Bazazi
JF-Expert Member
- Aug 18, 2008
- 2,806
- 3,476
Walakini mambo yamebadilika sasa. Kazi ya mwanamke sio utii. Hutaka usawa wa cheo na wa haki. Mwanamke wa sasa ni asi. Si vibaya kwa kadri mambo yaendeleavyo, lakini kujichukulia kibubusa – kama kipofu – kila litendwalo na mwanaume ili kuonyesha ulimwengu kuwa ana usawa ni upuzi pengine. Wanawake wameanza kuvuta sigara kwa sababu wanaume wanavuta. Huvaa suruali na mashati kwa sababu wanaume huvaa. Matokeo yake ni fujo kubwa. Hujui nani mwanaume au nani mwanamke!
Mipaka ya nguvu za mwanamke, hali hafifu, kuchoka upesi na moyo dhaifu humfanya hafai kwa kazi ngumu. Mwanamke ni malaika wa roho. Na apate usawa wa haki na wa cheo, lakini daraka lake katika maisha ni la Mapenzi, Huruma, Sanaa na hifadhi.
NB
- mtemedeni = aliyestaarabika, aliyeendelea
- asi = kutotii
- kibubusa = kipumbavu, kipofu, kama kipofu.
Shaaban Robert (1967). Diwani ya Shaaban 5: Insha na Mashairi. Thomas Nelson and Sons Ltd. Dar es Salaam. 105pp.