Mwanamziki mwingine Msondo Ngoma afariki dunia

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,444
Muda si mrefu mwanamziki wa Msondo Ngoma Josee Maina amefariki dunia ndani ya daladala alikuwa akienda kurecord Sinza.
Poleni ndugu wa marehemu pamoja na mashabiki wa Msondo Ngoma.
More news to come.
 
Very sad, RIP Josee Maina. Poleni sana wapenzi wenzangu wa Msondo ngoma...."Mambo hadharani"
 
MWIMBAJI MAHIRI WA MSONDO NGOMA MUSIC BAND JOSEPH MAINA AMETUTOKA.
KIONGOZI WA BENDI HIYO MUHIDIN MAALIM GURUMO AMEIAMBIA GLOBU YA JAMII KWAMBA MEREHEMU MAINA AMEFARIKI MILANGO YA SAA MBILI UNUSU ASUBUHI AKIWA NDANI YA DALADALA SEHEMU ZA TEMEKE MIKOROSHINI.
GURUMO ANASEMA MAINA ALIKUWA NJIANI KUELEKEA STUDIO SEHEMU ZA OSTABEI AMBAKO MSONDO NGOMA INAREKODI ALBAMU MPYA. NYIMBO NNE ZIKO TAYARI NA MBILI ZIMESALIA NA MAREHEMU ALIKUWA ANAENDA KUTIA SAUTI.
GURUMO AMESEMA MIPANGO YA MAZISHI ITAJULIKANA BAADA YA NDUGU WA KARIBU WA MAREHEMU KUWASILI DAR. HIVI SASA MAITI YUKO HOSPITALI YA TEMEKE ALIKOPELEKWA MARA TU BAADA YA UMAITI KUMKUTA.
MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU PAHALA PEMA PEPONI
AMINA
https://www.jamiiforums.com/attachm...m/3621d1234875302-msiba-msondo-band-maina.jpg
habari na picha kwa hisani ya blog ya Michuzi
 

Attachments

  • MAINA.jpg
    MAINA.jpg
    23.4 KB · Views: 356
MWIMBAJI MAHIRI WA MSONDO NGOMA MUSIC BAND JOSEPH MAINA AMETUTOKA.
KIONGOZI WA BENDI HIYO MUHIDIN MAALIM GURUMO AMEIAMBIA GLOBU YA JAMII KWAMBA MEREHEMU MAINA AMEFARIKI MILANGO YA SAA MBILI UNUSU ASUBUHI AKIWA NDANI YA DALADALA SEHEMU ZA TEMEKE MIKOROSHINI.
GURUMO ANASEMA MAINA ALIKUWA NJIANI KUELEKEA STUDIO SEHEMU ZA OSTABEI AMBAKO MSONDO NGOMA INAREKODI ALBAMU MPYA. NYIMBO NNE ZIKO TAYARI NA MBILI ZIMESALIA NA MAREHEMU ALIKUWA ANAENDA KUTIA SAUTI.
GURUMO AMESEMA MIPANGO YA MAZISHI ITAJULIKANA BAADA YA NDUGU WA KARIBU WA MAREHEMU KUWASILI DAR. HIVI SASA MAITI YUKO HOSPITALI YA TEMEKE ALIKOPELEKWA MARA TU BAADA YA UMAITI KUMKUTA.
MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU PAHALA PEMA PEPONI
AMINA
https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=3621&stc=1&d=1234875302
habari na picha kwa hisani ya blog ya Michuzi

Mod tafadhali iunganishe na ile ya awali, natanguliza shukrani
 
RIP Maina,Pole kwa ndugu, jamaa,marafiki na wapenzi wote wa Msondo.

Naomba taarifa kwa yoyote anayefahamu ni kwanini vifo vimekuwa vikiwaandama sana wanamuziki wa Msondo hasa safu ya waimbaji.
 
Mods tunaomba uiunganishe na ile ya awali tayari ipo hewani.
 
- Hii ni habari ya kusikitisha sana, mimi kama mpenzi mkubwa sana wa Msondo Ngoma ninatoa slaam za rambi rambi kwa wafiwa ni habari nzito sana kuikubali lakini ndio ukweli, Mungu amuweke mahali pema na pia Msongo iendelee.

- Tutamkumbuka Maina siku zote wka sauti yake saafi ya kutoa nyoka pangoni, hasa kwenye kibao cha "usia wa mama", poleni sana wazee wa Ilala, wazee wa Amana, na wazee wote wa Msondo Ngoma hili pigo kubwa sana kwa bendi yetu.

Mungu ambariki marehemu.
 
...Tuombe Mwenyezi Mungu amkubalie toba zake na amsamehe madhambi yake, na amlaze pahala pema, ...Yeye ametutangulia nasi tu njiani.

Amen.
 
Ni maskitiko Makubwa....kwa wanamsondo na watanzania wote kwa ujumla...naipenda sana Msondo...M/Mungu ailaze roho ya marehemu pahala pema peponi.
 
Mwanamuziki Msondo Ngoma afia kwenye daladala Dar
Na Ibrahim Bakari

MWANAMUZIKI mahiri wa Msondo Ngoma, Joseph Maina amefariki ghafla jana asubuhi akiwa ndani ya daladala.

