Mwanamke wa kitanzania na changamoto katika Ujasiriamali

afu cha kwako??
Lakini je, una ndoto kubwa kubwa??

Maana wakati mwingine ukiwa majukumu makubwa yanakufanya uwe na ndoto kubwa pia.

cha kwangu changu na nitaongezea kununua nguo za ndani, sabuni, mafuta ya kupaka, chumvi, pilipili na viungo vya pilau, pencils, diaries, flowers, greetings and post cards, perfumes na udi, night dresses, mashuka na vyombo jikoni.

Kuhusu kuota, sijawahi kuota na kama ninaota basi sikumbuki nilichoota.
 
Kuna mdada mmoja mtaani kwangu ana salon ya wanawake na anauza vocha za simu hapo hapo, katika hali ya kumuonesha kumuunga mkono huwa sinunui vocha sehemu nyingine yoyote ile, ninachokifanya mimi ata niwe mbali huwa nampigia simu ananiingizia kwenye line nitakayomuelekeza maana line zangu zote anazo.

Sasa kituko ni majuzi tu niliishiwa internet bundle saa nne usiku, nikampigia simu aniingizie airtime kwenye line ya Airtel akanijibu hana za kurusha zimekwisha, nikamwambia kwanguwa hiyo vocha unitumie kama text msg akaniambia simu yake ya tigo imeisha pesa, na yeye ndio muuza vocha, hivi mwanamke wa type hii tumuwezeshe kwa njia ipi?
 
Mara nyingi wanaume huwa wanasaidiana sana kwenye bishara. kasheshe ni kwa kina mama kusaidiana wenyewe kwa wenyewe.

Wapo wanawake wanaosaidiana kibiashara, najua kuna wanawake wanaenda Dubai, China kuchukua nguo, wanafundishana, wanaelekezana na kupelekana bila kusahau kutumana mizigo. Hayo yalikuwa sana zamani lakini kwa sasa tunaelimika na kwa kutumia mada kama hizi tunazidi kufunguka. Wale ambao bado wana tabia hizo basi hawajaingia kwenye biashara, katika biashara kuwa na network kubwa na nzuri ni sehemu ya mafanikio. Na network hii ni ya wafanyabiashara wenzako pamoja na wateja, hapo huna jinsi!
 
Kongosho,

Katika sababu zote ulizotowa naweza kukubaliana na namba 7 tu, na taboo hiyo wengine tulishaigaragaza.
 
Nadhani mwanamke kama mwanamke ukiamua kusimama mwenyewe unaweza. Tatizo ni mipango madhubuti pia utekelezaji.

Kwangu mimi information ni kitu muhimu sana kwenye ujasiriamali ambapo lazima niwe nimefanya market research ya kile nilichodhamiria kufanya hapo hapo tayari nimejipanga na business plan yangu nikiwa najua A-Z ya kila kitu huku resorces zikiwa zimekamilika.

Kuwa mjasiriamali siyo tu kufuata upepo wa wengine wanafanya au wanafanya nini..Inahitaji uwe mbunifu na uje na kitu tofauti ili uweze kuwa na utofauti na hata kama ni kitu kipo tayari uje kitofauti, ujue SWOT analysis za unachotaka kufanya.

Ujasiriamali unahitaji uwajibikaji wa hali ya juu, uvivu uwe pembeni na kuwa well organized na mambo yako. Changamoto kadhaa hazikosekani, je unapambanaje nazo? siyo kuona 1st quarter umepata loss basi unaanza ku-give up hapana kuna miteremko yake kwenye ujasiriamali. Inabidi ujue wapi pa kuziba ufa au wapi pa kurekebisha.

Jambo lingine ni customer care..ambapo bongo ni mtihani kweli kweli..yaani mtu unaweza kuwa mjarisiamali tatizo unaringa ringa, vutia wateja na wape service inayotakiwa..kuwa creative na ideas mbali mbali..it makes a difference watu hawajui tu!!
 
Tatizo wanawake hawapo serious mara nyingi.

