani,
Namuomba Rahmani, akupe walau shinda.
5
Kiti usije kukonda, kwa kudekeza lohani
Yote unayoyatenda, yakufae maishani,
Usije ukawa punda, faida ya Baniani,
Namuomba Rahmani, akupe walau shinda.

Dotto Chamchua Rangimoto(Njano5)
0622845394/0784845394 Morogoro
 
Back
Top Bottom