Mwananchi wagoma kuchapa gazeti la dira sababu ya rostam!!

asha ngedere

Member
Nov 6, 2009
92
11
Wadau,
Habari za uhakika nilizozipata hivi punde zinasema kwamba, kiwanda cha uchapaji cha Mwananchi leo kimegoma kuchapisha gazeti la DIRA YA MTANZANIA.

Ofisa mmoja anaiyetwa Semu Kabugumila ambaye anahusika na masuala ya kiwanda amewagomea wamiliki wa gazeti hilo na kusema hatalichapa ingawa wakubwa wake hawana tatizo...mazungumzo yamefanyika lakini jamaa nasikia ameshikilia uzi, sababu anazozitaja ni kwamba kwanini awali lilikuwa linamilikiwa na Msama promotion na sasa linamilikiwa na dira media group. idara ya habari maelezo haina nongwa, ila jamaa nasikia haambiliki kabisa.

baadhi ya watu wanahisi kwamba huenda kwa sababu mwananchi (magazeti) ilikuwa ikimilikiwa awali na rostam aziz, balozi ruhinda na bm, na kwa vile gazeti hilo kwa siku za karibuni limefululiza kuandika habari zinazohusiana na rostam et al, basi kuna mkono wa rostam katika kuzuia kuchapishwa kwa gazeti hilo kupitia kwa huyo anayeitwa kabugumila.

lakini cha kushangaza ni kwamba, pamoja na pande hizo mbili kuingia mkataba wa maandishi, huyo kabugumila amekuwa akitoa taarifa za kutolichapa gazeti kwa kutumia simu ya kiganjani tu bila maandishi.

hii ndiyo taarifa ambayo wadau tunaweza kuijadili, kwani naona kama inatia hofu sana na kutishia uhuru wa habari nchini, kama ilivyotokea siku zile hujuma kwa gazeti la RAIA MWEMA.

Mjadala unakaribishwa.
 
Asha ngedere .... wewe ni mwandishi wa habari ... Duh yaani umechanganya chanaganya habari sijakuelewa kabisa
 
Gazeti la Dira lilichapisha kwa kina ile habari ya "jinsi Dowans walivyoizunguka Tanesco na Taifa".. go figure!
 
Kama ni kweli basi hiyo printing haus ya Mwananchi itakuwa inaendeshwa kienyeji mno... Huyo muhaya kabugumila anaamua tu kuzuia kuprint gazeti kwa kutumia simu ya kiganjani na kuinyima kampuni mapato na pia kuvunja mkataba halafu kampuni iwe inamuangalia tu??? Kweli Rostam kaiweka Tanzania mfukoni.
 
Kabigumila hajui Mwananchi wanauza hisa pale DSE? Ngoja tuone implication yake - kibiashara.
 
Kwani huyo Kabugumila anao wadhifa gani mpaka awe na nguvu za kusimama peke yake akasitisha mkataba ambao tayari umeishafungwa na kampuni. Kuna uwezekano mkubwa wa mleta habari hii, kutokuwa na ukweli kamili wa ni nini kinaendelea kuhusu suala hilo.
 
Hii itakuwa ni "taarifa zetu za kiintelijensia" Haiwezekani mtu mmoja azuie kuchapisha kitu ambacho kampuni kama Mwananchi imeingia mkataba. Mie naipotezea
 
Back
Top Bottom