Mara ngapi ushaenda ofisini ukamkuta sekretari mwanamke anaongea na simu nusu saa hajakuhudumia au kukusikiliza? mara ngapi ushaenda serikali iwe wizara ya ardhi, manispaa nk ukamkuta mwana mama anapaka rangi kucha?

Mara nyingi mimi nikienda ofisi ya serikali nikikuta wamama huwa naanza kuhofia kwamba hapo huduma hamna. Ni rahisi sana kwake kukujibu njoo wiki ijayo bila kufanya pilika pilika hata uone effort ya kutafuta hiyo kitu au kuulizia kwa mwenzake. Hata wanawake wenyewe mnajua kwamba huduma za mwanamke ni kimeo na kama ni restaurant yani kwa usafi mara kumi ukute wahudumiaji na wapishi wanaume.

Kuna kazi moja nilipewa nilipataga challenge sana sababu timu ilikuwa na wanawake kama 10 wanaume 2 , kila siku ugomvi yani muda mwingi naamua ugomvi na kushitakiana badala ya kufanya kazi za msingi. Baada ya miezi 6 kwa msaada wa HR nilifumua fumua nikabakisha wadada 2 ambao ni wapya si katika wale wa mwanzo mambo yakawa shwaaaari.Ni baada ya hapo kila nikiulizwa preference ktk kuongeza staff nawaambia lete MALE maana anakuja dogo fresh kutoka chuo lakini after 3 months anapiga kazi kuliko mdada mliokuwa nae 3 years.
 
Thank you very much Kongosho....Nimeipenda hii thread, ina utafiti na analysis nzuri sana kwa sisi kina mama wa kitanzania....umegusa kila angle hata sina la kuongeza....mwendo ndo huu si kila siku mapenzi hapa!
 
Tatizo wanawake hawapo serious mara nyingi.

Mara ngapi ushaenda ofisini ukamkuta sekretari mwanamke anaongea na simu nusu saa hajakuhudumia au kukusikiliza? mara ngapi ushaenda serikali iwe wizara ya ardhi, manispaa nk ukamkuta mwana mama anapaka rangi kucha?

Mara nyingi mimi nikienda ofisi ya serikali nikikuta wamama huwa naanza kuhofia kwamba hapo huduma hamna. Ni rahisi sana kwake kukujibu njoo wiki ijayo bila kufanya pilika pilika hata uone effort ya kutafuta hiyo kitu au kuulizia kwa mwenzake. Hata wanawake wenyewe mnajua kwamba huduma za mwanamke ni kimeo na kama ni restaurant yani kwa usafi mara kumi ukute wahudumiaji na wapishi wanaume.

Kuna kazi moja nilipewa nilipataga challenge sana sababu timu ilikuwa na wanawake kama 10 wanaume 2 , kila siku ugomvi yani muda mwingi naamua ugomvi na kushitakiana badala ya kufanya kazi za msingi. Baada ya miezi 6 kwa msaada wa HR nilifumua fumua nikabakisha wadada 2 ambao ni wapya si katika wale wa mwanzo mambo yakawa shwaaaari.Ni baada ya hapo kila nikiulizwa preference ktk kuongeza staff nawaambia lete MALE maana anakuja dogo fresh kutoka chuo lakini after 3 months anapiga kazi kuliko mdada mliokuwa nae 3 years.

Maundumula usitubanie ajira kisa umekutana na performance mbovu za wadada/ wamama. Ujue hilo limetokana na back ground zetu hapo ninamaanisha mila na desturi ambazo tumelelewa. Hatujalelewa kuwa wapiganaji ingawa kwa sasa serikali, NGOs zimetambua hayo na zinakuja na miradi tofauti ili kubridge the gap. Wale ambao ulishawafukuza hawapo, sasa huoni kama ukimuajiri dada aliyetoka chuo ndiyo unanafasi nzuri ya kumtengeneza ili awe tofauti na wale waliopita!
 
