Mwanamke wa Tunisia Apata Mimba ya Mapacha 12

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
2844766.jpg

Mwanamke mmoja wa nchini Tunisia ana Mimba ya watoto 12 Tuesday, August 18, 2009 8:40 AM
Mwanamke mmoja nchini Tunisia ana mimba ambayo ambayo haijawahi kutokea duniani ya watoto mapacha 12. Mwanamke huyo ambaye ni mwalimu katika shule moja nchini humo amevunja rekodi ya dunia kwa kuwa na mimba ya mapacha 12 lakini hata hivyo madaktari wameonya kuwa kuna uwezekano mdogo wa mtoto hata mmoja kuzaliwa akiwa hai.

Mwanamke huyo ambaye jina lake halikutajwa aliamua kutumia njia ya kupandikizwa ujauzito ya IVF baada ya kupata mimba mara mbili na mimba zote hizo kuharibika.

Mwanamke huyo hivi sasa ana mimba ya watoto mapacha 12, watoto wa kike sita na wa kiume sita.

Ikiwa mwanamke huyo atafanikiwa kutimiza azma yake ya kuwazaa watoto hao wote kwa njia ya asili bila kufanyiwa upasuaji, basi atakuwa amevunja rekodi ya mwanamke mmoja ambaye alizaa watoto tisa mapacha kwa njia ya asili.

"Ninachotaka ni kuwakumbatia watoto wangu na kuwaonyesha mapenzi yangu kwao" aliwaambia wafanyakazi katika hospitali moja kwenye mji wa Gafsa.

"Hii ni kama miujiza na tunaona kama tumebarikiwa baada ya kuhangaika sana kupata watoto".

Mume wa mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Marwan, alisema kwamba anasikia furaha kupita kiasi baada ya kusikia taarifa hiyo.

"Mwanzoni tulifikiri kwamba alikuwa na mimba ya watoto wawili mapacha" alinukuliwa Marwan akisema.

"Lakini jinsi tulivyosikia habari kwamba vichanga zaidi vimegunduliwa, furaha yetu ilizidi kuongezeka".

Hata hivyo wataalamu wa uzazi wamesema kwamba kuna uwezekano mdogo sana wa watoto hao kuzaliwa wakiwa hai.

Mmoja wa madaktari waliohojiwa alisema kuwa kuna uwezekano wa asimilia 1 kati ya 100 mtoto hata mmoja kuzaliwa akiwa hai.

"Inawezekana mtu kuwa na mimba ya watoto 12 kwa kipindi fulani lakini si kwa muda mrefu" alisema Peter Bowen-Simpkins, mtaalamu wa mambo ya uzazi wa Uingereza.

"Tatizo ni kwamba mji wa mimba hauna uwezo wa kubeba watoto wote hao 12"

"Watoto hao wanaweza wakawa hai tumboni katika kipindi cha wiki 22 hadi 23, wanahitaji matunzo ya kidaktari ya hali ya juu sana" alisema mtaalamu huyo.

Mimba ya mwanamke huyo wa Tunisia, imefananishwa na mimba ya Nadya Suleman wa Marekani "Octomum" ambaye alijifungua watoto nane, sita wa kiume na wawili wa kike kwa njia ya upasuaji, mwanzoni mwa mwaka huu.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2844766&&Cat=7
 
2844766.jpg

Mwanamke mmoja wa nchini Tunisia ana Mimba ya watoto 12 Tuesday, August 18, 2009 8:40 AM
Mwanamke mmoja nchini Tunisia ana mimba ambayo ambayo haijawahi kutokea duniani ya watoto mapacha 12. Mwanamke huyo ambaye ni mwalimu katika shule moja nchini humo amevunja rekodi ya dunia kwa kuwa na mimba ya mapacha 12 lakini hata hivyo madaktari wameonya kuwa kuna uwezekano mdogo wa mtoto hata mmoja kuzaliwa akiwa hai.

Mwanamke huyo ambaye jina lake halikutajwa aliamua kutumia njia ya kupandikizwa ujauzito ya IVF baada ya kupata mimba mara mbili na mimba zote hizo kuharibika.

...ndio maana siifagilii hiyo IVF,...kwa tamaa zao utaona wanang'ang'ania kuzaa na kusingizia eti ndio Mw' Mungu alivyotaka, kumbe anajua 'anauza' story.

...kwanza alikubalije hizo embroys zote 12 zipandikizwe? upuuzi mtupu!
 
Ingekuwa natural hapo ingekuwa poa, lakini kwa kupanikizwa ahhaa
 
Back
Top Bottom