Dereva wa basi la daladala lenye namba za usajili T582 AFL linalofanyika safari kati ya Mwenge na Temeke Mikoroshoni, Kassim Salum aliiambia Mwananchi jana kwenye Hospitali ya Temeke kuwa msanii huyo alifariki akiwa amekaa kiti cha mbele mlangoni.

"Unajua aliwahi kuingia, na sisi ilikuwa zamu yetu kupakia hapo Temeke Mikoroshoni, kulikuwa na abiria anataka kupanda, nilipomwambia asogee kiti cha kati, nikaona anakakamaa na muda mfupi akalala.

"Baada ya kuona hali ile, watu walijaa na niligeuza gari hadi kituo cha polisi Maghorofani, lakini na wao walinipa askari wakaniambia tuelekee hospitali ya Temeke," alisema Salum.

Hata hivyo, mwili wa Maina ulibakia kwenye kiti cha daladala kwa takriban saa nzima katika hospitali hiyo huku mashabiki na watu wengine wakielezea kumfahamu kama ni Maina.

Mwananchi ilifika hospitalini hapo na kukuta umati wa watu wakielezea masikitiko yao kutokana na kifo hicho.

Saa 7:11 mchana, kiongozi wa Msondo Ngoma, Muhidin Maalim Gurumo aliiwasili akifuatana na mpiga solo, Said Mabera, wacheza shoo na wanamuziki wengine.


Hata hivyo, wasimamizi wa chumba cha maiti walimruhusu Mabera kwenda kutambua mwili na aliporudi alithibitisha kuwa kweli ni Maina.


Gurumo alisema kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na miguu na bendi walikuwa wakiandaa utaratibu wa kumtafutia matibabu.


"Kwa kweli ni pigo kubwa kwani Maina alishiriki katika nyimbo zote za Msondo, alishiriki albamu zote ni pigo kwa sasa hatuna la kusema tutatoa taarifa," alisema.


Maina ambaye ameacha mke na watoto wa wawili alitunga kibao kumuimbia mke wake, Mama Cossy ambacho hakijatoka.


Maina ameongeza pengo la wanamuziki wakali wa bendi hiyo waliofariki miaka ya karibuni, akiwemo TX Moshi William, Athumani Momba na Suleiman Mbwembwe.
 
Alikuwa zenji pamoja na bendi ya msondo siku \ya ufunguzi wa tamasha la sauti za busara. Nakumbuka alikuwa anachechemea kudhihirisha kweli alikuwa na maumivu ya miguu. Haya mapigo ya pigo yataisha lini??? nasikia wajamaa wanatoana kafara. au ndo yale ya Rita Manlrey dhidi ya The wailers crew ndo yanatokea hapa?
Apumzike salama Maina
 
Msondo ni Baba ya Muziki hivyo Maina ni Mmoja wa waliofanikisha Msondo kupata heshima hiyo.
Alikuwa nayo toka enzi za Nuta Jazz-Juwata Jazz-Ottu mpaka sasa Msondo Mgoma.
Raha ya Milele Umpe Eee Bwana,
Na Mwanga wa Milele Umwangazie,
Apumzike kwa Amani......Amen.
 
Kifo cha mwanamuziki:Msondo wasimamisha maonyesho wiki moja


BENDI ya Msondo Ngoma, imesimamisha maonyesho yake kwa wiki moja kufuatia kifo cha mwanamuziki wake, Joseph Maina aliyefariki ghafla jana kwenye daladala.


Kiongozi wa bendi hiyo, Muhidin Maalim Gurumo, aliiambia Mwananchi jana kuwa hatua hiyo inatokana na wanabendi kuheshimu mchango wa marehemu Maina pamoja na kutumia nafasi hii kuomboleza.


“Tumesimamisha maonyesho yetu, kwa kipindi hiki nawataka mashabiki wetu kuwa watulivu na wastahimilivu katika kipindi hiki kigumu,” alisema Gurumo.


Habari zilizopatikana baadaye jana zilisema kuwa mwili wa Maina unatarajia kusafirishwa kwenda Tanga kwa mazishi yatakayofanyika kijijini kwao Mkuzi, Muheza Tanga baada ya heshima za mwisho zitakazotolewa leo nyumbani kwa kaka yake, Kurasini, Dar es Salaam.


Maina alifariki ghafla juzi asubuhi akiwa ndani ya basi la daladala lenye namba za usajili T582AFL linalofanyika safari zake, Mwenge na Temeke Mikoroshoni.


Gurumo alisema kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na miguu na bendi walikuwa wakiandaa utaratibu wa kumpatia matibabu.


"Kwa kweli ni pigo kubwa kwani Maina alishiriki katika nyimbo zote za Msondo walizopiga, alishiriki albam zote ni pigo kwa sasa hatuna la kusema tutatoa taarifa," alisema.


Maina ambaye ameacha mke na watoto wa wawili alitunga kibao kumuimbia mke wake, Mama Cossy ambacho hakijatoka.


Maina ameongeza pengo la wanamuziki wakali wa bendi hiyo akiwemo TX Moshi William, Athumani Momba na Suleiman Mbwembwe ambao tayari wamefariki.
 
Back
Top Bottom