Muinjilisti,

Sikuwafukuza mkuu sikuwa na mamlaka hayo, hata HR mwenyewe asingeweza kuwafukuza maana si kitu rahisi lakini kilichofanyika ni kuwatafutia departments nyingine wakatawanywa katika sehemu ambazo less sensitive na kwenye wanaume wengi kwahiyo kule kukaa mbali from each other na kuwa surronded na wanaume kwenye timu za mchanganyiko kuliwawasaidia sana hata wao na walifanya vizuri.Bahati nzuri hata hawakunichukia mwisho wa yote kwakuwa na wenyewe walikuwa wamechokana.
 
@maundumula

nadhani hapo naona kuna vitu viwii, kuna mapungufu ya female specie na business culture.

Ukilinganisha ufanisi wa kazi kati ya mwanamke na mwanamme walio katika sekta au ofisi moja wanaweza tofautiana ufanisi hasa mwanamme kuibuka kidedea.

Mfano ulotoa wa sekretary serikalini, naiangalia kama business culture ya utendaji wa kazi serikalini ni tofauti.
Hebu chukua sekretary mwanamke wa serikalini na sekretari mwanamke wa private sector halafu linganisha ufanisi wao wa kazi.
Yule wa psrivate sector ana nafasi kubwa sana ya kuwa bora kushinda wa serikalini.
 
FF nadhani unasema hayo sababu wewe unaweza kuwa umeshapata experience ya kutosha na mwamko mkubwa katika hili

hebu mfikirie mwanamke wa kawaida kabisa wa kitanzania.
Mi naona nloyataja kwa namna moja yanamgusa.

Tupe experience hiyo no 7 umeigaragazaje?

Kongosho,

Katika sababu zote ulizotowa naweza kukubaliana na namba 7 tu, na taboo hiyo wengine tulishaigaragaza.
 
@maundumula

nadhani hapo naona kuna vitu viwii, kuna mapungufu ya female specie na business culture.

Ukilinganisha ufanisi wa kazi kati ya mwanamke na mwanamme walio katika sekta au ofisi moja wanaweza tofautiana ufanisi hasa mwanamme kuibuka kidedea.

Mfano ulotoa wa sekretary serikalini, naiangalia kama business culture ya utendaji wa kazi serikalini ni tofauti.
Hebu chukua sekretary mwanamke wa serikalini na sekretari mwanamke wa private sector halafu linganisha ufanisi wao wa kazi.
Yule wa psrivate sector ana nafasi kubwa sana ya kuwa bora kushinda wa serikalini.

Nakubaliana na wewe, lakini ninachozungumzia hapa ni mwanamke VS mwanamme kwenye mazingira yanayofanana.

Kuna mambo kama uzazi ambao wanawake wengine hutumia kama excuse lakini si kweli wapo wamama maofisini yani akienda kujifungua mnamsubiri kwa hamu kwakuwa hamna watu wanaoweza kuziba pengo na akirudi tu from day one tofauti inaonekana. Kwahiyo kimsingi walio wengi ni kujiendekeza tu.
 
Siku hizi wanaanzisha vituo vya kulea watoto yatima. Naona hii business inalipa maana viko kila kona na mtaa na wamiliki wake ni wa mama
 
Hivi kama mwanamke umeolewa mumeo akifanikiwa si umefanikiwa na wewe?Au kwanini usimsaidie kufanikiwa kwa ushauri halafu wewe ukafanya majukumu yako ya kuhakikisha usalama wa familia?
 
hali inazidi kuwa ngumu, full kudaiwa 'facilitation fee'
 
Kwanini wanawake wasaidiwe wakati kila siku tunaambiwa wanawake wanaweza!!?? ni % chache sana ya wanawake ambao wanasupport familia wakiwa na kipato, so kwa upande wangu sioni tofauti ya mwanamke kuwa mama wa nyumbani au kuwa mfanyakazi/ mjasiliamari.

Pesa ya mwanamke ni ya mwanamke, lakini pesa ya mwanaume ni ya wote. nina experience ya kutosha kuhusu jambo hili, wanawake wa Kibongo wengi wao ni tatizo.

U have hit the truth. Inauma sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom